Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,231
- 44,437
Mkuu unaweza kushawishi kwa kujiamini pale tu kitu unachosimamia ni dhamira safi.Wananchi wana madai ya msingi na serikali inajua ni ya msingi lakini yaliyo nje ya mpango wao wenye maslahi tusiyoyajua.
Huwezi kushawishi u.puuzi zaidi ya kutumia nguvu hasa ukijua hula ya unao waongoza ni Watanzania! Hawa si wakuwaimbia nyimbo za falsafa ni kusema kwa kauli moja inatosha inabidi wasikilize umma kwa nguvu.
By the way mkuu,serikali imeshindwa kutushawishi, sawa.lakini huoni na sisi tumeshindwa kuwashawishi vile vile?
Hapa tukubaliane pande zote tumefeli na kuhatarisha muelekeo wa Taifa! Basi walau tusake muafaka!!!
Sisi unaotuita wajinga wa kufikiri,
Nataka nikuhakikishie hatusomi thread tukaishia hapo, we take it kidogo to next level of thinking.
1. Kauli/Thread hii imeandikwa na nani?
2. Thread hii imeandikwa wakati gani?
3. Thread hii imeandikwa katika mazingira gani?
4. Thread hii inamlenga nani? (For this matter OK as you've Just said MTWARA,Uongozi wa Vyama, BAVICHA)
Baada ya hapo sisi 'wajinga' ndio Analysist.
ok alitimiza ahadi ,ila katika uongozi huoni wapo wasaliti ambao binafsi ama wametumwa kuhujumu uongozi/taasisi fulani?Kwa maandiko unapaswa ''ulikate" lakini wangapi unawaona wanatembea na jicho moja! na una uhakika gani lililobakia halitakosea?
Ok! ikitokea likikosea nitachukua hatua nyingine,ila kama halita nikosesha na bwana wangu it is ok.
Well maandiko sehemu fulani Yesu alisema "yaacheni magugu na ngano yakue pamoja!" Ila hakusema wakati wa mavuno tuchanganye pamoja ngano na magugu,kila kimoja kitakaa sehemu yake
Hufai katika chain ya uongozi out ,hapa hahitaki kushawishi kama ulisha mkuza katika maadili ya uongozi na kuonywa,utaachwa na kuwa wa mataifa kama sii kufunzwa na ulimwengu
Wengine watakuambia alitimiza kilichoandikwa.
Mm siamini mia kwa mia hoja wa Mzee Mwanakijiji . uongozi ni pamoja na udiktete ktk uongozi na utendaji bora.Mi nashangaa kwa nini mnaangaika kuchangia hoja nyepesi kiasi hichi, na sikutegemea ianzishwe na mtu kama MMK,
Uongozi ni composition ya hayo yote aliyosema + kufukuza. Ingawa kufukuza ni hatua ya mwisho na inachukuliwa pale inapoonekana kubaki kwa hawa watu kuna madhara zaidi ndani ya taasisi kuliko kuondoka.
MMK umeweka mpaka wa uongozi sehemu ambayo siyo. Jaribu kusoma taasisi mbali mbali zenye nidham uone inajengwaje. Anza na jeshi ( sio lazima iwe Tz)
Uongozi ni kusimamia sheria na taratibu zilizopo. Uongozi ni mambo mengi.
Kazi pia ya kiongozi ni kumpeleka punda kunywa maji. Swala la kunywa ni juu ya punda.
Jifunze kwa Wilson Mandela na mke wake wa kwanza Winnie ujue athari za usaliti.
