Tahadhari kwa mliojipanga kununua hisa za makampuni ya simu...

Nadhani hamjui 'corporate culture'.
Makampuni yote makubwa yanapotaka kufanya maamuzi yatayogusa wananchi huwa yanaunda kikosi kazi kinachoitwa Lobby group. Hiki ni kikosi kitacho loby policy makers ili watunge sheria zitazofeva makampuni husika.
 
Kina Ruta na wenzako bado ni wachanga sana kwa uelewa wa kuendesha nchi ya viwanda na ninawashauri mtulie tu huko kwenye jukwaa la MMU maana ndilo size yenu!
 
Kama mnabisha kuwa hii si kazi ya lobby group, kwa nini sekta nyingine 'hazijalazimishwa' kuingia DSE? Kulikuwa na ulazima gani wa kampuni za simu kufanya ivyo? Mbona Helios wanaomiliki minara hawajalazimishwa kuingia DSE? Mbona Tanesco, IPTL and the like hawajaingizwa DSE?
 
Jamani, msije kusema napiga porojo, mimi nina digrii kadhaa kwenye mambo ya biashara, nimetumia karibu miaka kumi kusomea mambo ya kibiashara, kwa hiyo ndio maana naona bora niwataadharishe nyie mnaotegemea kununua hisa kwenye makampuni haya ya simu...

Kwa nini mtu huuza hisa?
Kuna sababu kadhaa za kuuza hisa, moja ni kuongeza mtaji ili kukuza biashara,
- Mbili ni pale mtu anapotaka kujitoa kwenye biashara huuza hisa zake kwenye biashara husika,
- Tatu ni kukusanya fedha ili kuweza kulipia madeni iwapo kampuni ipo kwenye hali ngumu kiuchumi.

Kwa nini kampuni nyingi za simu wanauza hisa, na kwa nini wanauza sasa?
- The market is not growing or its not profitable kwa hiyo wanauza hisa ili wawekeze kwenye biashara nyingine ambazo zina faida zaidi,
- Kwa nini wanauza hisa zao sasa? Hapo ndipo pa kujiuliza, kwa nini hawakuuza hisa zao labda miaka miwili, mitatu au mitano iliyopita? Jibu ni kuwa hakuna mtu anayeuza mali yake ikiwa inamzalishia, hakuna mtu anayeuza ng'ombe wa maziwa anayekamuliwa lita nyingi za maziwa. Ngo'ombe anauzwa akiwa amekwisha zeeka, au kama ni jike akiwa hana uwezo wa kutoa maziwa ya kutosha...
Study wanahisa wakubwa, Miaka ya hivi karibuni mwanahisa mkubwa Bwana Rostam aliuza hisa zake zenye thamani ya karibia bilioni mia tisa? Je jiulize, kama kampuni inafanya vizuri, kwa nini wanahisa wakubwa wanauza hisa zao badala ya 'kununua' hisa zaidi? Jibu unalo mwenyewe.

Je unapo nunua hisa unanunua nini?

Kwa kampuni za simu kwa hali ya sasa, unaponunua hisa, UNANUNUA JINA TU.
Haya makampuni makubwa ya simu kama Vodacom, Tigo nk walishauza minara yao yote ya simu kwa kampuni ya Helios Towers Tanzania.
Hawana majengo ofisi zote wamepanga,
Magari yao wamekodisha kwa kampuni mbali mbali za usafirishaji,
kwa hiyo haya makampuni yanamiliki jina tu... Hayana assets za maana. Usidanganyike na majina makubwa ya makampuni haya...
Waulizeni wenzenu walionunua hisa za Precision Air wametengneza faida sh ngapi?

Kiufupi mtaponunua hisa ikala kwenu hakuna atakaye watetea, Sheria ya manunuzi inatoa angalizo kwa mnunuzi wa bidhaa yeyote kwa kusema, 'Buyer beware'!

Kampuni halisi ya simu kwa hivi sasa hapa Tanzania ni Helios Towers ambayo ndiyo inamiliki minara ya mawasiliano (Hawa wengine wamebaki kuwa madalali wa sekta ya mawasiliano)... Siku wakija kutibuka wakakataa kupangisha minara yao, ina maana haya makampuni mengine ya simu yatatoweka... Kinachoyaweka haya makampuni ya simu hapa nchini ni vibali vya mawasiliano walivyouziwa na TCRA. Cku TCRA nao wakigoma ku renew leseni zao za mawasiliano huo ndio utakuwa mwisho wa makampuni husika...

