Tafakuri 10 mtekwaji wa mwaka Mdude

Tafakuri 10 mtekwaji wa mwaka Mdude

blix22

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
213
Reaction score
645
*TAFAKURI 10 MTEKWAJI WA MWAKA MDUDE*

*1. Akamatwa na Vyombo Vi3 vya Dola:*

Kadhia ya utekaji, kujiteka na/au kutekwa Mdude inaanzia hapa. Ukisoma tweets za mwanzo za wafuasi wa Chadema utacheka.

Kwamba Mdede kakamatwa mara na wanajeshi waliotumwa, mara polisi mara sijui watu waliovaa kininja. Mtu mmoja anakamatwa na watu watatu tofauti[emoji41];

*2. Watekaji watoa taarifa mitandaoni:* Ukifuatilia tweet za viongozi wa Chadema kama Halima Mdee na Lema utajua kuwa walikuwa wanawasiliana na watekaji.

Kuna mda wanapost eti Mdude anapelekwa Dar, mara sijui yuko kwenye buti mara sijui sasa hivi kachoka anashindwa kula. So walikuwa wanajua alipo na kila anachokifanya[emoji849]:

*3.Atekwa na Suti:* Huyo Mdude kavaa Suti siku alipookotwa...so alitekwa na suti, akateswa akiwa na suti, akatelekezwa akiwa na suti na kuokotwa akiwa bado kwenye suti yake hivyo hivyo[emoji2][emoji2]Basi hao watekaji ni wakarimu sana. Hongera yake.

*4.Alikuwa Dar au Mbeya:* Narudi tena kwenye tweet, viongozi wote wakuu wa Chadema walikuwa wanawaaminisha watu Mdude yuko Dar, lakini ghafla kaokotwa Mbeya🤦‍♂. Kwa nini walikuwa wanawapoteza watu maboya?Walikuwa wanamlinda nani?Mtekaji?

*5. Mtekwaji aporomosha maneno lukuki mpaka aambiwa tulia tulia*[emoji2][emoji2]Kuna video moja ya mtekwaji akiwa hospitali anatibiwa...yaani nesi anamfutafuta yeye anaporomosha maneno tu lukuki kueleza baadhi ya matukio akiwa na watekaji, mtekwaji mwenye hamu ya kuropoka, mtekwaji anayerekodiwa akiwa hospitali akitamani kuhadithia nyakati ngumu alizopitia.Huyu ni mtekwaji mgumu sana anayemiss moments akiwa na watekaji.

*6. Balozi ataka uchunguzi*

Huyu ni mekwaji maarufu sana. Nimeona Balozi wa Uingereza hapa nchini ambaye hajasema lolote kutopatikana binti wa nchini kwake Madeleine McCain aliyetekwa tangu 2007 hadi leo hajapatikana lakini anaacha huko anaingilia hili la Mdude akidai anataka uchunguzi. Hapa ndipo unarudi kwenge kisa cha "Pembe Tatu ya Bermuda." Balozi ana maslahi gani na Mdude. Is she part of it?

*7. Ya Lissu Yarejea, Naye Akataa kuhojiwa:*

Staili hii ni mpya lakini inazidi kuota mizizi. Wahanga wote wa matukio yanayoitwa "mabaya" hawataki "wabaya" wao wajulikane.

Kama ambavyo mpaka Leo Lissu anayesafiri kwenda Ulaya na Marekani kula bata hataki kuhojiwa wala dereva wake, leo nasikia huko Mbeya mtekwaji wetu mwenye suti naye na wapambe wake wamegoma kuhojiwa kuhusu utekwaji wake[emoji15][emoji15][emoji15]Tafakari. Mwalimu huenda ni yule yule;

*8. Kujipanga muhimu;*

Cha kujifunza katika masuala ya utekwaji wa kujiteka ni kujipanga.Katika hili mlivamia mno kuropoka katika social media kiasi cha "kiki" mliyotaka ikae saaana ikawatisha hata vijana mliotaka wakae na mtekaji muda zaidi ili kiki ziendelee, wakapanic na kumuachia mapema sasa naona ninyi ndio mmepanic sasa na mnaonekana, kama nilivyoeleza katika na. 9 na 10, hili la Mdude kutoka mapema hamkuwa mmejiandaa nalo.

