Maswali mazuri sana haya.
CCM ingawa ni wazuri sana katika kuiba kura, kuiba kura si rahisi hivyo.Na katika kila uchaguzi wapinzani wao wanajifunza kitu kipya na ni jinsi gani kuwabana wasiibe kura, kwa hiyo wakajishtukia it is only a matter of time watafikia sehemu watashindwa kuiba kura.
Sasa wakaona ikifikia wakashindwa kuiba kura, wasikose kila kitu, waweke serikali ya mseto ili hata wakishindwa kura wapate kuwa katika serikali. Na mwaka huu kuna uwezekano mkubwa wa CUF kushinda.
Bila kujali misimamo ya kisiasa, mimi naona hii habari ya serikali ya mseto inawapunja CUF, kwani CUF wakishinda sasa hivi watatawala na CCM. Lakini mtu mwingine anaweza kusema CUF walikuwa hawana jinsi, kwa sababu wangekataa mseto CCM wangeendelea kuiba kura tu kila uchaguzi.
Kikwete anategemea kuendelea kupeta tu, labda kidogo Zenj ndiko hakujajulikana vizuri kama miaka yote maana huko ndiko kuna uchaguzi, huku bara ni formalities tu na kuangalia CCM imeshinda kwa asilimia ngapi, hususan uchaguzi wa rais.
JMK hawezi hata kumuachisha kazi katibu mkuu wake, ataweza kuisambaratisha CCM? Halafu aisambaratishe kwa kisa gani wakati maslahi yake yako CCM ?