Majibu na Maswali yangu kwa Jenerali Ulimwengu

Albert Msando

Verified Member
Nov 2, 2010
1,019
0
Salaam Jenerali,

Kabla sijasema neno kuhusu mada nina angalizo kwenye kichwa cha habari cha mada iliyozaa mjadala ninaoanzisha, "Jenerali...umewaacha mashabiki wako njia panda”. Kwa mtazamo wangu mtu anayeshabikia kitu ni kutokana na sababu fulani, na kwa bahati mbaya ni ngumu kubadili 'ushabiki'. Kwa mfano, ukiniuliza kwa nini mpaka leo nashangilia Liverpool FC sina jibu! Matatizo ninayoyapata kwa kufungwa na timu za ajabu, uchungu anaopata mtoto wangu mwenye umri wa miaka 10! kwa kuona Liverpool inafungwa si mdogo! Namhurumia kwa nini amekuwa mshabiki kwa sababu tu baba yake na yeye ni mshabiki wa timu inayofungwa!
Mbaya zaidi, sijawahi kufikiria 'kuhama' Liverpool na kushabikia timu inayoshinda ingawaje mtoto wangu wa kumzaa anataeseka nayo, mimi nateseka kwa kero za kusemwa na mashabiki wa Man U, Chelsea, Arsenal etc!! Cha kushangaza wachezaji wanahama, na wao ndio wanalipwa! Makocha wanahama, na hao ndio wanaolipwa! Wakichemsha wanafukuzwa!! Mashabiki hawalipwi, hawahami, hawafukuzwi!

Napata tatizo kuwafikiria mashabiki wa Jenerali Ulimwengu walio njia panda! Je ni kina nani? Wana hali gani? Furaha? Huzuni? hawalipwi, sina uhakika kama watahama, ila wanafukuzwa kama hoja zenyewe ndio hizi!! Huo ndio ushabiki! Sasa naomba tulitafakari neno ‘ushabiki’ kwa muda wetu wa baadae ili tuone je ni lazima kumshabikia mtu?

Nikirudi kwenye barua ya Jenerali. Kuna wengine wanaiona nzuri. Labda wako wengi. Kuna wengine inachefua. Na wenyewe wako wengi. Mimi imenikera. Imenikera sana.

Imenikera sio tu kwa sababu ni ndefu na Raisi hataisoma, ni kwa sababu Jenerali analijua hilo lakini kwa makusudi ameamua kutupotosha. Sana sana labda Raisi atasomewa na kama watamsomea wataruka yale ambayo hawataki Raisi ayasikie (kama yapo)
Kwa kuangalia baadhi ya mistari naomba kuonyesha sababu za kero zangu kwa kutumia mistari ilimo kwenye barua hiyo ili kuepuka kukurupuka!! nitarudia maneno yalimo kenye barua hiyo (kwa rangi)

Pili, napenda kukupongeza kwa ushindi uliopata katika uchaguzi uliopita, ushindi uliodhirisha kwa mara nyingine tena jinsi ambavyo wewe kama mwanasiasa unakubalika machoni mwa Watanzania.
Umekuwa ushindi unaodhihirisha imani iliyojengeka katika nyoyo za Watanzania kwamba wewe, Jakaya, utawaongoza vyema ili waondokane na adha zilizowazingira, hususan ufukara uliokithiri na unaoendelea kujijenga kila siku miongoni mwao bila ya kuwapo kwa ishara kwamba viongozi wao wanajua au kujali hali zao.

Anachosema (na anachoamini) Ulimwengu ni kwamba;
i) Ushindi ni ishara ya kukubalika kwa JK.
iii) JK anakubalika machoni mwa watanzania.
Na anaendelea na imani yake;
i) ‘Ushindi’ wa JK unadhihirisha imani
ii) Imani ya watanzania
iii) Imani kwamba JK ataongoza vyema
iv) Watanzania wana adha hususan ufukara
v) Ufukara umekithiri
vi) Ufukara unaendelea kujijenga kila siku
vii) Hakuna ishara kwamba viongozi wanajua au kujali hali hiyo.

Mosi, Jenerali, ni watanzania wapi unawaongelea? Unataka tuamaini kwamba ‘binadamu wote ni sawa’ kwa hiyo watanzania wote wanamkubali JK? Au ni watanzania waliomchagua? Hivi unataka tuamini kwamba watanzania tunafanana sio tu mawazo pia hali zetu za maisha? Na waliokuwa wanamkubali Dr Slaa na Prof Lipumba ni wakenya?? Walikuwa wanasafirishwa kutoka sehemu nyingine kuhudhuria mikutano ya Dr na Prof? na waliopiga kura kwa Dr na Prof wameonyesha ishara gani? Kumkubali JK?

Hii ndio hoja yako?

Sawa, hayo ni mawazo yako Jenerali na haki yako ya Kikatiba kuwaza. Lakini,
Unakubali kwamba ‘watanzania’ wana adha ya ufukara (ingawaje hoja yako inatujumuisha wewe na mimi (watanzania) eti tuna adha ya ufukara!! Huoni tatizo hapo??). Tuendelee, umesema 'ufukara huo unaendelea kujijenga kila siku'. Kwa hiyo unakubali na kulitambua hilo. Sasa Jenerali, ina maana unakubali ufukara umeendelea kujijenga kila siku ikiwa ni pamoja na 2005 mpaka leo!! JK bado hajaingia madarakani? Hiyo imani ya ‘watanzania’ imejengeka lini? 2005 au 2010? Nadhani, kwa maneno yako, ni 2010 na watanzania tumeonyesha ishara kwa kumpa ushindi!!

Ni sababu ipi imekufanya usidiriki kusema moja kwa moja kwa 'mkombozi' haoni ufukara unakua na ni yeye kama kiongozi haonyeshi ishara ya kujali? Au unaongea kwa mafumbo? Kama ulikuwa unamfumba, ili nini?

