Tafakuri: Police wanahusika utekaji na mauji ya RAIA wema?

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
"kibaya zaidi nimefikishwa kituoni centro RPC ananiambia una bahati tumekukamata asubuhi watu wanaonalakini ungekamatwa usiku MTU yoyote asione tungekupoteza" Anasimulia:Mdude Nyagari a.k.a. Sumu ya nyigu mnamo 18/4/2017.

Massa machache baada ya kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili kada kindakindaki wa chadema ndugu Mdude Nyagali,alisema maneno mazito ambayo kwa namna ya kipekee sana inabidi tuyaangalie kwa jicho la Tatu. Katika kile alichokiita kuteswa na pengine kunusurika kuuwawa na polisi,hebu tujiulize Polisi wanahusika utekaji na mauaji ya RAIA wema hapa nchini kutokana na maneno ya RPC Iringa?.
Kwa maneno hayo ya RPC,je, RAIA wema wataonesha ushirikiano kwa askari polisi?.
Karibuni tujadili pamoja.
Hii ni nchi yetu sote. Amani tuliyonayp tuilinde kwa nguvu zetu zote bila kujali itikadi ya vyama vyetu.
ONYO: Bandiko hili lisihusishwe na mauaji ya Askari wetu 8 Pale Mukuranga. JF where we Dare To speak Openly.
 
Video:polisi vs RAIA wema
 
Attachments

  • Askari.mp4
    3.8 MB · Views: 13
"kibaya zaidi nimefikishwa kituoni centro RPC ananiambia una bahati tumekukamata asubuhi watu wanaonalakini ungekamatwa usiku MTU yoyote asione tungekupoteza" Anasimulia:Mdude Nyagari a.k.a. Sumu ya nyigu mnamo 18/4/2017.

Massa machache baada ya kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili kada kindakindaki wa chadema ndugu Mdude Nyagali,alisema maneno mazito ambayo kwa namna ya kipekee sana inabidi tuyaangalie kwa jicho la Tatu. Katika kile alichokiita kuteswa na pengine kunusurika kuuwawa na polisi,hebu tujiulize Polisi wanahusika utekaji na mauaji ya RAIA wema hapa nchini kutokana na maneno ya RPC Iringa?.
Kwa maneno hayo ya RPC,je, RAIA wema wataonesha ushirikiano kwa askari polisi?.
Karibuni tujadili pamoja.
Hii ni nchi yetu sote. Amani tuliyonayp tuilinde kwa nguvu zetu zote bila kujali itikadi ya vyama vyetu.

Ndiyoooooooo!. Wanahusika. Sasa nidhahiri. Huwezi kumkamata mtu unamhoji ati kwa nini anaikosoa serikali mtandaoni, unamtesa na kumwapia ashukuru umemkamata watu wakiona. La sivyo ungemmaliza. Hivi tuna jeshi la polisi au tuna genge la wauaji?

Kwa mantiki hii, kwa nini tusiamini kwamba watu wanaopotea ki imla wanatekwa na hili genge pasipo watu kuona wala kujua na kuwamaliza?

Hii ni nini maskin kwa taifa langu Tanzania?

Kwa nini wakuu wasitangaze tu kwamba ni n chi yenye utawala wa ki imla kama ilivyo North Korea watu wajue kwamba ni watumwa na mateka katika nchi waliyodhani ni yao? WAtu wakiambiwa, bila shaka kila kaya, na kila jamii zitahamasisha wajumbe wake kukaa kimya, kuwa watii na kutokuhesabu wana haki yoyote ya kusema neno katika nchi yao. Wafatundishwa kuwa watill wakishukuru Mungu kila wanapopata nafasi ya kuliona jua likichomoza. Watashukuru Mungu kama kunakuwa na fedha za kujikimu wanabaki nazo baada ya kukatwa kodi. Watashukuru Mungu kama kutakuwa na hospital au kama wakiweze kupata tiba wanapoumwa.

Hawataisumbua tena serikali maana watakuwa wanasubiri kifo. Bila shaka wataongeza mshikamano katika kaya kwa kuwa hawatakuwa wanajua nani atapotezwa muda gani. Muda wote utakuwa ni wa utayari wa kuuawa.

Ninaomba tu kama ndivyo, basi tangazo lipite, lili watu wasiendelee ku risk maisha kwa kudhani wanauwezo wa kutoa mchango wa mawazo wakati hawana huo uhuru wala haki hiyo. Itakuwa ni kuokoa wananchi wengi kutoka katika mauti za ki imla.
 
Back
Top Bottom