Tafakuri Yangu Ya Leo; Jenerali Ulimwengu Bakora Ya Watawala Acha Iwaadabishe Tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakuri Yangu Ya Leo; Jenerali Ulimwengu Bakora Ya Watawala Acha Iwaadabishe Tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMBOTA, Mar 30, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ……W’re polite and progressive by day, more tibalist than even the Kenyans by night…..

  Ukweli kama huu anaoweza kuusema Jenerali Ulimwengu ndio umewafanya watawala wengi kumwogopa mwanaharakati huyu kushinda hata UKIMWI, nani nchi hii asiyemfahamu Jenerali Ulimwengu? Licha ya mwandishi huyu kukumbwa na misukosuko hata ya kutaka kunyang’anywa uraia aah wapi Bwana! Jenerali Ulimwengu hana mpinzani kwa jinsi anavyosimamia ukweli.
  Pengine kwa waandishi wachanga wenye lengo la kufika alipofika Jenerali waanze mapema kukataa rushwa ambazo huwafanya kutumia kalamu zao kusifia uharamia kuliko kukosoa utawala mbovu, Alleluya Mungu Mwenyezi kwa kutupatia Jenerali Ulimwengu mwenye uwezo wa kuwasemea masikini wan chi hii, mwenye uwezo wa kukemea udini na ukabila , mwenye uwezo wa kumhoji hata rais bila uwoga nani kama Jenerali?
  Naam Jenerali Ulimwengu ni bakora ya watawala acha iwachape tu!

  Nani kama jenerali, Ulimwengu tumwone
  Nani anayetujali, yu wapi tusemezane
  Nani tumpe kibali, ukweli akawachane
  Jenerali Ulimwengu, kiboko ya watawala.

  Wamesuka njama nyingi, zote zimegonga mwamba
  Jenerali ndio kingi, wanyonge tunampamba
  Wanaoweka vigingi, hao wote ni mafamba
  Jenerali Ulimwengu, bakora ya watawala


  Nani asiyefahamu, Jenerali ni shujaa
  Yu wapi tumuhukumu, kwa kuzidi kuzubaa
  Jenerali ni muhimu, Arusha hata kondoa
  Jenerali Ulimwengu, sindano ya mabwenyenye


  Wakiwa maofisini, watawala wanalia
  Wakisoma gazetini , hofu inawaingia
  Kwa Jenerali makini, Mwema Raia sikia
  Jenerali Ulimwengu, msome Raia Mwema


  Beti tano nakomea, mengi nimeongelea
  Ulimwengu endelea, uovu kuufunua
  Ukweli tunaujua, wewe unatutetea
  Jenerali Ulimwengu, mtetezi wa wanyonge.  Nova Kambota Mwanaharakati,
  0717-709618 au 0766-730256
  novakambota@gmail.com
  www.novatzdream.blog.com
  Tanzania, East Africa
  Jumatano 29 March 2011.


  ulimwengubc.jpg
   
 2. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,464
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Ni poem lakin msg imefika. Heko ulimwengu!
   
 3. J

  Joblube JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nanachompendea JU si mkabila wala si mdini na si mpenda rushwa hongera JU
   
 4. R

  Rangi 2 Senior Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jenerali Ulimwengu ni kichwa kile.
  Namheshimu sana yule bwana.
   
 5. R

  Rangi 2 Senior Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  I liked this poetic flavor in here...
   
Loading...