Unaendelea,
hamasa na mapenzi waliyoonyesha Watanzania kwako tena ni kielelezo kwamba wanayo imani kuwa bado unaweza kuwa mkombozi wao

Jenerali, unataka tuamini kwamba hamasa na mapenzi yanayoonyeshwa kwenye kampeni za uchaguzi ni kielelezo cha imani? Kwa hiyo wanaopewa fedha, ahadi za kufaidi baada ya uchaguzi, nafasi za kuteuliwa kama ahsante, kofia, kanga, sabuni, sukari etc wanasukumwa na imani ya kutaka mkombozi!! Huyo ni wewe kweli au kivuli chako?

Kwa nini wanaamini hivyo, mimi sijui, lakini ukweli ni kwamba hivyo ndivyo wanavyoamini.
Huu ukweli umeupata wapi Jenerali? Umewahi kuniuliza kama naamini hivyo? Unafikiri Sitta anaamini hivyo? Mama Kilango anaamini hivyo? Ni nani anaamini hivyo? Unadai ni watanzania!! Umeongea nao?? Ishara zako unatoa wapi? Kwa kuangalia hamasa na mapenzi wakati wa kampeni za uchaguzi!!?
Jenerali unataka mtu ambaye ni Raisi wa nchi aamini hivyo? Hiyo ndiyo unaita kweli?? Na umeweka wazi tusome ili tujue unachomwambia Raisi! Akikusikiliza sitashangaa ila nitamuachia Mungu.
Ni kwa nini umerudia hiyo barua? Huku ukijua kabisa umeirudia, umeandika kama vile JK ameingia madarakani kwa mara ya kwanza. Hivi kabla ya kuwa Raisi JK alikuwa si kiongozi? Hakuwa waziri? Wakati nchi ilipozama JK alikuwa wapi? Unasema amerithi mzigo, maneno hayo yanatoka moyoni mwako??

Hoja yangu Jenerali

a) JK alikuwa kiongozi kabla ya mwaka 2005. Alikuwa ni waziri. Na kama ulivyosema alianza kusafiri nje ya nchi toka mwaka 1974 mlivyokutana Bulgaria na bado anasafiri!!! Nchi imeanza kuzama lini? Tuambie!!

b) Ufukara haujaanza leo wala jana. Ulipoanzia JK alikuwepo kama kiongozi mwenye nafasi ya kuupunguza hata kama hakuwa Raisi au alikuwa ni mmoja wa waliosabanisha ufukara huo na alikuwa anaona nchi ikizama. Akaacha izame leo hii anataka kuitoa ilipozama!! Kama ni kwenye maji hata akiitoa si itakuwa na kutu na injini haifanyi kazi? Ni sawa na kwenda kuitoa MV Bukoba ziwani sasa hivi wakati uliicha ikzame! Kwa nini hakuzuia isizame? Huoni kwamba angekuwa ni shujaa badala ya ‘mkombozi’? Tunataka shujaa na siyo mkombozi!! Usinikwaze na kunisabisha nikatenda dhambi! angeanza na ushujaa ndio atukomboe

c) Chama kilichomlea JK na watangulizi wake ni kile kile kinacholaumiwa kusababisha ufukara huo! Na umekubali unajijenga kila siku (hata ile miaka ambayo JK amekuwa Raisi. Labda kwako miaka 5 sio mingi, lakini kwa mtu asiye na ada ya mtoto, asiye na uhakika wa mlo, asiye na nyumba bora, asiye na uwezo wa kuvaa mavazi mazuri, asiyejua mimi na wewe tunaongea nini hapa kwa sababu hajui kusoma, hana internet au computer, umeme nk. Miaka mitano no mingi sana! Sana! Unawazungumzia imani yao na unaifikisha kwa Raisi yule yule aliyekuwepo miaka 5 iliyopita! Utasema ni kukumbushana??

Unamkumbusha jina lake au nini? Hivi naweza kukumbusha wewe unaitwa Jenerali Ulimwengu?? Miaka yote umeitwa hivyo iweje umesahau jina lako? Ina maana JK anaweza kusahau shida za watanzania au majukumu ya kiongozi wa nchi umeamua kumkubusha??

d) Imani ya kwamba JK ni mkombozi ni potofu. Umeileta wewe. Huna mamlaka yoyote ya kuwazungumzia watanzania. Huwezi ukawaongelea ‘watanzania’ kwa upotoshaji mkubwa kama huo. Huo ni ushabiki! Na nimesema kuhusu tatizo la ushabiki. Unajua wazi kabisa JK amekuwepo siku zote kama kiongozi katika nchi hii. Serikali zote mbili zilizopita alikuwepo. Alifanya nini? Labda umkumbushe hayo mazuri aliyoyafanya na utukumbushe na sisi!

e) Kwa nini usimkumbushe Raisi mazuri au mabaya aliyoyafanya badala ya kutuletea porojo na kutusababishia hasira na kututendesha dhambi?? Kama kweli unaweza kusimamia ukweli ungemwambia Raisi haya yafuatayo;

i) Miaka 5 ya uongozi wake ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama ilivyotarajiwa kama Raisi.

ii) Kwa miaka 5 ameendelea kutokujali ufukara ambao umeendelea kujengeka. Hii hoja ungeiweka wazi bila kumumunya maneno na kuficha ficha!

iii) Baraza la mawaziri lililopita lilikuwa hovyo na halikumsaidia katika utendaji.

Kwa sasa inatosha kusema kwamba mawaziri utakaowateua, na watendaji wengine wengi unaoruhusiwa kuwateua, hao ndio watakaounda timu yako. Hawa wote ni wachezaji; wewe ndiye kocha au meneja. Timu ikicheza vibaya, ikafungwa wewe ndiye wa kulaumiwa. Ikicheza vizuri ikashinda, wewe ndiye wa kusifiwa.

