Kariakoo hakuna changamoto kubwa, wanasiasa uchwara wanalikuza

Nkerejiwa

Senior Member
Feb 25, 2014
146
214
UKWELI MCHUNGU KUHUSU KARIAKOO, KUNA CHANGAMOTO NDOGO LAKINI WANASIASA WANAIKUZA

Anaandika Mchumi Deograsius Andre
(Baadhi ya vitu tusivyopenda kuvisikia kuhusu kariakoo.)

UZI mfupi.

Naomba usome mpaka mwisho uielewe vizuri sana hoja yangu.

Malalamiko ya kodi yaliyoibuka na wafanyabiashara ni ya msingi sana katika kuboresha mfumo mzima wa kodi na urahisi wake kati ya walipaji na wakusanyaji @TRATanzania. Sasa wakati serikali imesema wazi kuwa watalimaliza kwa mazungumzo siku ya jumatano natumai litaisha

ILA
MGOGORO HUU NI TAFULANI PANDE ZOTE MBILI.

Mimi naamini kuwa wafanyabishara wa kariakoo wanaolipa kodi (Wenye maduka) ni wachache sana kuliko wale ambao hawalipi kodi(Machinga). Tena wale wasiolipa kodi ndio wanaofanya biashara zaidi kuliko hata wale wanaolipa kodi.

Hivyo lazima mzigo uwaelemee wale ambao wanalipa kodi. Na cha ajabu hawa machinga wanaweka biashara zao mbele ya maduka ya walipa kodi hivyo kuzuia biashara zao. Na Tuliona juhudi za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam katika kuhakikisha wafanyabiashara hawa wanapangwa zikifeli.

Na zilifelishwa na wafanyabiashara wenyewe. Wengi wanagoma, Wanakimbia ukaguzi ukipita wanarudi. sio kwa ubaya ila hawa machinga ni wajanja wajanja na kwa sababu ni sehemu yao ya kujipatia kipato nisiwasagie kunguni sana. Sasa moja naimani serikali inajua kuwa.

1. Kariakoo ni kitovu cha biashara nchini. Na kama kitaboreshwa basi kodi itakayopatikana pale itakuwa huenda ni kubwa kuliko kodi ya mkoa fulani mzima kwa kipindi fulani.

2. Wafanyabiashara hao hao wanaolalamikia kodi wengi wao sio walipa kodi (wanakwepa kodi).

3. Kodi ni kubwa na wengi wametoa mifano ni kweli lakini mabadiliko ya kodi siyo jambo la siku moja. Inahitaji mchakato kuanzia kwenye importy duty, excise duty, VAT hata Income Tax ili kuleta usawa.

4. Base ya serikali yetu kwenye mapato ni Kodi. Na
Wengi wanakwepa kodi na wengi wanapigia chapuo mfumo wa vitambulisho vya wamaachinga ambao utekelezaji wake ulikua na walakini.

HIVYO BASI.

Kodi siyo fair sawa.
Usajili wa stoo siyo fair ni sawa.
Rushwa kwa mamlaka ni suala la kukemewa na kila mtu hasa @takukuru_tz

LAKINI JE.

Muamko wa wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari upoje. (EFD)
Uongozi wa wafanyabiashara kazi yao ni nini na wao ndio wakuwasemea wafanyabiashara na Kujadiliana na serikali namna ya kusuruhisha migogoro hii kabla ya Kuandamana.

Je kuandamana ni njia sahihi.?
Na maswali mengine ya kujiuliza.

Kwanini sasa na siyo wakati mwingine wote huo?

Ushirikiano huu ungetolewa kipindi cha mchakato wa kupangilia biashara si ingekuwa rahisi kudeal na hili pia.
HOJA YANGU SASA.

1. Wafanyabiashara tunastahili kufanya biashara kwa amani lakini pia tusikwepe wajibu wetu wa kulipa kodi kwa hiyari.

2. Njia sahihi ya kusuruhisha matatizo ya kikodi ni kunegotiate na serikali kupitia uongozi wa wafanyabiashara ndio wajibu wao.

3. @TRATanzania mnasemwa vibaya lakini naimani hamsingiziwi na nyinyi wekeni mikakati yenu vema. Na mikusanye kodi kwa haki.

4. Lakini pia hapa kwetu kodi ya ongezeko la thamani ambayo ilibidi iwe inakusanywa kikamilifu na EFD machine inachepushwa sana. Aidha na wafanyabiashara
Wenyewe ama mamlaka.

5. Serikali hii ambayo inadai kuwa ni sikivu haikupaswa kusubiri hali hii ifike hapa. Ila negotiation ndio suluhu ya jambo hili.

6. Naimani ndugu @KassimMajaliwa_ na jopo lake watalavyoenda kuzungumza na wafanyabiashara basi waangalie pia.

Na suala la mpangilio wa wafanyabiashara kariakoo. Ili kila mtu alipe kodi kulingana na anavyofanya biashara. Na wafanyabiashara pia waache janja janja ya kutumia machinga kukwepa kodi.

NB: Nasisitiza madai yetu wafanyabiashara ni ya msingi lakini pia tuangalie upande wetu.

Na mazingira yetu ya kodi. Je ni nani anaelipa kodi na nani halipi na mbona wote tunafanya biashara. Na vipi juu ya matumizi ya EFD.

Zinaumiza sawa lakini mi sheria na kudeal na sheria ni mchakato

"KWA PAMOJA TUNAWEZA FANYA KARIAKOO KUWA KITOVU CHA BIASHARA NA MAPATO NCHINI"
"Nasimama na Serikali lakini nasimama pia na wafanyabiashara."

1. Uongozi timizeni majukumu yenu
2. Suruhisheni na zungumzeni na serikali kila pale mnapoona mnaonewa msisubiri hali ije kuwa mbaya jukumu lenu ni nini.

Naomba niishie hapa.
Naitwa Deograsius Andrew
 
Baada y siku mbili wamachinga watakosa Cha kuuza nao watajiunga kwenye mgomo, itamlazimu Samia kutinga kariakoo
 
Back
Top Bottom