Tafsiri halisi ya turnover na changamoto ya ulipaji kodi

kizito2009

Senior Member
Jan 6, 2010
172
223
Katika Jedwali la kodi la TRA unatumika mfumo wa kutumia turnover kukadiria kodi.

Kwa mtu mwenye turn over isiyozidi milioni 20 analipa presumptive tax ya tzs 865000 ambayo ni sawa na kama 5% ya mapato yote kwa mwaka ambayo ni sawa na kiasi cha TZS 72000 kwa mwezi.Iwapo hesabu hazijakaguliwa.

Vile vile kwa anaelipa kiwango cha chini cha kodi yaani TZS TSHS 150,000 na turnover ya TZS 7500000 kodi yao ni sawa na 2% ya mapato yao ambayo ni sawa na TZS 12500 kwa mwezi.

Tutafakari na kujadili katika mtazamo wa kibiashara je viwango hivi vya kodi vinalipika?Je ni rafiki kibiashara hasa ukizingatia hali ya biashara kwa sasa.
Je itapendeza kama Vile vitambulishao vya magufuli vitawaongeza na watu hawa kwa ajili ya kuhakikisha makusanyo yanaongezeka.ili habari za kodi za asilimia na/mahesabu waachiwe makampuni.Wajasiriamali wadogo wawe na uwezo wa kulipa kodi kwa fasta

Nawakilisha tujadili
 
budget ya mwaka 2019/2020 imetoa grace period kwenye kupata TIN ya biashara, hivyo grace period inavyoisha tayari utakuwa unajua turnover yako, profit, na challenges zote kwenye biashara yako, nia ni kwamba TRA wanapokuja kukukagua, wakukague with facts na sio assumptions.

Kwa uzoefu wangu presumption waga tight mwaka wa kwanza wa biashara, baada ya hapo waga ipo in favor ya mfanya biashara, sababu wafanya biashara kamwe hawawezi kwambia their true turnover, mtu mwenye turnover ya 200mil atasema turnover yake ni 20mil, still transactions nyingi kwenye biashara Tanzania hazipiti kwenye mifumo rasmi, hivyo wafanyabiashara wengi hawalipi kodi, matokeo yake wachache wanaolipa wanaminywa sana.
 
ikumbukwe pia presumption ya kodi hufanywa pale mtu unapokuwa hauna mahesabu yoyote, suluhisho ya hili swala ni cashless transaction system ambayo serikali inatarajia kuianzisha before 2023, hapo kila mtanzania atalipa kodi, maana hata ukienda gengeni hautotoa cash, hivyo kwa mfanyabiashara itakuwa rahisi ku track matumizi na mapato ya biashara yake.

Changamoto kubwa ya wafanyabiashara wadogo ni kuwa na record ya mapato bila kuweka record ya matumizi, matokeo yake wakija TRA mtu unashindwa justify matumizi, yani hata wewe mwenyewe ukijaribu balance mambo hayaendi, but with cashless system, kila kitu kitakuwa kipo sorted out.
 
Back
Top Bottom