Tahadhari kwa namba hizi

Tahadhari kwa namba hizi

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
102,676
Reaction score
126,848
Wakuu heshima zenu,

0787-332977 Samweli, 0689-694153 Shabani A.K.A Dr na 0787-407501 (Mzungu)

Tahadhari kwa hizi namba tajwa hapo juu.

Siku ya Jumatano tarehe 19/10/2016 saa 3 asubuhi alinipigia bwana mmoja anajiita Samweli (0787-332977) akanitaja kwa jina nilosajili kwenye line yangu ya airtel na kuniuliza leo hujaenda kazini? Nikajibu ndiyo nipo home, akasema mimi naitwa Samweli(Mkurungezi wa kampuni nipo Dodoma) naomba uende AICC Hospital utamkuta Dr Shabani(0689-694153) mwambie Samweli ameniomba nisimamie mzigo wake wa dawa boxes 40 akataja jina gumu la dawa silikumbuki vizuri kila box shilingi 400,000 x 40 = 16,000,000.

Kuna mzungu anatokea KIA nakutumia no yake mara moja atakupigia mwambie wewe ni mwakilishi wa Kampuni na atakukabidhi million 24 cash, million 16 utalipa AICC na million 8 ni faida tutagawana mimi, mhasibu wangu na wewe, nikamjibu sawa. Baada ya muda mfupi akanipigia huyo Shabani A.K.A dr akaniuliza wewe ndiyo mwakilishi wa Samweli? Nikamjibu ndiyo. Mwambie wakaguzi wa TRA wanataka 480,000 cash bila mhuri wa TRA mzungu atakataa, nikamjibu kuwa ongea naye mimi nimeambiwa kusimamia kupaki mzigo (alipotaja hiyo hela nikaanza kushituka kuwa hapa kuna jambo).

Baada ya muda Samweli akapiga cm akaniambia nimeongea na dr anataka 480,000 cash, akajifanya analalamika vibaya sana nikamwambia million 8 kutoa lakini 480,000 baki 7,520,000 mbona ni faida kubwa sana? Akasema isiwe tabu hapa mfukoni nina 280,000 naomba uniongezee laki 2 nikamwambia isiwe tatizo tuma hiyo 280,000 kwenye airtel money yangu nitaongezea hiyo laki 2 akasema sawa.

Baada ya kama dak 5 Shaban (dr) akapiga akasema Samweli amenitumia 280,000 amesema laki 2 unatoa wewe nikamjibu ni kweli natoa mimi lakini nipe dak 20 tu, baada ya dak 15 nikampigia nikamwambia nipo hapa getini japo sikuwa getini njoo unipokee au nielekeze ofisini kwako nipo na hela.

Akasema ukiingia mlinzi atashituka nikamjibu mbona watu wengi wanaingia hashituki kwani anajua nakuja kufanya nini na wakati mimi nakuja kuonana na dr wangu? Wewe tuma kwenye simu nikamwambia poa ngoja niende airtel money town, Arusha airtel money ni za shida nyingi ni m-pesa akaniambia fanya haraka naandaa mzigo nije nao hotelini atapofikia mzungu na mhasibu wenu.

Baada ya dak kama 5 mzungu feki(0787-407501) akapiga akaniambia anapata supu karibu na Golden Rose wapo na mhasibu wa kampuni lakini anavyoongea kimombo nikajua huyu ni tapeli, nikamwambia nakuja hapo nikufuate akakataa akasema anatafuta hoteli ya kulala na kupokelea mzigo.

Baada ya muda kidogo akanipigia Samweli (mkurugenzi feki) akaniuliza unafanya kazi gani? Nikamwambia nipo Monduli kambini akakata simu nikapiga hakupokea tena mpaka leo.

Hawajamaa ni matapeli wazoefu ukikurupuka unaenda na maji, maswali nilijiuliza inakuwaje mtu ambaye unamjua umuulize unafanya kazi gani? Kama wewe ni mkurugenzi wa kampuni dr anashindwaje kukuamini 480,000 wakati mnafanya biashara ya mamilioni? Maswali ni mengi sana siwezi kuandika yote.

Hawajamaa wamesajili majina yale ambayo wanayatumia kutapeli lakini ukituma pesa hutakaa uwapate na wanaomba hela kidogo iliusishituke. Tuwe makini jamani nimeona ni wafahamishe msije mkatapeliwa na sijui na wanazitoa wapi no za simu za watu pamoja na kutaja eneo ulipo, kama hawashirikiani na watu wa customer care basi wanashirikiana na watu wa karibu yako.

Tusikimbilie hela za haraka unaweza kutapeliwa kirahisi sana.

Nilichelewa kuirusha/post kutokana kuwa na majukumu mengine nilikuwa sijapata muda wa kuichapa.

Jamani mimi siyo mwandishi wa habari kwa hiyo mapungufu mtanisamehe japo lengo langu ni tahadhari kwa wadau wasijitapeliwa.

Asanteni.
 
