Tahadhari: Biashara HARAMU ya Polisi Barabara ya Bagamoyo

Tahadhari: Biashara HARAMU ya Polisi Barabara ya Bagamoyo

Wale wapi kama wewe mfanyabiashara uapitanjia za panya na unakwepa kodi lazima tuelewane tu , mbona misamaha ya kodi mingi tu na inayotunyonya tena katika sekta za juu kabisa madini , utalii nk. Na mbona watumishi ni mara ngapi ofisini mnajiandikia safari na overtime za uongo ..au kwa vile hamuonekani?

Uozo umeanzia juu , hivi unajua hali ngumu ya polisi inaletwa na serikali yenyewe ? posho tatizo , mafuta wanaomba omba mishahara midogo ,nyumba wanazokaa sasa hoi bin taabani lol..nyinyi acheni ii siyo kazi mapolisi wa kike sasa WP ndo kabisa wanajiuza ..we unajua kuna mtoto wa kigogo serikalini ana kamuni yake ya kusupply vitu fulani jeshi la polisi nchi nzima ..analipwa 40bilion kwa Mwezi ? na hiyo pesa inalipwa kwenye bajeti ya jeshi la polisi kila mwka ? tumechoka bora uchukue chako mapema tuuuuuuuuu...!!!
 
Hivi nyie watu mnafikiri bila ya mbinu kama hizo, haya maziwa ya NIDO mtaweza kuyanunua madukani?,hiyo biashara haina mkono wa mtu wowote mkubwa,wadau wakubwa wa hiyo biashara ni wapemba ni mchezo wa siku nyingi, nenda kule ununio uone sukari zilivyozagaa,kila nyumba za wenyeji ni maghala ya bidhaa.Kwa undani zaidi nenda pale mbuyuni njia panda ya kunduchi mtafute dereva wa lori la mchanga akupe mkanda mzima.
 
Hongera Dr kwa kufuatilia hiyo kitu, hakuna chochote wanachosafirisha zaidi ya unga, biashara ya wenyewe hiyo ndiyo maana inalindwa, kuwa muangalifu isiwe nawe wanakufuatilia
 
Update............................06/11/2012

Leo katika maeneo ya mbuyuni gari la police lenye number za usajili T332AVN likiwa na askari waliovaa nguo za kiraia gari lao lilikuwa linaeleka Tegeta pale mbuyuni walisimama katikati ya barabara na askari wawili wakashuka na kuelekea kwenye gari mbili aina ya Canter moja ilikuwa na number za usajili T927BKL NA lingine sikuweza kupata numba zake maana lilikuwa mbele kidogo.

Hizi Canter zilikuwa na mzigo sijui nini maana baada ya hizi canter kwenda na hawa police waliovaa nguo za kiraia waliingia kituo cha mafuta Camel Africana (kama sijakosea jina la kituo) na kuwashusha hawa police

Swali linaloniumiza ni biashara gani inaendelea hapa?


Hayo uliyoyaandika yanatokea hata hapo Kipunguni. Magari hayo hayo ya doria yanashusha mapipa ya mafuta kwa jamaa moja usiku wa manane! Halafu yeye anayauza Ukonga-Banana kwa bei ya kutupa! Kila siku saa nane usiku wanashusha mzigo na wakirudi huchukua pesa na kuacha mapipa mengine ya mafuta. Sijui mafuta haya wanayatoa wapi..! Tunasema majambazi au wezi wako kumbe polisi ndo wanaongoza..
 
Hao police imekua ni kazi yao! Hata me nimeshuhudia two times, wanasimamisha gari wanapewa buku kumi. Ni mizigo isiyolipiwa kodi inakuja na majahazi na kushushwa mbweni! Imekua ni kama mradi wao! Sijui IGP anajua haya! Wanaaibisha jeshi la police! Bado kuzunguka na magari ktk machimbo ya mchanga kudaka pesa kwenye malori!!kazi sio yao ila kwa kua wana njaa wanalazimisha wapewe pesa.
 
kwa polisi kufanya hivyo sishangai.........


kesho mtasikia kuwa ni madini yanasafirishwa ...(assumption yangu tu hii)

na wahusika hawatofanywa lolote...


ccm oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Kuna BANDARI BUBU kule mbweni karibu na chuo cha TISS kila mzigo wa mkubwa hushushia huko na kusimbwa na hayo malori yanavunga ya mchanga. we lory mchana hayafuniki mchanga kama sheria inavyosema kkn ucku kila lory limefunika. Na police ndo wasindikizaji mizigo ya mafisadi na vigogo wa CCM. Hiyo ndo nchi inavyoliwa ucku.
 
Back
Top Bottom