*9. Chama chashindwa kutoa tamko la maana:*

Kitu kingine angalia, ukiacha kataarifa kafupi ka mtandaoni, sijaona Chadema wakitoa tamko la kina.Je, Chama hakijafurahi nini mtekwaji kurudi mapema? You see it!

*10. Kwa nini Mbowe kakimbilia ya Makonda na sio ya Mdude:* Akiwa Kanisani kumsindikiza Mzee Mengi kwa nini Mbowe kaongelea suala la Makonda na wachaga na hakugusia kabisa la kijana wake Mdude? Hapa ndipo ninapoikumbuka makala moja iliyowaonya vijana wa Chadema wanaopewa "assignment" ya kutukana ili watoke kumbe wanaishia kutekwa.

Alamsiki.
 
Ulicho andika uchuzi mtupu,yaani huelewiki unazungumzia kitu gani umeandika Mdude kabla sijamaliza kusoma kwa umakini umekimbilia kwa Mh. Lissu sijakaa Sawa kukusoma umechepuka kwa Mbowe na Makonda.Uko mirembe wodi namba ngapi nikuletee matunda.
 
elfu saba isikufanye upoteze thamani ya utu wako na isikufanye ujitoe ufahamu kijana,hata andika yako inaonesha ni mtu aliyekulupushwa kuandika!Najua vijana kadhaa watapewa jukumu la kufanya damage control katika hili na wengine watafanya matukio(Skendo) kadhaa ili kuleta distractions among citizens ila wakubwa zako wakumbuke jinai inadumu na haki haipotei ila hucheleweshwa tu.

Naionea huruma nchi yangu, nakisikitikia Chama changu ninachokipenda tokea ujana wangu.
 
*6 Wewe una maslahi gani na watekaji mpaka unataka uchunguzi usifanyike?
 
Unakunywa mataputapu unakuja kuandika mashudu humu sasa ulitaka wamvue nguo kwan Mo dewji walimbadilushia nguo? Jinga kabsa ww
 
Kwa hiyo ulitaka kusemaje labda? Au tukusaidie nini?
 
Sasa we mwenyewe umejichanganya, sasa una tofauti gani na hao.
 
Mtoa mada ameleta mada nzuri sana kuwa kutekwa na kurudishwa kwa Mdude CHADEMA kuna mkanganyiko mkubwa sana ,Maana umeonyesha wahusika waweza kuwa ni wale wa Lissu, kwa hiyo kinachotakiwa ni kuleta uchunguzi wa nje ile waweze kuweka kila kitu wasi kuhusu hawa watu ambao wanaitwa WASIOJULIKANA.kuletwa kwa uchunguzi wa nje ni ili majibu yake yasiwe kuegemea sehemu yeyote kati ya maadui wa kawaida na mambo ya kisiasa
 
Mlikuja na ngonjera hizo hizo sakata la expansion joint, hadi leo hii kijana ameshinda kesi na hakuna yeyote aliyechukuliwa hatua.

Kama tuna vyombo vya usalama haviwezi kuwapata na kuwabaini hao unaodai walimteka huyu jamaa bila kujali wanatoka chama gani au ni akina nani, tuna hali mbaya zaidi kuliko inavyoonekana.

Hauwezi kutetea huu unyama kwa viwango vyovyote vile.
 
Mama Akwelina alikua analia akitamka maneno haya "...haya mambo nilikua nayaonaga kwenye Tv tu, sikutarajia kama ipo siku yatabisha hodi nyumbani mwangu..." nakuhakikishia leo yule mama hana Imani na Chombo cha ulinzi tena, siku yakibisha hodi kwako hutakuja tena kuandika pumba hizi
 
IMG_20190509_183548.JPG
 
Ulicho andika uchuzi mtupu,yaani huelewiki unazungumzia kitu gani umeandika Mdude kabla sijamaliza kusoma kwa umakini umekimbilia kwa Mh. Lissu sijakaa Sawa kukusoma umechepuka kwa Mbowe na Makonda.Uko mirembe wodi namba ngapi nikuletee matunda.

We kila kitu umekielewa ila kutokana na itikadi yako kuwa uko upande huo unajifanya hujaelewa
 
Back
Top Bottom