Vodacom sells towers to Helios in $75 million deal: report | TelecomEngine.com

Bharti Airtel to sell 1,350 towers in Tanzania to American Tower Corp

Tigo Tanzania Sells Tower Assets to Helios Towers
OK sawa hebu Shauri watu wanunue hisa kampuni gani sasa
 
Wewe utakuwa pia na degree ya uongo kabisa....
Pamoja na hiyo degree yako lakini unaonekana wewe ni muongo na siyo mfatiliaji kabisa au husikilizi maswala ya msingi au ya uchumi au hata bunge hukuwai kusikiliaza.

Ni kutaarifu tuu kuwa sheria mwaka huu bungeni ulipelekwa muswada bungeni wamabadiliko ya sheria na iliongezwa kifungu kinacho yalazimu makampuni ya simu na madini kujiorodhesha kwenye masoko ya hisa...na sheria iliwataka makampuni hayo kujiorodhesha mwishoni mwa mwezi huu wa kumi na mbili na ndicho kitakacho fanyika na sheria iliwataka makampuni yote kuuza asilimia 25 ya hisa walizonazo kwa Umma na kila mwezi watu watakuwa wanapewa gawio...
Hivyo mwisho wa mwezi huu makampuni ya simu yote na mengine yataji orodhesha kwenye soko la hisa dares-salaam(DSE)
Hivyo kusema wanauza hisa kwakuwa wana hali mbaya ya kiuchumi ni uongo na upotoshaji wa kiwango chajuu kabisa bali wanafanya hivyo kulingana na matakwa ya kisheria.
Punguzeni kupotosha watu japo ni kweli ulio wazi kuna faida na hasara za kununua hisa
Umeongea ukweli kabisa, inaonekana jamaa alikurupuka bila kujua kwa nn kampuni za simu zinauza hisa
 
Kama mnabisha kuwa hii si kazi ya lobby group, kwa nini sekta nyingine 'hazijalazimishwa' kuingia DSE? Kulikuwa na ulazima gani wa kampuni za simu kufanya ivyo? Mbona Helios wanaomiliki minara hawajalazimishwa kuingia DSE? Mbona Tanesco, IPTL and the like hawajaingizwa DSE?
Wewe usiendelee kuonyesha ujinga wako. TANESCO imekuwa ikipata hasara miaka yote kabla ya mwezi uliopita kutangaza faida. Hao wangeenda sokoni wangechemka. IPTL mkataba wao ulikuwa wa muda mfupi hapo awali na muendelezo wake si wa uhakika. DSE wanajitahidi sana kuvutia wawekezaji bahati mbaya makampuni hayavutiwi na listing kwa sababu ya illiquidity na lengo lao la kuhakikisha hisa hazitoki nje.
Soko la mawasiliano bado imara. Ungekuja na financial statements zao ungeshawishi na si hivi.
 
OK sawa hebu Shauri watu wanunue hisa kampuni gani sasa
Mimi ninakwambia nunua hizo hisa sasa hivi ingawa gawio linaweza lisiwe zuri mwanzoni ila kutokana na hali ya uchumi, hisa zinaweza kuwa undervalued. Mbeleni zitalipa. Soko la mawasiliano linazidi kukua.
 
Wewe niite muongo ila nenda UKANUNUE JINA. Fedha ni zako na sina mamlaka nazo... Mimi kama expert kazi yangu ni kutoa angalizo, na nimetimiza majukumu yangu kwa umma wa watanzania... Hasa ndugu zangu wasio na upeo mkubwa juu ya mambo ya biashara, wasije wakaliwa kama walivyoliwa kwenye DECI...
Hivi ww unaweza kujiita expert kweli!! Kwa uongo huu na kutisha watu ndo ujiite expert. Kwa taarifa yako tu, biashara inayo fanya vizuri africa ni biashara ya simu labda NA ya bia (vileo) makampun ya simu ni matajiri sana. Sasa serikali imetunga sheria ili badala ya utajiri wa makampun haya ya simu na madin kwenda kwa wamilik wachache ni bora pia kuwashirikisha Wananchi. Kwa hiyo makampun hayo yamelazimishwa kuuza biashara zao kwa 25% kwa Wananchi wa kawaida kupitia soko la hisa kabla ya january 2017. Hizi ni habari Njema sana mkuu wala sio za kupuuza.

Lakin ni ukweli kuwa sio kila biashara inaweza kufanywa na kila mtu. Kama ww ni muoga wa kuwekeza basi nyamaza waachie wataalamu wa ku take risk na am sure itawalipa sana.

Serikali hii inataka makampun yote, mabenk na taasisi zote za biashara zifanye biashara na Wananchi wa kawaida ili na wao wasimamie na kufaidi uchumi wao.

Ndo maana unamsikia Magu anasisitiza kuwa serikali haiwezi kufanya biashara na mabenk au makampun. Waende kwa Wananchi wafanye nao biashara.

Inapaswa kuwa hivo. Hapa mwanzon utaona kama ni balaa, ni shida, kama ni anguko la kiuchumi lakin baada ya miaka mitatu hivi ndo mtaanza kuelewa Magu alikuwa anawapeleka wapi. Nyie wenyewe mtamvulia kofia. Tulieni muone.
 
Tatizo la nchi hii kila mtu anajifanya eti yeye no expert wa kila jambo kama mleta mada anavyowaongopea watu kwa kujiita expert na kuleta uchambuzi wake wa uongo uongo.
Sekta ya mawasiliano ni kati ya sekta iliyo thabiti kwa nchi za afrika.
Ni sheria tu iliyopitishwa inayoyabana makampuni ya simu kuuza 25% ya hisa zake kwa wananchi otherwise wasingeuza
 
Kama mnabisha kuwa hii si kazi ya lobby group, kwa nini sekta nyingine 'hazijalazimishwa' kuingia DSE? Kulikuwa na ulazima gani wa kampuni za simu kufanya ivyo? Mbona Helios wanaomiliki minara hawajalazimishwa kuingia DSE? Mbona Tanesco, IPTL and the like hawajaingizwa DSE?

Ndugu mtaalam, asante kwa nia njema ya kufahamisha wengine kile unachoamini kuwa unakifahamu. Pamoja na nia njema hiyo, hoja yako haijajengwa na "facts" za swala hili. Ukweli ni kwamba
A)makampuni haya yametakiwa kuuza hisa kwa mujibu wa sheria. Wao wenyewe wamejitahidi ku-lobby wasiuze imeshindikana.
B)Helios siyo kampuni ya simu, bali ni "real estate" company, ambao wamespecialize ktk telecoms infrustructure. Walichonunua Toka kwa Tigo na Vodacom ni minara, vijumba vya mitambo na miundo mbinu mingine. Mitambo yenyewe ya mawasiliano iliyofungwa ktk vijumba na minara hiyo bado inamilikiwa na Tigo na Vodacom
D)Hata makampuni ya miundombinu ya mawasiliano kama Helios na American towers nao sheria hiyo hiyo inawabana na wanalazimika kuuza hisa DSR
E)kwa wajumbe wote: stable as it is, the telecoms industry is no longer as profitable as it used to be. Gharama za uendeshaji zimepanda sana, ushindani umeshusha sana bei, na mapato hayakui isipokuwa tu yale yatoka ayo na matumizi ya mobile money na data. Ambayo hayajawa makubwa kufidia gharama, na upungufu wa mapato ya kupiga simu na sms.
F)kuonyesha ni namna gani siyo chaguo la makampuni haya kuuza hisa ktk soko "changa" kama DSE, American Towers wamegoma kuchukua minara ya Airtel (japo makubaliano yote yalishakamilika), kwa sababu tu hawako tayari kuuza share zao 25% ktk DSE. Hofu yao kubwa ni kwamba thamani ya hisa zao zitaathiriwa sana na udogo na instability ya DSE, Uchumi wetu na thamani ya shilingi yetu, pamoja na mambo mengine.
Bado wanajadiliana na serikali namna ya kuwa "excempted" wasiuze hisa zao DSE.
 
Wewe usiendelee kuonyesha ujinga wako. TANESCO imekuwa ikipata hasara miaka yote kabla ya mwezi uliopita kutangaza faida. Hao wangeenda sokoni wangechemka. IPTL mkataba wao ulikuwa wa muda mfupi hapo awali na muendelezo wake si wa uhakika. DSE wanajitahidi sana kuvutia wawekezaji bahati mbaya makampuni hayavutiwi na listing kwa sababu ya illiquidity na lengo lao la kuhakikisha hisa hazitoki nje.
Soko la mawasiliano bado imara. Ungekuja na financial statements zao ungeshawishi na si hivi.
Nakuunga mkono, walete figures.
 
Lililonishtua ni minara kutokuwa yao?unapimaje value ya kampuni hizo kwa uhakika?kama nimemwelewa mtoa Mada vizuri ni kwamba zinategemea zaidi Jina au kitu kinaitwa goodwill tuu.kama ni hivo wengine tumeshituka mpaka tupate maelezo ya kina.unauzaje bunduki ukabaki na Risasi?
 
Back
Top Bottom