Hukuwa na sababu ya kuongelea mawaziri wapya kabla hujasema tatizo la waliopita ambao wengine atawarudisha!! Kwa nini unaongelea ‘timu ikicheza’ wakati imeshacheza?? Si utumie mfano uliopo badala ya ‘abstracts’!! alishateua mawaziri kabla kuwa mkweli na useme walifanya vizuri au vibaya! Mwambie asikie!

iv) Kujuana kulikuwa kwingi katika nafasi zote za utendaji. Watu wengine waliteuliwa ili kuondoa mipasuko na kuvunja makundi. Siasa!! Hao wamemponza sana.

v) Amezungukwa na watu kama wewe. Kusema ukweli wanaanza na maneno mengi ya kupaka mafuta, wanazunguka weeee, wanaremba remba maneno na kumuaminisha kwamba tatizo si yeye ila ni wengine!! Hawamwambii ukweli kama ulivyo kwa kuogopa kwamba Raisi atajisikia vibaya!

Ni vyema ukasema ukweli na ukausimamia kama ulivyo. Maneno yako;
Lakini ninaamini kwamba unanijua vyema na unaelewa kwamba kujadili masuala kama haya ni sehemu ya jinsi nilivyo. Iwapo kati ya mambo nitakayoyasema katika waraka huu yatakuudhi, natanguliza kuomba radhi; na iwapo yatakuchosha, naomba uyatupilie mbali.
Sio tu tuishie kwenye kujadili, ni lazima tuishi tunayoyazungumza!! Sioni ni kwanini Raisi ataudhika na uliyoyasema. Hakuna jipya, ingekuwa hivyo angeudhika kila siku akiangalia maisha ya wananchi wengi fukara na masikini! ndio hali halisi.
Angeudhika kwa kuangalia picha za maelfu ya wananchi waliokuwa wakihudhuria mikutano ya Dr na Prof huku wakitoa hisia zao! Angeudhika kwa kuangalia wabunge wa CCM walioangushwa kwa aibu au waliozomewa na wananchi mbele yake.

Angeudhika na upuuzi unaofanywa na baadhi ya maofisa wa juu wenye kutegemewa katika taifa ambao wanakurupuka wanatoa taarifa za kupotosha bila kufikiria athari zake. Kwa mfano Jeshi wakati wa uchaguzi, PCCB wakati wa kumsafisha Chenge……hayo ni maudhi!! Lakini sijaona kama yamemuudhi Raisi wetu ndio maana unaona mpaka sasa wanaendelea na maisha yeye unamshauri aendelee kutabasamu na asikunje sura!! Mungu anatuona!!
Angalizo: kumuachia Mungu ni kwa sababu sijaona mtu mwingine wa kumuachia! Yeye pekee ndie tegemeo letu kwa hapa tulipofika, samahani, tulipofikishwa!!!

Wasalaam.

tartoo

Senior Member
Jul 2, 2010
129
0
Salaam Jenerali,

Kabla sijasema neno kuhusu mada nina angalizo kwenye kichwa cha habari cha mada iliyozaa mjadala ninaoanzisha, "Jenerali...umewaacha mashabiki wako njia panda". Kwa mtazamo wangu mtu anayeshabikia kitu ni kutokana na sababu fulani, na kwa bahati mbaya ni ngumu kubadili 'ushabiki'. Kwa mfano, ukiniuliza kwa nini mpaka leo nashangilia Liverpool FC sina jibu! Matatizo ninayoyapata kwa kufungwa na timu za ajabu, uchungu anaopata mtoto wangu mwenye umri wa miaka 10! kwa kuona Liverpool inafungwa si mdogo! Namhurumia kwa nini amekuwa mshabiki kwa sababu tu baba yake na yeye ni mshabiki wa timu inayofungwa!
Mbaya zaidi, sijawahi kufikiria 'kuhama' Liverpool na kushabikia timu inayoshinda ingawaje mtoto wangu wa kumzaa anataeseka nayo, mimi nateseka kwa kero za kusemwa na mashabiki wa Man U, Chelsea, Arsenal etc!! Cha kushangaza wachezaji wanahama, na wao ndio wanalipwa! Makocha wanahama, na hao ndio wanaolipwa! Wakichemsha wanafukuzwa!! Mashabiki hawalipwi, hawahami, hawafukuzwi!

Napata tatizo kuwafikiria mashabiki wa Jenerali Ulimwengu walio njia panda! Je ni kina nani? Wana hali gani? Furaha? Huzuni? hawalipwi, sina uhakika kama watahama, ila wanafukuzwa kama hoja zenyewe ndio hizi!! Huo ndio ushabiki! Sasa naomba tulitafakari neno ‘ushabiki' kwa muda wetu wa baadae ili tuone je ni lazima kumshabikia mtu?

Nikirudi kwenye barua ya Jenerali. Kuna wengine wanaiona nzuri. Labda wako wengi. Kuna wengine inachefua. Na wenyewe wako wengi. Mimi imenikera. Imenikera sana.

Imenikera sio tu kwa sababu ni ndefu na Raisi hataisoma, ni kwa sababu Jenerali analijua hilo lakini kwa makusudi ameamua kutupotosha. Sana sana labda Raisi atasomewa na kama watamsomea wataruka yale ambayo hawataki Raisi ayasikie (kama yapo)
Kwa kuangalia baadhi ya mistari naomba kuonyesha sababu za kero zangu kwa kutumia mistari ilimo kwenye barua hiyo ili kuepuka kukurupuka!! nitarudia maneno yalimo kenye barua hiyo (kwa rangi)

Pili, napenda kukupongeza kwa ushindi uliopata katika uchaguzi uliopita, ushindi uliodhirisha kwa mara nyingine tena jinsi ambavyo wewe kama mwanasiasa unakubalika machoni mwa Watanzania.
Umekuwa ushindi unaodhihirisha imani iliyojengeka katika nyoyo za Watanzania kwamba wewe, Jakaya, utawaongoza vyema ili waondokane na adha zilizowazingira, hususan ufukara uliokithiri na unaoendelea kujijenga kila siku miongoni mwao bila ya kuwapo kwa ishara kwamba viongozi wao wanajua au kujali hali zao.

