Tafsiri ya Matokeo ya Kura ya maoni ZNZ

Nyunyu

JF-Expert Member
Mar 9, 2009
4,354
1,010
Ndugu zangu wana JF,

Kwa makini nimekuwa na tafakari ya matokeo ya (Kura ya amoni) referendum Zanzibar na kupata maswali mengi yasiyo kuwa na majibu. Kwa matokeo haya; naamini yataleta mgongano wa uendeshaji wa nchi, ikizingatiwa Serikali ya CCM imekuwa ikisistiza kuwa ZNZ si nchi bali sehemu ya JMT!! Ni wazi matokeo yanaelezea hali ya uchaguzi wa rais ZNZ baadaye mwaka huu.

Nina maswali yanayonisumbua;

  • Imekuwaje CCM waasiibe kura ili kuendeleza uongozi wao?
  • Kikwete anategemea nini baada ya matokeo Oct 2010?
  • Inawezekana JMK ameamua kuisambaratisha CCM kwa fair elections?
Naomba kuwakilisha tujadili hili.
 
Maswali mazuri sana haya.


CCM ingawa ni wazuri sana katika kuiba kura, kuiba kura si rahisi hivyo.Na katika kila uchaguzi wapinzani wao wanajifunza kitu kipya na ni jinsi gani kuwabana wasiibe kura, kwa hiyo wakajishtukia it is only a matter of time watafikia sehemu watashindwa kuiba kura.

Sasa wakaona ikifikia wakashindwa kuiba kura, wasikose kila kitu, waweke serikali ya mseto ili hata wakishindwa kura wapate kuwa katika serikali. Na mwaka huu kuna uwezekano mkubwa wa CUF kushinda.

Bila kujali misimamo ya kisiasa, mimi naona hii habari ya serikali ya mseto inawapunja CUF, kwani CUF wakishinda sasa hivi watatawala na CCM. Lakini mtu mwingine anaweza kusema CUF walikuwa hawana jinsi, kwa sababu wangekataa mseto CCM wangeendelea kuiba kura tu kila uchaguzi.

Kikwete anategemea kuendelea kupeta tu, labda kidogo Zenj ndiko hakujajulikana vizuri kama miaka yote maana huko ndiko kuna uchaguzi, huku bara ni formalities tu na kuangalia CCM imeshinda kwa asilimia ngapi, hususan uchaguzi wa rais.

JMK hawezi hata kumuachisha kazi katibu mkuu wake, ataweza kuisambaratisha CCM? Halafu aisambaratishe kwa kisa gani wakati maslahi yake yako CCM ?
 
Kwa mfano ikitokea CUF wakashinda na wao kuunda serikali ya mseto; wakaongea wao huko wakafika hatua ya kudai uhuru toka JMT. Kwamba hawaoni umuhimu wa muungano and so ni bora wajitenge itakuwaje? Huoni CCM wamezidi kusogeza matatizo kooni?

Believe me wazanzibari wana uwezo wa kuweka tofauti zao za kiitikadi na kuweka mslahi ya nchi yao mbele, ushaidi ni huu muafaka. Hakuna ajuaye waliyoongea Maalim na Karume mapka wakashikana mkono!!!

Mi naona kama mabadiliko makubwa yanakuja vile....
 
Sasa hivi tumeishaondoka kwenye maximum (yaani chama kimeshika hatamu kwa njia yoyote). Sasa hivi tupo kwenye downstream ya CCM na muda si mrefu CCM wakakuwa chali kabisa. Wee subiri
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom