Tafakuri baada ya mgomo wa Madaktari!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakuri baada ya mgomo wa Madaktari!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KakaKiiza, Mar 17, 2012.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Juzi tulishuhudia mgomo wa madakitari ulivyotikisa nchi na ndugu zetu wakafa kwa sababu ya mgomo!!mgomo uliochukua jumla wiki mbili za kwanza na wiki moja ya mwisho!

  Nikweli kama auna huruma moyoni au kuuguza hutaona migomo ya madakitari nikama wimbo unaoimbwa kwa lugha usiyoijua!
  Ukweli tunajua Madakitari nchi nzima wanafanya kazi kwenye mazingira yaliyo magumu nasiyoyakuridhisha kabisa na siyo madakitari pekee hata Askari Polisi,Walimu,afisa ugani wote hawa wanafanya kazi kwenye mazingira yaliyo magumu sana,lakini aimaanishi wagome kwakuwa wapo kwenye mazingira magumu!
  Kiujumla watumishi wa serikali wote wanafanyakazi kwenye mazingira magumu sana!!
  Kwa mantiki hii mgomo wa madakitari ulikuwa haki lakini ulikuwa na mapungufu kwa kuzingatia jinsi walivyo uapproach kwakutozingatia maisha ya watanzania wenzao na vile kutozingatia kitaaluma yao pia,Mfano Nikama mwanajeshi akipewa adhabu lakini anaona siyo stahiki hata kama anahaki inambidi atumikie adhabu alalamike baadae!!!

  Je kwa kufikiria kwa karibu je ni watoto wangapi walikufa kutokana na mgomo huo??
  Je akina mama wangapi walifia mawodini na watoto wao tumboni??
  Je wazee wasiojiweza ni wangapi wamekufa??
  Je ni wangapi walitakiwa kufanyiwa Operation hawakufanyiwa na wakafa??
  Je niwangapi wamepata ulemavu wa maisha kwakukosa huduma ya haraka??
  Yote hayo natafakari naona kweli kulikosekana busara na serikali wakaona nivyema wampeleke waziri mkuu ndo aokoe jahazi lakini wakasahau huu msemo chini!
  Ni upofu kudhani wazee ndiyo wenye busara zaidi!!
  Ninachokiona nia ilikuwa nikuongea na Rais lakini wakati mumeua ndugu zenu,wengine wamekuwa vilema wamaisha!! ni halali nyie kuitwa wauaji!!!!!
  Lawama amuwezi kuzikwepa kuna baadhi ya Maprofesa wanasema hata wao waliona walifanya makosa lakini kitukikiamliwa na jumuia nawao hawakuwa na lakufanya!!
  Kwa maana hiyo huo mgomo ulikuwa wakihuni.
  Siku nyingine madkitari fikirieni njia mbadala kuidai serikali!
   
 2. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,349
  Likes Received: 10,487
  Trophy Points: 280
  jana nimeshuhudia mama mjamzito akiandikiwa rufaa kwenda muhimbili kwa sababu vifaa vya kufanyia operesheni havijasafishwa(NOT STERILISED) kisa cha vyombo hivi kushindwa kusafishwa ni kukosekana kwa umeme,ule wa grid ya taifa na ule genereta ambalo limeharibika yapata mwezi mzima sasa na mzabuni wa kutengeneza ni wa wizara ya afya.
  Pia niliangalia karatasi iloyotumika kuandikia rufaa ilikuwa ni kama ya kufungia maandazi(UHaba wa stationeries)

  ili kupunguza gharama za mafuta ambulensi ile ilibidi kusubiri wagonjwa wengine kama watatu hivi wapelekwe kwa pamoja.

  Ninachokiona kwa madaktari sio kwamba wanalalamikia maslahi yao tu bali mauzauza kwenye sekta ya afya kwa ujumla.

  Vitu ambavyo vinalalamikiwa vipo ndani ya uwezo wetu hivyo serikali ilikumbushwa kuikumbuka sekta hii.kwani tumetumia sh ngapi kwenye sherehe za miaka hamsini ya uhuru?fedha hizi zilitoka wapi?

  Kama tunaipenda nchi yetu kwa dhati ni wakati wa kujiuliza ni asilimia ngapi ya pato la taifa(ondoa misaada) inatumika kwenye afya na jee inaendana na makibaliano ya kimataifa?

