Nguniani
JF-Expert Member
- Nov 8, 2014
- 1,139
- 1,313
Habari,
Msaada juu ya maana ya hii ndoto
Nimeota kulikua na vita ya mataifa matano ambayo yaliamua kuungana so nchi yangu ilikua ni adui kwa hayo mataifa basi Siku moja usiku nchi ikawa imevamiwa tukawa chini yao usiku huo so Mimi nakaomba niende chooni.Wakati naenda nilivyo fungua tu mlango nikaona kiongozi mkuu wa Yale mataifa akitoa maelekezo.Sasa wakati narudi ndani nikasikia kidogo alicho kua anaongea juu yetu.
Basi nilivyo ingia tu ndani akatumwa askari wao, nikamwambia najua umetumwa kuniua sababu nimesikia mlicho kua mna agizwa. Nika mwambia naomba usiniiue basi askari akaniambia panda juu ya Dari utakapo pata muda wa kuchomoka huko chomoka.
Basi punde askari alipo niambia nipande juu kukawa kumetokea mvutano nje kama watu wana resist,hilo likawa tobo na sisi kutoka nje.
Tulivyo toka njee Mimi na marafiki zangu kadhaa tukaona hapa si pa kukaa sisi tukimbie,wakati tunakimbia risasi zikaanza kurindimaa kufikia mbele mbele kidogo nikashaanga tu rafiki zangu wamedondoka chini,hivyo wakawa wamepoteza maisha pale.
Kwa mbali nikawa naona kuna mama anakuja yaani mke wa kiongozi mkuu,wakati huo mimi nimechuchumaa basi nikaona na mimi nijifanye nimekufa hivyo nikaji pakaza damu za wale rafiki zangu ili akifika pale ajue wote tushapoteza maisha.
Yule mama alivyo fika pale alikua amejawa na hasira sana,akaanza kuongea maneno ambayo yaliniuma sana,nikajikuta kwa ujasiri mkubwa nimesimama na nikaanza kubishana nae sasa pale nikama nilimshika simba sharubu hasira zilimjaaa mnoo kiasi kwa angekua na silaha angenimaliza tu pale pale.
Wakati tunabiahana,yule mama aliongea kwa sauti ya juu sana tena alitumia lugha nyingine nadhani alimaanisha kuna mtu kasalia huku.Upande wetu wa Kulia ndipo nikaona piki piki zao zile zenye matairi matatu ikija,inaonesha walee viongozi wa juu ndio walikua upande ule wakishuhudia Yale yaliyo kua yameagizwa.
Nikasema hapa bila kupoteza muda kabla hajanifikia niondoke,nikakimbia kama hatua 10 tu nikakutana na mto ile nageuka naona ile piki piki ikija kwa kasi sana upande wangu nikavuka mto ule nikapotelea mashambani,kulikua na maindi tupu ingekua ngumu kwake kujua nimetokomea upande upi.Hiyo ndo ikawa pona pona yangu.
HIYO NDIO NDOTO NILIYOOTA USIKU WA KUAMKIA LEO.ANAEWEZA KUCHANGIA MAWAZO YAKE JUU YA MAANA YA NDO HII ASISITE KUTIRIRIKA.
Sent using Jamii Forums mobile app