Wre polite and progressive by day, more tibalist than even the Kenyans by night ..
Ukweli kama huu anaoweza kuusema Jenerali Ulimwengu ndio umewafanya watawala wengi kumwogopa mwanaharakati huyu kushinda hata UKIMWI, nani nchi hii asiyemfahamu Jenerali Ulimwengu? Licha ya mwandishi huyu kukumbwa na misukosuko hata ya kutaka kunyanganywa uraia aah wapi Bwana! Jenerali Ulimwengu hana mpinzani kwa jinsi anavyosimamia ukweli. Pengine kwa waandishi wachanga wenye lengo la kufika alipofika Jenerali waanze mapema kukataa rushwa ambazo huwafanya kutumia kalamu zao kusifia uharamia kuliko kukosoa utawala mbovu, Alleluya Mungu Mwenyezi kwa kutupatia Jenerali Ulimwengu mwenye uwezo wa kuwasemea masikini wan chi hii, mwenye uwezo wa kukemea udini na ukabila , mwenye uwezo wa kumhoji hata rais bila uwoga nani kama Jenerali? Naam Jenerali Ulimwengu ni bakora ya watawala acha iwachape tu!
Nani kama jenerali, Ulimwengu tumwone Nani anayetujali, yu wapi tusemezane Nani tumpe kibali, ukweli akawachane Jenerali Ulimwengu, kiboko ya watawala.
Wamesuka njama nyingi, zote zimegonga mwamba Jenerali ndio kingi, wanyonge tunampamba Wanaoweka vigingi, hao wote ni mafamba Jenerali Ulimwengu, bakora ya watawala
Nani asiyefahamu, Jenerali ni shujaa Yu wapi tumuhukumu, kwa kuzidi kuzubaa Jenerali ni muhimu, Arusha hata kondoa Jenerali Ulimwengu, sindano ya mabwenyenye