My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,930
- 13,335
Nchi ni lazima iongozwe kisheria ili kutoa haki kwa watu wake wote.
Taifa likiongozwa kwa mihemko ya chuki binafsi na chuki za kisiasa, hilo taifa huitwa " Maandazi Republic ".
Maana yake ni kwamba, ni taifa lisilo jitambua lilipotoka na linapokwenda.
Niliwahi kuhudhuria kesi ya rafiki yangu nchini Uingereza enzi zile nikibeba Box, rafiki yangu ambaye ni raia wa UK, alifikishwa mahakamani kwa kutuhumiwa kutoa lugha ya matusi kwa mtalaka wake.
Alimwambia ni mpumbavu na mjinga.
Siku ya hukumu, hakimu alimsafisha mtuhumiwa na kusema hana kosa lolote lile kisheria linalopaswa kumtia hatiani.
Hakimu alitoa hukumu na kusema.
"A fool is any person that lacks or completely suffers no prudence,hence having no prudence doesn't imply an insult, and a stupid is a person whose deeds show that he/she is absolutely uneducated,hence being a stupid doesn't mean that you have been insulted ".
"Mpumbavu ni mtu aliyepungukiwa au hana hekima kabisa, kuwa mpumbavu siyo tusi, na mjinga ni mtu ambaye matendo yake yanaonyesha kuwa hana Elimu, kuwa mjinga siyo kwamba umetukanwa".
Sehemu ya hukumu hiyo ilisema hivyo, hakimu alidai hivyo ndivyo alivyoitafsiri sheria.
Serikali inapoamua kumpiga marufuku msanii na kumfungia kazi zake kwa sababu tu ameimba kibamia, neno ambalo ni la mitaani ni kichekesho kweli.
Ni tafsiri ipi ya kisheria ambayo inatambua kuwa kibamia ni tusi?
Kibamia ni bamia ndogo kuliko zote, na bamia ni mboga, iweje leo Jamhuri,("The entire government is regarded as Republic and any decisions made by any top official therein are mentioned as decisions carried out by the Republic of the particular country ".)
Itambue kuwa kibamia ni tusi bila chombo cha kutafsiri sheria ambacho ni mahakama kuridhia?
Tanzania ni taifa linaloheshimika kimataifa kwa miaka mingi mno, hatutakubali kuwa "Maandazi Republic "kwa sababu ya watendaji wachache wa serikali kutunga sheria kandamizi kwa sababu zisizojulikana.
Serikali imejigeuza kuwa mahakama, shame on you!