  Tusiwe wanafiki,huwezi kumfananisha daktari na mlinzi,afisa ugani au hata mwalimu.kosa la daktari halirekebishiki,sasa tukimuacha aende kufanya kazi huku ana hasira tutarajie mauaji ya halaiki.

  Madaktari nimewapenda sana wanasiasa,waandishi,wanataaluma na watanzania kwa ujumla wamewasikia na kuwaelewa barabara.kuanzia mwezi wa kumi na mbili mwaka jana mpaka leo hakuna siku tuliokosa kusikia mgomo wa madaktari.

  Babu yenu siungani na wazee mabwanyenye wa dar es salaam kwa sababu najua iko siku nitakuja na tatizo la tezi dume(BPH) mniandikie rufaa ya india kwani najua vifaa vitakuwa hakuna.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 3. rwamashugi

  rwamashugi Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni hoja ya kinafiki sana. Fikiria Madaktari walianza kilio chao tangia 2005 lakini wakanyamazishwa.Hakuna hata raia mmoja aliye sikika kuwaunga mkono. Wengi wamekimbia nchi kwenda nchi za jirani ,na sisi tumenyamaza.
  Madaktari tumewafanya Vitendea kazi,Vibarua,kazi ya wito wa kufa maskini,watoto wao kuvaa viraka.
  Wito:Wananchi tunatakiwa kuwaunga mkono Ma Dr ili wapate haki zao.
  Mbona wakienda Botwana,Zimbabwe,Zambia, wanalipwa?.
  Je hizo nchi zina uchumi mzuri kuliko sisi?

  Mwisho:Kilio kipelekeni kwa Serekali ili imalize chanzo cha tatizo.Ila tukisubiri kulalamikia matokeo
  Mgomo uko pale pale na wahanga ni sisi.Wakubwa si wanaenda INDIA ,UJERUMANI ...???

  MAWAZO MGANDO KAMA YA KWAKO NDIYO YANASABABISHA VIFO VYA WATU.
   
 4. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na matamshi yako kabisa hasa kwenye red!Ila hoja ya msingi ni jinsi gani madakitari walivyo handle mgomo!!kama wewe ni dakitari basi wewe ukufahuru maana hata miiko ya udakitari huna!!kwani wale madakitari ni mbuzi hata mbuzi zina viongozi wake kwa maana hiyo jumuia za madakitari ndo zingeishinikiza serikali nakwenda kwenye meza ya mazungumuzo na siyo kugoma!!
   
 5. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,349
  Likes Received: 10,487
  Trophy Points: 280
  mbona unaonekana kama vile hukuwepo nchini na hukufuatilia sakata la mgomo wa madaktari?
  Kwa taarifa yako wamarekani wamesema wanapata deni kubwa kwa kuendelea kusaidia nchi kama zetu.mwaka huu mwisho wa misaada ya global fund sasa hapa ndio tutajua serikali haijawekeza kwenye afya.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Iache Serikali kama ilivyo. Madaktari waliokwenda Ikulu kujadiliana sidhani kama wana hamu ya kurudi tena huko.

  Nna uhakika kabisa, mtasikia au itakuwa kimya kimya hata uongozi wa chama chao hawana hamu nao tena. Eehh jamani msifikiri Serikali unaweza kuipangia na kuipa masharti utakavyo wewe, kuna mipaka na hiyo mipaka lazima iheshimiwe. Huwezi kabisa kumpa ultimatum Rais ya kuwa amwachishe kazi waziri na naibu waziri wakati hujamuonesha kabisa kosa lao.
   
 7. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,349
  Likes Received: 10,487
  Trophy Points: 280
  wazee tumemshauri awafute kazi hao mawaziri na mawaziri wengine wasiojituma.subiri kidogo inshallah mwaka hautaisha

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 8. M

  Mukalabamu Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ushawahi kutibiwa na dk kama jibu Ni ndio ina maana ulitibiwa na mbuzi?wewe ninavyokusoma hata mamako mzazi unaweza kumpa hili jina ili mradi ufurahishe mabwana zako
   
 9. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Nikweli mkuu ulichosema!!nakuunga mkono!
   