Anachosema (na anachoamini) Ulimwengu ni kwamba;
i) Ushindi ni ishara ya kukubalika kwa JK.
iii) JK anakubalika machoni mwa watanzania.
Na anaendelea na imani yake;
i) ‘Ushindi' wa JK unadhihirisha imani
ii) Imani ya watanzania
iii) Imani kwamba JK ataongoza vyema
iv) Watanzania wana adha hususan ufukara
v) Ufukara umekithiri
vi) Ufukara unaendelea kujijenga kila siku
vii) Hakuna ishara kwamba viongozi wanajua au kujali hali hiyo.

Mosi, Jenerali, ni watanzania wapi unawaongelea? Unataka tuamaini kwamba ‘binadamu wote ni sawa' kwa hiyo watanzania wote wanamkubali JK? Au ni watanzania waliomchagua? Hivi unataka tuamini kwamba watanzania tunafanana sio tu mawazo pia hali zetu za maisha? Na waliokuwa wanamkubali Dr Slaa na Prof Lipumba ni wakenya?? Walikuwa wanasafirishwa kutoka sehemu nyingine kuhudhuria mikutano ya Dr na Prof? na waliopiga kura kwa Dr na Prof wameonyesha ishara gani? Kumkubali JK?

Hii ndio hoja yako?

Sawa, hayo ni mawazo yako Jenerali na haki yako ya Kikatiba kuwaza. Lakini,
Unakubali kwamba ‘watanzania' wana adha ya ufukara (ingawaje hoja yako inatujumuisha wewe na mimi (watanzania) eti tuna adha ya ufukara!! Huoni tatizo hapo??). Tuendelee, umesema 'ufukara huo unaendelea kujijenga kila siku'. Kwa hiyo unakubali na kulitambua hilo. Sasa Jenerali, ina maana unakubali ufukara umeendelea kujijenga kila siku ikiwa ni pamoja na 2005 mpaka leo!! JK bado hajaingia madarakani? Hiyo imani ya ‘watanzania' imejengeka lini? 2005 au 2010? Nadhani, kwa maneno yako, ni 2010 na watanzania tumeonyesha ishara kwa kumpa ushindi!!

Ni sababu ipi imekufanya usidiriki kusema moja kwa moja kwa 'mkombozi' haoni ufukara unakua na ni yeye kama kiongozi haonyeshi ishara ya kujali? Au unaongea kwa mafumbo? Kama ulikuwa unamfumba, ili nini?

Unaendelea,
hamasa na mapenzi waliyoonyesha Watanzania kwako tena ni kielelezo kwamba wanayo imani kuwa bado unaweza kuwa mkombozi wao

Jenerali, unataka tuamini kwamba hamasa na mapenzi yanayoonyeshwa kwenye kampeni za uchaguzi ni kielelezo cha imani? Kwa hiyo wanaopewa fedha, ahadi za kufaidi baada ya uchaguzi, nafasi za kuteuliwa kama ahsante, kofia, kanga, sabuni, sukari etc wanasukumwa na imani ya kutaka mkombozi!! Huyo ni wewe kweli au kivuli chako?

Kwa nini wanaamini hivyo, mimi sijui, lakini ukweli ni kwamba hivyo ndivyo wanavyoamini.
Huu ukweli umeupata wapi Jenerali? Umewahi kuniuliza kama naamini hivyo? Unafikiri Sitta anaamini hivyo? Mama Kilango anaamini hivyo? Ni nani anaamini hivyo? Unadai ni watanzania!! Umeongea nao?? Ishara zako unatoa wapi? Kwa kuangalia hamasa na mapenzi wakati wa kampeni za uchaguzi!!?
Jenerali unataka mtu ambaye ni Raisi wa nchi aamini hivyo? Hiyo ndiyo unaita kweli?? Na umeweka wazi tusome ili tujue unachomwambia Raisi! Akikusikiliza sitashangaa ila nitamuachia Mungu.
Ni kwa nini umerudia hiyo barua? Huku ukijua kabisa umeirudia, umeandika kama vile JK ameingia madarakani kwa mara ya kwanza. Hivi kabla ya kuwa Raisi JK alikuwa si kiongozi? Hakuwa waziri? Wakati nchi ilipozama JK alikuwa wapi? Unasema amerithi mzigo, maneno hayo yanatoka moyoni mwako??

Hoja yangu Jenerali

a) JK alikuwa kiongozi kabla ya mwaka 2005. Alikuwa ni waziri. Na kama ulivyosema alianza kusafiri nje ya nchi toka mwaka 1974 mlivyokutana Bulgaria na bado anasafiri!!! Nchi imeanza kuzama lini? Tuambie!!

b) Ufukara haujaanza leo wala jana. Ulipoanzia JK alikuwepo kama kiongozi mwenye nafasi ya kuupunguza hata kama hakuwa Raisi au alikuwa ni mmoja wa waliosabanisha ufukara huo na alikuwa anaona nchi ikizama. Akaacha izame leo hii anataka kuitoa ilipozama!! Kama ni kwenye maji hata akiitoa si itakuwa na kutu na injini haifanyi kazi? Ni sawa na kwenda kuitoa MV Bukoba ziwani sasa hivi wakati uliicha ikzame! Kwa nini hakuzuia isizame? Huoni kwamba angekuwa ni shujaa badala ya ‘mkombozi'? Tunataka shujaa na siyo mkombozi!! Usinikwaze na kunisabisha nikatenda dhambi! angeanza na ushujaa ndio atukomboe

c) Chama kilichomlea JK na watangulizi wake ni kile kile kinacholaumiwa kusababisha ufukara huo! Na umekubali unajijenga kila siku (hata ile miaka ambayo JK amekuwa Raisi. Labda kwako miaka 5 sio mingi, lakini kwa mtu asiye na ada ya mtoto, asiye na uhakika wa mlo, asiye na nyumba bora, asiye na uwezo wa kuvaa mavazi mazuri, asiyejua mimi na wewe tunaongea nini hapa kwa sababu hajui kusoma, hana internet au computer, umeme nk. Miaka mitano no mingi sana! Sana! Unawazungumzia imani yao na unaifikisha kwa Raisi yule yule aliyekuwepo miaka 5 iliyopita! Utasema ni kukumbushana??

