Tahadhari kwanza kabla ya madhara

Tahadhari kwanza kabla ya madhara

Username 20

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
741
Reaction score
1,513
Kwanza kabisa natoa pole za dhati kwa ndugu zetu wote walioondokewa na wapendwa wao, sote njia yetu ni moja. Tulitoka kwake na kwake tutarudi

Naomba kuwatahadharisha na hawa watu, roho yangu inaniambia sio watu salama

Mange kimambi amekuwa mstari wa mbele sana kuibua uozo wa serikali ikiwemo kutoa nyaraka nyeti (tusijadiri sana kuwa anazipataje).

Lakini roho yangu inaniambia anahusika na kuwabaini watu wanaoipinga serikali hasa hasa walio kwenye nafasi nyeti

Kwanini nasema hivyo, ni kwamba Mange amehusika kuhujumu,

1: Kauaminisha umma kuwa JWTZ wapo pamoja na raia na kwamba waliofanya mauaji ni askari kutoka Uganda (hii naamini ni propaganda imetumika kulinda majeshi yetu yasiomekane ni maadui wa raia)

2: Baada ya utulivu kurejea katumika pia kuzuia taarifa kuonea kwa kuwatisha watu wasiongee kawaida kuwa TCRA inasikiliza mazungumzo wakati huo huo mtandao ukawa upo chini maana ake huwezi kutuma picha wala video lkn pia hutakiwi kutoa taarifa kwa kupiga simu kawaida

Idara ya TISS imekuwa ikiajiri watu wake nyeti kutoka familia za watu wale wale waliotumikia idara hasa vitengo nyeti, kama baba yako au mama yako hakuwahi kuwa mkubwa kitengo fulani huwezi kuajiriwa sehemu nyeti kwenye idara ya TISS

Vinginevyo utabakiwa kuajiwa TISS kitengo cha chini sana na utaishia kuwa mlinzi tu wa viongozi ama dereva wa magari yao

Nadhani mpaka hapo mnaweza kuwaza Mange ametoka familia gani na anazipataje nyaraka hizo

Sasa kazi kwenu nyie endeleeni kumpa taarifa mkiamini ana uadui huo na serikali

Pia kuna huyu bwana wa kuitwa Kepteni TESHA, huyu ndio kahusika kumpata na kumpoteza Barozi Polepole

Alijitokeza na kujifanya anaikosoa serikali na kuwa kamuandikia barua mkuu wake (CDF) kumtaarifu kuwa haungi mkono mambo yanaoendelea, akaaminisha kabisa kuwa asilimia kubwa ya jeshi haliungi mkono na kuwa kuna uwezekano wa jeshi kuchukua nchi

Hapa bwana Polepole alijaa mzima mzima akatoa mpaka location akiamini huyu bwana ni mwenzake

Ni nani alitoa detail za kuuaminisha umma kama kweli Tesha ni mwajiriwa wa jeshi, namba yake ya kazi jeshini, intake nk.

Kwanini zilitolewa haraka vile lkn pia kwann jeshi halikumkana, bado alietoa taarifa ya JWTZ akawa ni aliekuwa mpambe wa rais Magufuri

Huu ulikuwa ni mchongo wa kufanikiwa kuwadaka bwana Polepole na askofu Gwajima

Sema walikurupuka tu kumdaka Polepole, Gwajima akawa kasanuka lkn wangetulia kidogo walikuwa wanawadaka wote

Kuukosoa uongozi wako jeshini ni uasi vipi ni hatua zipi zimechukuliwa kwa kepten Tesha JWTZ wamehusika moja kwa moja kwenye siasa za nchi hii na wanatakiwa kuubeba huu msalaba ukizingatia pia walichangia mpaka mabasi na helkopta kwenye kampeni za CCM

Mwisho usiamini sana wakosoaji au wapinzani ukadhani ni kweli wanakosoa kwa dhati wengine mamluki tu wanafanya ili waujue uliko upinzani wa kweli na waumalize,

Ni nani alimjua Mzee Ally Kibao kabla ya kifo chake alikuwa na madhara gani kwa serikali kwanini aliuwawa, vp mnahisi Mbowe hahusiki?

Ile press ya Godbless Lema January kabla ya uchaguzi wa ndani wa CHADEMA mnadhani zile detail alizotoa alizipata wapi, lkn aliahidi atarudi na akirudi mambo yatakuwa hadharani ni mambo yapi hayo na alilenga kumfunua nani?

Siku iwe njema kwetu sote, wapumzike kwa amani wote waliondoka na sakata hili la maandamano,
Mungu ibariki Tanzania
 
Maelezo mengi ila umeandika takataka tu.

Wewe ni mlamba asali na unatetea walamba asali wenzako.
 
Unaongea na pia unaandika ila nikueleze bado haujui chochote katika Mambo ya intelejensia hivyo subiri ratiba mpya ya kuandamana tukapambane tena hayo ya uchambuzi wa kiintelejensia waachie wachumia tumbo akina Yericko nyerere wenye ndoto za kuwa majasusi ila wameishia kuwa watizamaji wa Mambo ya usalama pasina kuhusika na chochote .

Ahsante
 
Back
Top Bottom