adamWaEden
New Member
- Nov 24, 2020
- 2
- 1
Geto kuna joto😓 ,feni haiwaki na malipo ya umeme ni zamu yako.Chini ya kitanda kuna Panya anatafuna soksi ya mguu wa kushoto inayotoa harufu flan hivi sio rafiki!😷 Pembeni kuna Dundo moja kuu kuu ulilodumu nalo kwenye shida na raha! Umejiegesha kitandani na Kinjunga chako ulichokunja ki'26 kwenye pindo!
Kiswaswadu kinaita na kuita na wala hujishughulishi nacho📲 kwa kuwa tu ushajua si mwingine ila ni Mzazi mwenzio anataka kuulizia kuhusiana na matumizi ya mtoto! Usiwasahau ndugu zako nao wanasubiri mchango wa shangazi yako aliyekatwa ziwa kutokana na saratani ya matiti uliwaahidi leo ukasema kuna mchongo bado unausikilizia! Ghafla unakuna kichwa baada ya kusikia Faza hausi nae anagonga mlango ameshachoshwa na kalenda zako!
Amini usiamini chochote unachokipitia mda huu ni mapito tu! Mtatuzi wa matatizo yako yote ni wewe mwenyewe! Washkaji kibao tunaishi nao wana mawazo(ideas)🧠 chanya sana ila wengi tunasingizia mitaji!
Sa kwa mfano hamna wakutupa mitaji tunafanyaje!? Lazima ipo njia amini! Usimlaumu mtu yeyote.Tatizo sio Elimu uliyonayo au ulichokisomea,haijalishi hata kama ulikuwa unapiga sana kelele darasani.Hakuna anaekuroga mchawi ni wewe mwenyewe! Baba na Mama washamaliza sehemu yao kwa kifupi hawana lawama na wewe na hawana lawama kwa mungu.
Tunawakanyagia sana raia wanaopiga misele na gari za Madingi zao watoto wa mtaa tunaita TAGI UBAVU! Utasikia "ile sio yake ni ya baba yake!"ni kweli ila Baba ake ndo mtaka cha uvunguni so mwache afurahie matunda ya mshua!
Na we tafuta sasa mwanao aje kutamba! Yaani umasikini umetuzidi mpaka tunatafuta waku'share nae machungu eti!!😩 Kwenye kila familia ya kishua unayoifahamu ilianza na masikini mmoja aliyejitoa kubutua kombolela kuokoa wengine.
Hatujazaliwa familia za kishua ila tuna nafasi ya kutengeneza familia za kishua.Cha msingi,we agana na nyonga.! Nadhani mpaka sasa ushajua nini cha kufanya
#sindanoZamasaa💉
#streetmastermind🧠