Unamkumbusha jina lake au nini? Hivi naweza kukumbusha wewe unaitwa Jenerali Ulimwengu?? Miaka yote umeitwa hivyo iweje umesahau jina lako? Ina maana JK anaweza kusahau shida za watanzania au majukumu ya kiongozi wa nchi umeamua kumkubusha??

d) Imani ya kwamba JK ni mkombozi ni potofu. Umeileta wewe. Huna mamlaka yoyote ya kuwazungumzia watanzania. Huwezi ukawaongelea ‘watanzania' kwa upotoshaji mkubwa kama huo. Huo ni ushabiki! Na nimesema kuhusu tatizo la ushabiki. Unajua wazi kabisa JK amekuwepo siku zote kama kiongozi katika nchi hii. Serikali zote mbili zilizopita alikuwepo. Alifanya nini? Labda umkumbushe hayo mazuri aliyoyafanya na utukumbushe na sisi!

e) Kwa nini usimkumbushe Raisi mazuri au mabaya aliyoyafanya badala ya kutuletea porojo na kutusababishia hasira na kututendesha dhambi?? Kama kweli unaweza kusimamia ukweli ungemwambia Raisi haya yafuatayo;

i) Miaka 5 ya uongozi wake ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama ilivyotarajiwa kama Raisi.

ii) Kwa miaka 5 ameendelea kutokujali ufukara ambao umeendelea kujengeka. Hii hoja ungeiweka wazi bila kumumunya maneno na kuficha ficha!

iii) Baraza la mawaziri lililopita lilikuwa hovyo na halikumsaidia katika utendaji.

Kwa sasa inatosha kusema kwamba mawaziri utakaowateua, na watendaji wengine wengi unaoruhusiwa kuwateua, hao ndio watakaounda timu yako. Hawa wote ni wachezaji; wewe ndiye kocha au meneja. Timu ikicheza vibaya, ikafungwa wewe ndiye wa kulaumiwa. Ikicheza vizuri ikashinda, wewe ndiye wa kusifiwa.

Hukuwa na sababu ya kuongelea mawaziri wapya kabla hujasema tatizo la waliopita ambao wengine atawarudisha!! Kwa nini unaongelea ‘timu ikicheza' wakati imeshacheza?? Si utumie mfano uliopo badala ya ‘abstracts'!! alishateua mawaziri kabla kuwa mkweli na useme walifanya vizuri au vibaya! Mwambie asikie!

iv) Kujuana kulikuwa kwingi katika nafasi zote za utendaji. Watu wengine waliteuliwa ili kuondoa mipasuko na kuvunja makundi. Siasa!! Hao wamemponza sana.

v) Amezungukwa na watu kama wewe. Kusema ukweli wanaanza na maneno mengi ya kupaka mafuta, wanazunguka weeee, wanaremba remba maneno na kumuaminisha kwamba tatizo si yeye ila ni wengine!! Hawamwambii ukweli kama ulivyo kwa kuogopa kwamba Raisi atajisikia vibaya!

Ni vyema ukasema ukweli na ukausimamia kama ulivyo. Maneno yako;
Lakini ninaamini kwamba unanijua vyema na unaelewa kwamba kujadili masuala kama haya ni sehemu ya jinsi nilivyo. Iwapo kati ya mambo nitakayoyasema katika waraka huu yatakuudhi, natanguliza kuomba radhi; na iwapo yatakuchosha, naomba uyatupilie mbali.
Sio tu tuishie kwenye kujadili, ni lazima tuishi tunayoyazungumza!! Sioni ni kwanini Raisi ataudhika na uliyoyasema. Hakuna jipya, ingekuwa hivyo angeudhika kila siku akiangalia maisha ya wananchi wengi fukara na masikini! ndio hali halisi.
Angeudhika kwa kuangalia picha za maelfu ya wananchi waliokuwa wakihudhuria mikutano ya Dr na Prof huku wakitoa hisia zao! Angeudhika kwa kuangalia wabunge wa CCM walioangushwa kwa aibu au waliozomewa na wananchi mbele yake.

Angeudhika na upuuzi unaofanywa na baadhi ya maofisa wa juu wenye kutegemewa katika taifa ambao wanakurupuka wanatoa taarifa za kupotosha bila kufikiria athari zake. Kwa mfano Jeshi wakati wa uchaguzi, PCCB wakati wa kumsafisha Chenge……hayo ni maudhi!! Lakini sijaona kama yamemuudhi Raisi wetu ndio maana unaona mpaka sasa wanaendelea na maisha yeye unamshauri aendelee kutabasamu na asikunje sura!! Mungu anatuona!!
Angalizo: kumuachia Mungu ni kwa sababu sijaona mtu mwingine wa kumuachia! Yeye pekee ndie tegemeo letu kwa hapa tulipofika, samahani, tulipofikishwa!!!

Wasalaam.

Crapppp!!!!!!!:nono:
 
Lorah

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
1,193
0
Kejeli jamani...
saa nyingine inawezekana nikumvika mtu kilemba cha ukoka
 
Sn2139

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
835
500
Crapppp!!!!!!!:nono:

Sio crap, ni ujumbe muhimu sana, si kwa Ulimwengu na Kikwete peke yake, bali kwa jamii nzima ya wa-Tz ambao tunakosa ujasiri wa kusema ukweli na kuusimamia.

Ndugu Tartoo naomba usome tena ujumbe huo ukiwa umetulia. Kama wewe si mnafiki utakubaliana na huyo ndugu MsandoAlberto. Mimi nampongeza kwa ujumbe wake.
 
Mfwatiliaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
1,325
0
Mkuu MA
yaani umenifanye nilengwe na machozi ya huzuni ulivyochambua mantiki ya ujumbe aliotupelekea Comrade Ulimwengu.
Huyu bwana nadhani tayari ameshachakachuliwa na kundi la mafisadi waliochangia kuliangamiza taifa hili, ambao anakuwa nao kila jioni kwenye ile klabu maarufu pale Upanga.
Anyway, nitamuuliza kulikoni..at the moment, clarification is very crucial, hatuwezi kuendelea kuongeza madonda mapya ya kuuguza wakati yaliyopo bado hayajapona!!
 
sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
397
195
Hayo ni maoni yake,na Jenerali pia alitoa yake na mkumbuke hiyo barua imetoka kwenye gazeti la wiki iliyopita si mpya bali ni ukumbusho wa kile alichoandika wakata huo Jk anaingia madarakani.Hivyo Ulimwengu anao uhuru wa kuamua ni namna gani atoe ujumbe kwani yeye anaelewa mlengwa ndio ujumbe utamfikia vizuri.Pia jamaa walishamvua uraia ni katika maswala ya kutetea haki za wananchi,Ombi langu kwa MsandoAlberto iweke sawa hiyo makala yako halafu ichapishwe kwenye magazeti husika.
 
Mzalendo80

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
2,509
2,000
Nasema hivi Kikwete sio Rais wangu, Dr.Slaa ndio rais wangu. Jen Ulimwengu ni fisadi tu hana mpango wowote katika hii nchi yetu zaidi ya kuenzi ufisadi. Kikwete ni mchakachuaji na hakubaliki na Watanzania labda kwa wana ccm na familia ya Jen Ulimwengu ndio anakubalika, lakini sisi watanzania hatumkubali anaongoza kiditekta kama Mugabe. Nina imani kuwa kikwete hakubaliki zaidi ya watu 2Mil waliobakia wote waliongezewa kwenye uchakachuaji.
 
Albert Msando

Verified Member
Nov 2, 2010
1,019
0
At least you have read it. Imagine now you have a President and or a Minister who doesnt read to reach a judgment like yours!! You could be a better President or Minister! You read crap and can tell the difference (even if its your way).
 
Ncha

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
254
195
Ulimwengu akimaliza kuchapa yake MA nae apost. then wasomaji tupime.
 
Deo

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
1,218
1,250
Fasihi ni ngumu. Mwalimu wangu aliitwa Kizelahabi nikiwa fomutu. Namkumbuka anisaidie nilitoroka darasa siku zile
 
Mauza uza

JF-Expert Member
Jul 24, 2008
2,099
2,000
MA uko juu umechambua kinagaubaga utumbo wa JU na mafisadi waliomzunguka JK.kula tano.
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,114
2,000
Hayo ni maoni yake,na Jenerali pia alitoa yake na mkumbuke hiyo barua imetoka kwenye gazeti la wiki iliyopita si mpya bali ni ukumbusho wa kile alichoandika wakata huo Jk anaingia madarakani.Hivyo Ulimwengu anao uhuru wa kuamua ni namna gani atoe ujumbe kwani yeye anaelewa mlengwa ndio ujumbe utamfikia vizuri.Pia jamaa walishamvua uraia ni katika maswala ya kutetea haki za wananchi,Ombi langu kwa MsandoAlberto iweke sawa hiyo makala yako halafu ichapishwe kwenye magazeti husika.

mimi ni mmoja wa "mashabiki" wa Jenerali Ulimwengu. nilianza kumfuatilia alipokuwa mkuu wa wilaya, nadhani Ilala (kama sikosei), mbunge, na enzi zile za group of 77. nilimuona kama mtu wa aina yake hapa Tz. mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo, anajua lugha nyingi, msomaji mzuri wa vitabu, majarida na "visomwa" mbalimbali, aina ya mtu ambaye ni adimu sana hapa Tz.

alipoanzisha gazeti la RAI (Nguvu ya Hoja), nilifarijika sana kusoma gazeti lililosheheni ujenzi wa hoja na ukuzaji wa fikra. nilipata tatizo kidogo alipokuwa mpiga kampeni mkuu wa Mkapa mwaka 1995. kwa mawazo yangu wakati ule, watu kama Jenerali walitakiwa wawe moderators, wakichambua pumba na mchele kwa kutumia akili zao pevu walizojaliwa na Mungu, na kuwashauri wanamageuzi na wanaccm namna bora ya kucheza mchezo ulio fair. kitendo cha Jenerali kujitupa nyuma ya Mkapa, akimpa kila aina ya sifa, na kuwepo katika campaign team yake, niliona kama ni usaliti fulani kwa maslahi ya taifa letu. lakini pia niliona anayo haki ya kuwa na msimamo wake binafsi kwa hiyo niliishia kujifariji tu kwamba nitaendelea kuwa shabiki wake kwa uzito wa hoja zake na upevu wa uchambuzi wake.

kwa upande mwingine, kitendo cha Jenerali kusimama pamoja na Mkapa wakati anatangaza nia yake ya kugombea urais enzi hizo za 1995, na baadae kumpigia kampeni kubwa sana, na kweli alishinda, na kuendelea kumsifia na kutoa ushauri katika siku za mwanzo za rais Mkapa, kilinifanya nimuone kama mtu anayeona mbali kweli. kampa sapoti mtu ambaye kweli ameshinda, amecheza karata yake kwa "winner". ila baada ya fallout yake na Mkapa, akaanza kumchambua kwelikweli. Jenerali huyo huyo akawa ni mwiba kwa serikali ya Mkapa. tatizo nini? hakupewa angalau ka cheo? maana hoja nzito alizojenga kwa Mkapa ilikuwaje zime expire kwa muda mfupi tu, na kugeuka kuwa shubiri? kwa bahati mbaya haya yalijirudia wakati wa JK. ikumbukwe kwamba ni magazeti ya Habari corporation yaliyotumika kummaliza Salim, kwa kumzushia machafu kibao. baada ya uchaguzi ndio akaanza na barua ndefu kwa Jakaya. yale yale! sasa mwenzake Salva Rweyemamu kaukwaa, na wengine siwakumbuki majina yao kwa sasa. Jenerali hakupata kitu.