Hawa jamaa ni hatari.Mimi walinipigia nikabaki nacheka.Eti mtu anakwambia anamjua muuza viatu vya shanga na batiki.Halafu ya hivyo vitu bei yake anajua.Anataka umpigie muuzaji ubargain bei aliyokupangia.Kuna mzungu anatoka ngorongoro atavichukua Kia kwenda navyo ng'ambo.Yaani ni full comedy.Usipokuwa mjanja unaliwa.
 
Wanapataje no za watu kama wahashirikiani na watu wa customer care? ndiyo swali langu.
 
Kuna tapeli anaitwa Yellow Kid Weil katika interview alisema "Binadamu ni 99% mnyama na 1% ndiyo ina huo ubinadamu, hii 1% ndiyo inasababisha madhila yote kutokana na tamaa, hamu ya kupata faida bila kuitolea jasho au kutolea jasho kidogo ndiyo inafanya watu waumie wanapokutana na watu kama sisi"
 
Ukiwa na tamaa ya kupata hela nyingi kwa ghafla au kuamini mambo ya ushirikina lazima utatapeliwa.

Jana nilipokea sms ifuatayo kutoka kwa namba ya mtu nisiyemjua:
"Kaka ahsante sana kwa mganga uliyetuletea. Kwa sasa hivi baba hali yake inaendelea vizuri kabisa hadi tunashindwa kuamini kama baba ndiye yule aliyekuwa ameugua kiasi kile. Hata vile vifaa vyetu vilivyokuwa vimeibiwa nyumbani tumeshangaa tulipoamka asubuhi ya leo tumevikuta vimerudishwa mlangoni kwetu na wezi na vyote vikiwa vimetimia. Hakika duniani kuwa watu wana madawa....". Nikajua anakotaka kunipeleka. Niliyomwandikia siwezi kuyaandika hapa lakini hakurudia tena kuniandikia.
 
Ukiwa na tamaa ya kupata hela nyingi kwa ghafla au kuamini mambo ya ushirikina lazima utatapeliwa.

Jana nilipokea sms ifuatayo kutoka kwa namba ya mtu nisiyemjua:
"Kaka ahsante sana kwa mganga uliyetuletea. Kwa sasa hivi baba hali yake inaendelea vizuri kabisa hadi tunashindwa kuamini kama baba ndiye yule aliyekuwa ameugua kiasi kile. Hata vile vifaa vyetu vilivyokuwa vimeibiwa nyumbani tumeshangaa tulipoamka asubuhi ya leo tumevikuta vimerudishwa mlangoni kwetu na wezi na vyote vikiwa vimetimia. Hakika duniani kuwa watu wana madawa....". Nikajua anakotaka kunipeleka. Niliyomwandikia siwezi kuyaandika hapa lakini hakurudia tena kuniandikia.
Alianza ''kukulewesha'' ili kama una shida uingie mkenge uombe kujua vizuri kuhusu huyo mganga na akuelekeze utakavyoweza kumpata. BTW Babati mtu anawezaje kukuamini umsimamie biashara yake yenye kuhusisha fedha nyingi huku hamjuani. Utapeli wa namna hiyo ni wa zamani sana na umeshaliza wengi wenye tamaa.
 
Mimi aliwahi kuniambia anaitwa Mr. Mkwawa. aliniambia kuna mzigo wa dawa za mifugo nikauchukue kwa Dr yuko wizara ya mifugo alinitajia hela ndefu kama m48 hivi. Wakati ananipa maelezo nilishahisi huo mchezo. Nikamwambia kuna kaka yangu pale Wizarani ngoja nimwambie afanye hilo deal. Soon akakata simu. Nilipompigia tena alijifanya hakumbuki lolote
 
Hivi mtu unaingiaje kwenye mtego kama huo?! Yaani mtu ambae hata kufahamiana hamfahamiani but from nowhere anakupigia simu ya mchongo! Wanaoingia kwenye mitego kama hii ni maboya wazoefu!
 
TCRA nayo ni bure kabisa
Mbona wanakamatwa sana tu na jeshi la polisi kwa msaada wa TCRA. kimsingi likishatokea tatizo kama hilo jitahidi kuripoti kituo cha polisi karibu yako na uwaachie hizo namba. Jeshi la polisi na TCRA wapo makini sana mkuu na nimeshuhudia wengi tu wanamna hio wamekamatwa
 
Hao nishawazoea sana, maeneo ya kanda ya ziwa wanajiita UNHCR, ni mataperi balaa mmoja wao namfahamu kaeni macho hasa ndugu zangu mlioko nyumbani maeneo ya Bulyanhulu, Geita na Kahama
 
Mahakama zetu utaambiwa ushahidi na kupoteza muda , cha msingi ni kubwa makini na hawa matapeli.
 
Cha kufanya ni watu kuwa makini na ku maintains privacy yao

Kuna mbinu nyingi za kujikinga na hizo threat hasa kwenye mitandao,lakini

Ikumbukwe kuwa kwa sasa hii crime imefikia next level ukiacha huo utapeli wa kiihivo sasa hivi wanatumia mbinu hizo kwenye identity theft, psychological threat, na hata kutekwa nk.
 
Back
Top Bottom