 10. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Rais ana wshauri wake kwa maswala ya siasa,uchumi,hata katika wizara anaye waziri wa nchi sera na mipango,mawaziri ofisi ya rais,waziri mkuu wote hao nikumsaidia rais katika utendaji wake wakila siku!Mgomo wakuacha watanzania wanakufa na kusema unashinikiza serikali iwatendee matakwa yenu na itekelezi mara moja nikutokuwa na moyo wa uzarendo kuna sekta ambazo kwa vyovyote vili hazitakiwi kugoma mfano Polisi wafunge yale malango na maabusu waachiwe je nchi hii itakalika???wewe unawazidi polisi katika kufanya kazi kwenye mazingira mabovu??kutolipwa mishahara kwa wakati??kutopewa malimbikizo yao kuhamishwa bila kulipa je wakigoma??
  Ndiyo maana milango yapolisi haijawai kufungwa tangu ilipofunguliwa!!
   
 11. M

  Mukalabamu Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Watanzania tunaponzwa na unafiki,ethics zinaendana na haki na zinamhusu kila mtu katika nafasi aliyonayo,siasa,dini na uganga wa kienyeji vyote vina miiko yake,ur wewe mahali ulipo unafuata miiko ya kazi yako? Kama ndiyo,basi ubarikiwe kama sio basi stop pointing your fecal stained fungerà on others,anza na nafsi yako,wanasiasa unaoeapigania ni nani anafuata ethics za uongozi?tafakari
   
 12. M

  Mukalabamu Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Sasa unataka madaktari wadai haki za polisi?kama hawalalamiki uenda wameridhika na kazi zao,aliyevaa viatico ndiye anayejua vinambana lussi gani,cha msingi Ni kuboresha mazingira ya kazi katika secta ya ina,sasa hv jamii inaamini na kuwa huwezi kufanya kazi serikalini ukala na watoto wakaenda shule,kwa hiyo wewe unaona polisi wale rushwa na kushirikiana na majambazi na madaktari waendekeze rushwa kwa wagonjwa lakini serikali yako ya kishenzi isiguswe?watu wenyewe mawazo kama ya kwako hatuwahitaji tena Tanzania hii
   
 13. rwamashugi

  rwamashugi Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 14. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,349
  Likes Received: 10,487
  Trophy Points: 280
  hao mawaziri wangekua wanamshauri vyema mgomo ungetokea?mbona unajitoa akili.
  Milango ya muhimbili iliwahi kufungwa toka muhimbili ianzishwe?madaktari ni vidume bwana mkubali mkatae

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 15. M

  Mukalabamu Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  inaonekana we Ni mmoja wa wanaokula hela zao wanazopewa,siku wakiingia barabarani na siraha kudai haki zao ndo mtajuagharama za kutetea serkali dhalimu isyojali watumishi wake na wananchi,Mara ngapi umesikia polisi na wanajeshi wamehusishwa na ujambazi?Mara ngapi askari wanawakodisha majambazi siraha? wewe unaona Sawa tu
   
 16. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Yaani unafananisha polisi na daktari? Khaaa! Polisi wana miiko yao kwa sababu zao na doctors wana miiko yao pia tofauti, hata accountant anamiiko yake, in general Graduate yeyote anaapa pale anapotunukiwa shahada yake. Hebu tafuta mfano mwingine kama upo wa kumfananisha doctor. Mie nawaheshimu hawa watu, nilipata stroke for eight months na fracture in the skull wamenitibu sana kwa upendo, tena ndugu zangu wasipokuwepo jamaa walikuwa wananisaidia hata kunipeleka toilet. Acheni tu polisi ni kweli ana kazi ngumu ila amekuwa trained kuzifanya hizo kazi, na sio wote kuna vitengo mbalimbali. Fahamu kuwa kila mtu ana kazi yake, though siwezi kusapoti migomo ila ni vizuri pia mkikwaruzana mkajua kumalizana mapema kabla ya maafa.
   
 17. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,349
  Likes Received: 10,487
  Trophy Points: 280
  hivi sakata la vipimo vya ukimwi limeishia wapi?sasa hivi ukitaka kupimwa ukimwi unaambiwa vifaa hakuna.halafu nahisi hata mheshimiwa rais alipima kwa kutumia vipimo feki....halafu anasema hajui kosa la mawaziri.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
Loading...