sasa baada ya hapo ndio magazeti ya Habari Corporation tukaona yanamilikiwa na Rostam. baadaye Jenerali akaibuka na Raia Mwema, kuendeleza ile falsafa ya RAI. Rostam, kwa kuamini kwamba watu wanalipenda RAI kwa sababu ya jina lake sijui, mara baada ya kulimiliki, akaanza kujaza "hoja" zake humo. nadhani sasa RAI sio nguvu ya hoja tena, bali ni NGUVU YA MAFISADI. na wapenzi wa RAI bila shaka si wale wachambuzi wa hoja wa enzi zile. turudi kwa Jenerali. inaonekana kwamba Rais anapoingia madarakani, Jenerali humpamba na kumsifia. baadae anamgeuka. napendekeza kwamba Jenerali anafanya haya yote kwa maslahi binafsi. kwa nafasi yake, upana wake wa akili na mawazo, kama angekuwa kweli mwanamageuzi kutoka rohoni mwake, angetusaidia sana hapa Tz. lakini amechagua kutumia uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja, kufanya mambo ambayo mtu ungeweza kusema anatuliza njaa zake mwenyewe, na uchu wa "power" uliofichika.

ila kwa hili la kuchukua barua ya Jakaya ya enzi zile na kuichapisha tena vile ilivyo, hapo Jenerali amechemka. siyo yule Jenerali ninayemfahamu. mazingira ya barua ile wakati wa ushindi wa kishindo wa asilimia 80, tena kama ni kuchakachua basi kwa mbali mno (si unajua tena mwizi lazima aibe tu, hata kama ni kujiibia mwenyewe), sio mazingira ya asilimia 61 ya kulazimisha na kuchakachua. nguvu iliyotumika na ccm na dola 2010 kukirejesha ccm madarakani, ambapo hata wanaccm wengi tu wamepigia kura upinzani, ni ushahidi tosha kwamba mazingira haya ni tofauti na ya 2005. Jenerali pia anayo miaka 5 ya JK ambayo angeweza kuifanyia tathmini, au kiutumia katika kumulika "barua" hii ya sasa. iweje Jenerali atupe desa la 2005 wakati tupo katika mazingira tofauti kabisa? yaani anatupatia majibu yaleyale ya mtihani uliotoka 2005, wakati mtihani wa 2010 ni tofauti kabisa!

nawasilisha
 
Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,862
0
Miye nilisema tangu zamani kwamba waandishi wengi wa habari hapa nchini wanaandika kwa kusukumwa na 'tumbo' tu. Inawezekana Generali yupo kwenye mawindo ya 'ulaji' kwenye awamu hii ya mwisho ya jk. Nahisi Generali amekumbuka msemo unaosema 'ukishindwa kupambana na adui basi jiunge nae'.
 
Muadilifu

Senior Member
Sep 26, 2007
150
195
Nadhani hatujamuelewa Jenerali. Naamini aliamua kuichapa tena (ikiwa na marekebisho kidogo) barua aliyomuandikia JK mwaka 2005 ili JK mwenyewe pamoja na wasaidizi wake wajipime kutokana na ujumbe wa barua hiyo. Mimi sina shida nayo kabisa.
 
LeopoldByongje

JF-Expert Member
Apr 28, 2008
372
0
Naona mjadala ni Mzuri. Angalizo. Kwa aliyeisoma Makala hiyo Jenerali Ulimwengu katika utangulizi alieleza kuwa barua hiyo aliiandika Mawaka 2005. Kwa hiyo isomwe katika Mkhtaza wa 2005 na ulinganishe 2010. Makala hiyo itahitimishwa wiki hii. Na hapo ndipo tutajua Jenerali anataka kutupa ujumbe gani. Mimi nashauri tuache ushabiki tusome na tujadili hoja.
 
Albert Msando

Verified Member
Nov 2, 2010
1,019
0
naomba turudie maneno ya Jenerali,

Kwa kuwa mazingira ya wakati huo na ya leo yanashabihiana sana, na kwa kuwa bado Barua ile Ndefu ya Wazi ina hoja ambazo zinatukumbusha yaliyopita na kututabiria yajayo, tunairejea barua hiyo ambayo maudhui yake yanabaki yaleyale hata kama imehaririwa hapa na pale kusahihisha makosa ya chapa.

jenerali hajasema 'mazingira' ya wakati ule na ya leo ni yapi! Je alikuwa anamaanisha kwamba JK ameshinda kwa asilimia zile zile? Kwa sababu hajaweka wazi mazingira yapi anayazungumzia bado kuna tatizo katika hoja yake! Kwa mtazamo wangu 'mazingira' ya wakati ule na sasa ni tofauti sana!!

JK 'ameshindwa' uchaguzi 2010. Anguko la anachokiita hamasa na upenzi (angalia asilimia alizopata na wabunge wa chama chake walioanguka) ni ishara ya kushindwa hata kama alipata kura za kumtosha kuendelea kuwa Raisi. Huitaji akili ya kupeleka roketi kuona hilo! Mazingira yanawezaje kuwa sawa? Hata ufukara anaozungumzia Jenerali hauko kwa kiasi kile kile. Kama 2005 ilikuwa ni ufukara, sasa hivi ni ufukara uliokithiri. Ni vitu viwili tofauti.

Maudhui ya barua hiyo ni nini? Kumkumbusha JK majukumu yake? Inawezekana amesahau? Kuna tofauti kubwa sana ya kusahau na kutojua. Inawezekanaje JK asahau? Kwa nini sio kwamba hajui? Ni vigezo vipi Jenerali anatumia kushawishi kwamba JK amesahau na sio kwamba hajui?

