Tafuta hiki kitabu usome

Tafuta hiki kitabu usome

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
Nimetafakari sana, na nimeona kwamba, sio kwamba nchi yetu inapita katika kipindi chochote kile, ila imekwama, na watu pekee wa kuweza kuikwamua ni sisi wenyewe watanzania, sisi ndio tatizo, katika kila nyanja ya maisha yetu, sisi ndio wachangiaji wakubwa wa matatizo tuliyo nayo, na tunaendelea kutengeneza matatizo mengi zaidi.

Naomba nichukue fursa hii, kuchangia namna ya kutoka hapa tulipo, kwa kupendekeza maeneo au namna ya kupata ufahamu wa namna ya kujikwamua kutoka hapa tulipo.

Tafuta kitabu hiki usome: CRITICAL THINKING, CONCEPT & TOOLS, ni bei nafuu sana, nimekinunua kwa Dollar 9 tu.tembelea website hii upate taarifa zake, vitabu vingine na references nyingine nyingi za maarifa: Critical Thinking , jitahidi kuzunguka kwenye hiyo website bila kuchoka.

Kama kuna mtu anaweza kujitolea tukakusanya pesa na kununua kitabu/vitabu hivi na kuvisambaza huko vyuoni tuwasiliane.

Kitabu Kingine Tafadhali
Kinapatikana online kwenye PDF, kinaitwa "confessions of an economic hit man", Ukisoma hiki utaelewa ni kwa nini nchi wafadhili (kama tulivyozoea kuwaita-sababu baada ya kukisoma utakubalina na mimi kuwapa jina la nchi majambazi au nchi matapeli) ziko tayari kutoa mipesa mingi kujenga mabarabara, vinu vya kufua umeme n.k.
 
Back
Top Bottom