Tahadhari kwa watumiaji wa bodaboda Dar

DAMAS DAMIAN

Senior Member
Apr 8, 2011
115
54
Kuna kamata kamata inaendelea katika Jiji la Dar kwa kwa watumiaji wa boda boda ambao hawatumii Helment.

Polisi kwasasa wanakamata dereva na abiria kama wakiwakuta mmepanda piki piki bila kuvaa Helment.

Ukikamatwa kwa makosa mengine unaweza kutozwa faini barabarani lakini kwa hili la helmet ni lazima abiria na dereva wako muende mkalale rumande na kisha mtapelekwa mahakamani kufunguliwa mashtaka.

Mahakamani kuna fine, kifungo cha miezi sita, au vyote kwa pamoja. Hali hii imesababisha usumbufu mkubwa na upotevu wa fedha na muda kwa mambo ambayo yanaepukika.

Tafadhali ili kukwepa kukutana na kadhia hii, usimpakie abiria ambaye hataki kuvaa Helment, abiria usipande boda boda kama hana Helment kwa ajili yako.

POLISI KATIKA HILI HAWANA MZAHA, TAFADHALI SHARE KUWASAIDIA NA WENGINE.
 
Nimeiona hiyo pale bonde la msimbazi dereva wa bodaboda na abiria wao wote wamejazana kwenye defender za polisi...Tutii SHERIA
 
haya wamesikia
 
haki ya nani pikipiki ikisimamishwa nitakimbia zaidi ya mjamaica Bolt
 
Amri ilishatolewa na mkuu wa mkoa P, Makonda kuwa ukipanda pikipiki bila helmet ni kosa la kutaka kujiua.

Kwahivyo ni sawa tu.. kwa usalama zaidi barabarani
 
kaka niliishi dodoma hii sheria ilifuatwa sana 2014/15 ila sasa naona imelegea kidogo.Ilifika mahali dereva anakwambia vaa helment la sivyo siendi.nilipenda sana
Ukumbuke huu utawala kiboko ya wabishi
 
Back
Top Bottom