Maswali yangu yanatokana na maneno yake;

Lakini ni lazima yatajwe mara kwa mara, ili tujikumbushe na tusije tukayasahau, kwani yanaweza kusahauliwa. Tulimsikia Rais Mstaafu kabla yako akisema kwamba katika uongozi wake wa miaka kumi alisahau kilimo. Sasa, kama inawezekana kusahau kile kinachoitwa "uti wa mgongo" wa uchumi wa taifa, sembuse "kucha" kama michezo!

Hivyo, basi tukumbushane kila wakati majukumu yetu. Nasema yetu, kwa sababu si yako peke yako. Hili ni jambo ambalo linahitaji kusisitizwa. Majukumu haya ni yetu sote, sote raia wa Tanzania, na kila anayetutakia mema. Tukilitambua hili, tutakuwa tumeepuka mtego wa kukusabilia wewe na serikali yako kila mzigo wa Taifa.

Lengo ni kukumbushana. Hili ni lengo jepesi sana. Sikubaliani na Jenerali hata kidogo. JK hajasahau. HAJASAHAU. HAIWEZEKANI.

Mkapa hakusahau kilimo, alikipuuza. Hakukijali.

Kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini, Kilimanjaro Mkapa alisema hadharani kwamba wananchi wa Kata hiyo wamsubiri arudi akishaenda Dar es Salaam atawapelekea majibu kuhusu mradi wa maji ya umwagiliaji wa Kikuletwa kwa sababu wananchi hao walimchagua Mbunge wa Upinzani (kipindi hicho) Ndugu Ngawaiya!!

Haikuwa kusahau, ilikuwa ni dharau kwa wananchi na taifa. Na Jenerali kusema bila kukemea upuuzi wa 'kusahau kilimo' ni tatizo. Yeye sio mtu wa kusema tu!! Anakosaje ujasiri wa kukemea???

Hiyo barua hakuna haja ya kuimalizia. Kama ni yale yale aliyosema 2005 basi tutatoa photocopy na 'kuisoma'. Kwa nini apoteze ukurasa (kurasa) za gazeti kurudia kitu ambacho alishakiandika na ametuambia ndio hicho hicho ataendelea nacho?? Ni heri Wanajamii tutoe photocopy tusambaze kokote tulipo!! Kila mtu akitoa copy mbili kwa sh. 100 tutazambaza copy nyingi kuliko nakala za magazeti na nafasi hiyo iandikwe habari nyingine yenye maana zaidi!!

Ni haki yake kutoa maoni kama ilivyo haki yangu na wengine kujibu. lakini pia ikumbukwe hana haki ya kupotosha. Ni vyema akatumia haki yake ya kukemea na kuonya. JK na Mawaziri wake si wakushauriwa, ni wa kuonywa. Hatuwezi kuendelea kumshauri Hosea, Sijui Mnadhimu wa Jeshi, Kamishna wa Usalama wa Taifa kwa kufanya maamuzi ya ajabu ajabu! Toka lini Kamishna wa Usalama wa taifa ukatokeza hadharani ovy ovyo hata kama mtu kasema uongo??? Kuna tofauti gani ya kuwa Kamishna na Katibu Mwenezi wa Chama??? Au wameambukizwa akili za Makamba??

Leo hii kiongozi kama Makamba anaulizwa swali na mwandishi wa habari anamjibu 'ningekuwa na namba ya simu ya mkeo ningempigia na yeye achukue fomu za uspika' anaulizwa swali lingine anajibu 'ulitaka nikamfunge Chenge mdomo kwa kamba'. Huyo ni kiongozi, Katibu Mkuu wa Chama chenye Serikali!! Sasa huyu naye tumshauri au ni kukanywa na kuwajibishwa??

Wale wote wanaotaka hii nchi iende kwa kuremba remba wakae pembeni. Hakuna muda wa kushauriana, watu wafanye kazi maendeleo ya kweli yaonekane basi!! Ushauri tutawaachia viongozi wa dini!! Acha wao washauri kwanza wana a more bigger moral call than many of us!!

Kwa kumalizia, JK na wengine wote ambao wenye nafasi za uongozi (hata kama ni kiongozi wa upinzani) ni wakukemewa na kukanywa!!! Wameshasikia sana ushauri na hawajali!!
 
nndondo

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
1,251
2,000
Nami pia nikupe big up MA, hakuna unafiki hakuna fasihi wala falsafa inayowakilishwa na huu upuuzi wa jenerali ulimwengu, wengi tunashangaa kinachomsumbua na hasa kilichomsababishia anguko hili maana ni kama vile RAIA MWEMA inaamua kutupa mtoto na maji ya kuogea, huwezi kuamini huyu ndie mwenyekiti wake. Naweza kukubaliana na wale wanaosema ana lake jambo.
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
11,857
2,000
Hayo ni maoni yake,na Jenerali pia alitoa yake na mkumbuke hiyo barua imetoka kwenye gazeti la wiki iliyopita si mpya bali ni ukumbusho wa kile alichoandika wakata huo Jk anaingia madarakani.Hivyo Ulimwengu anao uhuru wa kuamua ni namna gani atoe ujumbe kwani yeye anaelewa mlengwa ndio ujumbe utamfikia vizuri.Pia jamaa walishamvua uraia ni katika maswala ya kutetea haki za wananchi,Ombi langu kwa MsandoAlberto iweke sawa hiyo makala yako halafu ichapishwe kwenye magazeti husika.

sidhani kama kilichomvua uraia jenerali ni kutetea maslahi ya wananchi. Nimjuavyo jenerali(kutokana na makala zake) ni mnafiki aliyekubuhu. Kama ana taalum ya uandishi basi he remains an irresiponsible journalist: reason: majuma machache kabla ya uchaguzi jenerali alimkemea nd kalönzo musyoka pale aliposema kuwa wa tz tumchague kikwete kwani tz na east africa bado tuna mhitaji. Ulimwengu alitumia maneno mengi ya kejeri juu ya kauli hiyo( tazama post kwenye international forum inayomtaka vp wa kenya) nashangaa kwanini hapa ana toa kauli tofauti.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom