Tahadhari kwa watumiaji wa bodaboda Dar

Tahadhari kwa watumiaji wa bodaboda Dar

Ile Picha ya mkuu wa mkoa nayo haiwezi kutumika kama ushahidi???

MAKONDA.jpg

Uungwana ni vitendo, kama kweli gurudumu zilikuwa zinazunguka basi ingependeza naye akaungana na hao waliojazana bonde la Msimbazi!!
 
Kofia ngumu ni kwa usalama wako kama anayo moja vaa ww yy aendeshe bila helmet
 
Kuna kamata kamata inaendelea katika Jiji la Dar kwa kwa watumiaji wa boda boda ambao hawatumii Helment.

Polisi kwasasa wanakamata dereva na abiria kama wakiwakuta mmepanda piki piki bila kuvaa Helment.

Ukikamatwa kwa makosa mengine unaweza kutozwa faini barabarani lakini kwa hili la helmet ni lazima abiria na dereva wako muende mkalale rumande na kisha mtapelekwa mahakamani kufunguliwa mashtaka.

Mahakamani kuna fine, kifungo cha miezi sita, au vyote kwa pamoja. Hali hii imesababisha usumbufu mkubwa na upotevu wa fedha na muda kwa mambo ambayo yanaepukika.

Tafadhali ili kukwepa kukutana na kadhia hii, usimpakie abiria ambaye hataki kuvaa Helment, abiria usipande boda boda kama hana Helment kwa ajili yako.

POLISI KATIKA HILI HAWANA MZAHA, TAFADHALI SHARE KUWASAIDIA NA WENGINE.
Helment ni nini?
 
Je!! Kiafya Suala La Abiria Wote Kutumia Kofia Moja Limekaaje?? Ukizikatia Kofia Hizi Zitakuwa Zinavaliwa Na Dada Zetu Wenye Nywele Zenye Dawa.
Ni kwasababu watanzania tumekuwa sio wabunifu tu lakini tunaweza kabisa kupokezana helmet bila madhara yoyote. Kwa mafano wenye boda boda wanaweza kutemebea na vitambaa vingi visafi ambavyo watampa mvaaji ili atangulize kichwani kabla ya kuvaa helmet. Akiwa na vitambaa eg vyeupe kama dozen moja vinamtosha kabisa kumpa kila mpandaji chake. Na baada ya matumizi jioni anakifua na kupiga pasi tayari kwa kesho yake.
 
Back
Top Bottom