Kachanchabuseta
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 7,263
- 685
WanaJF wanaishi maeneo yote ya kuelekea bagamoyo
watakubaliana na mimi ninachokisema sasa hivi. Hiki kitu kimenichukiza
maana ni unyonyaji wa hali ya juu.
Muda wa Usiku kuanzia saa 2
Malori ya kubeba michanga yanakuwa mengi mida ya usiku yakitokea bagamoyo kuelekea
mjini, ukiangalia kwa makini kilichopo ndani sio mchanga bali ni vitu vingine. Katika uchunguzi
wangu nimegundua vitu wanavyobeba ni bidhaa zinazoshushwa kwa njia za panya sehemu za mapinga na ikelege.
Kichofanyika ni meli ya mizigo ikifika karibia na njia za panya wanashusha mizigo na kupakia kwenye boti ndogo ndogo
na kivisogeza njia za panya pale ikelege na mapinga na seheme nyingine ili kukwepa kodi.
Mida ya Asubuhi kati ya saa 11 hadi saa 1
Gari hizi hizi zinakuwa zinaelekea mjini lakini mara hii inakuwa canter ambazo zimezibwa kotekote Gari za police wale wa dolia
wanakuwa wanazindikiza hizi gari. Leo kwa mara ya tatu nimeshudia police wakisimamisha hizi gari na kuingia ndani ya gari na gari linaondoka then wanashushwa mbele baada ya kilometa 2 hivi
Biashara HARAMU YA POLICE
Mpaka sasa najiuliza kwanini hawa police wa dolia na Trafic wa barabarani wanasindikiza haya magari?
Kwanini wanayasimamisha kwenye foleni na kuyapanda kisha kushuka mbele baada ya kilometa 2 hvi?
Kwanini njia ya Bagamoyo inakuwa na police wa dolia wengi?
Source: MIMI mwenyewe nimeshudia
Nitawapiga picha na kuzileta hapa
NB: Naomba waandishi wenye mapenzi mema na maendeleo ya Tanzania wafuatilie hii kitu maana inaonekana imeanza muda mrefu zamani walikuwa wanatumia njia ya panya ya Kunduchi
Update............................06/11/2012
Leo katika maeneo ya mbuyuni gari la police lenye number za usajili T332AVN likiwa na askari waliovaa nguo za kiraia gari lao lilikuwa linaeleka Tegeta pale mbuyuni walisimama katikati ya barabara na askari wawili wakashuka na kuelekea kwenye gari mbili aina ya Canter moja ilikuwa na number za usajili T927BKL NA lingine sikuweza kupata numba zake maana lilikuwa mbele kidogo.
Hizi Canter zilikuwa na mzigo sijui nini maana baada ya hizi canter kwenda na hawa police waliovaa nguo za kiraia waliingia kituo cha mafuta Camel Africana (kama sijakosea jina la kituo) na kuwashusha hawa police
Swali linaloniumiza ni biashara gani inaendelea hapa?