Tahadhari kwa mliojipanga kununua hisa za makampuni ya simu...

Nakushukuru sana umenifumbua macho. Nilitaka kununua hisa za millioni thelathini lakini kwa ushauri ulioutoa sitatoa hata senti tano yangu. Ahsante kwa taarifa nzuri
 
Wewe niite muongo ila nenda UKANUNUE JINA. Fedha ni zako na sina mamlaka nazo... Mimi kama expert kazi yangu ni kutoa angalizo, na nimetimiza majukumu yangu kwa umma wa watanzania... Hasa ndugu zangu wasio na upeo mkubwa juu ya mambo ya biashara, wasije wakaliwa kama walivyoliwa kwenye DECI...
Hongera sana kwa elimu yako na kweli yametia. Hisa za vodacom mpaka leo kimya
 
Ma "nguli" wa elimu ya biashara wamekutana, Mimi nashuhudia minyukano tu huku nikipata elimu ya soko la hisa! baada ya hii post tunaomba msomi mwingine ajitokeze awachokoze leanernd brothers tushuhudie wanavyotifuana..
 
Asante mkuu!
Niliposoma tu andiko lako nikakubali. Watanzania ni wabishi sana na huwa hawataki kuambiwa. Wote waliokubishia wanaona aibu sasa. Ila statement yako ya mwisho ya ''Buyer beware'' imenifumbua macho sana. Huwa najiuliza kwann huwa hawashitakiwi? Lkn jibu nikalipata kwenye hayo maneno mawili. Laiti watanzania wangejua wasingenunua hisa vodacom. Hongera, andiko limetimia asiyesikia na asikie sasa. Nimesoma kuanzia page ya 1 mpaka ya mwisho. Watanzania ni wabishi sana.
Hongera sana mtoa uzi. natamani huu uzi ungekuwa pinned ili watu wasome. Nimekupa 100% hapa ni A
 
Back
Top Bottom