Shukran kwa busara naona siku hizi unatoa mawazo ya ki-utu uzima.au mambo yaelemea kwa uwapendaoUongozi ni ushawishi. Uongozi siyo kutegeana, kutegeshana, kunyemeleana na kufukuzana. Na uongozi siyo vitisho au mikwara. Kiongozi anayeishi kwa vitisho ni kiongozi aliyeshindwa hoja. Hili ni kweli kwa vyama vile vile; chama kinachoishi kwa vitisho kimeshindwa hoja. Tafakari
Kuna watu wana matatizo; watu wanapenda kufikiria vitu kwa upenyo mdogo sana na hii ni hatari. Kuna matukio mengi ambayo yametokea nchini na yote nimeyafikiria katika kauli hiyo hapo juu. Tumeona mwitiko wa serikali dhidi ya wananchi wa Mtwara walioandamana kuhusu suala la gesi. Mwitikio wa serikali umekuwa ni kejeli, mikwara na vitisho siyo ushawishi. Hili tumeliona huko nyumba ambapo serikali pia imetumia nguvu dhidi ya wananchi kwa sababu imeshindwa kuwashawishi.
Haya ya CDM nayo yanaweza kuwemo humo humo kwani nayo yanaonesha tatizo lile lile la kushindwa kushawishiana. Watu wanapotengeneza mitandao ambayo badala ya kufanya sapoti ya mtu yanaanza kumtega mtu, kujaribu kumwangusha au kumchafua ni kwa sababu watu hao wameshindwa hoja (na hapa nazungumzia pande zote zinazogongana - hakuna aliye salama).
Sasa mtu anaweza kujaribu kwa kutumia hoja lakini mtu asiyeweza hivi hutumia kushawishi kwa kutumia nguvu (ziwe za physical, law, procedures au hata jina lake).
Tusifikiri kidogo let think wider than personal politics.
Uongozi ni ushawishi. Uongozi siyo kutegeana, kutegeshana, kunyemeleana na kufukuzana. Na uongozi siyo vitisho au mikwara. Kiongozi anayeishi kwa vitisho ni kiongozi aliyeshindwa hoja. Hili ni kweli kwa vyama vile vile; chama kinachoishi kwa vitisho kimeshindwa hoja. Tafakari
sisi waislam tunaamin siku zote mtu ukitaka kufaulu maishani basi subiri kwa rah'mani,ikitimia miadi wa juu hurudi chini,kama kubeba boxi nje ya nchi kumeshinda utawezaje kujenga hoja??kichwa kazi yake ni kufikiri,wewe ukaamua kwa khiyari yako kukimbilia nje ya nchi kwenda kukiharibu kichwa chako kwa kubebea mabox,ona upeo wako ulivokosa maono ya mbali,- haya maneno yameandikwa na mtu ninayewaambieni all the times anafaa kugombea urais huko kwenu, huyu dr. Kitila na zitto, basi ndio wanafaa, wengine wote hawafai kiongozi ni yule anayeweza kukosoa bila kuogopa nyie mmezoea kuogopana na kutishana tishana tu, sasa hapa mmepewa kubwa yao ona mnavyohangaika hangaika, tulizeni boli tafakari hapa!!
Le mutuz
sisi waislam tunaamin siku zote mtu ukitaka kufaulu maishani basi subiri kwa rah'mani,ikitimia miadi wa juu hurudi chini,kama kubeba boxi nje ya nchi kumeshinda utawezaje kujenga hoja??kichwa kazi yake ni kufikiri,wewe ukaamua kwa khiyari yako kukimbilia nje ya nchi kwenda kukiharibu kichwa chako kwa kubebea mabox,ona upeo wako ulivokosa maono ya mbali,
huelweki unacheka au unalia,umeyagharim sana maisha yako,unatia huruma sana,,
unatembea hali ya kuwa ushakuwa maiti mda mrefu sana,pole sana ndugu yangu
Uongozi ni ushawishi. Uongozi siyo kutegeana, kutegeshana, kunyemeleana na kufukuzana. Na uongozi siyo vitisho au mikwara. Kiongozi anayeishi kwa vitisho ni kiongozi aliyeshindwa hoja. Hili ni kweli kwa vyama vile vile; chama kinachoishi kwa vitisho kimeshindwa hoja. Tafakari
Tafakari ya Mwanakijiji leo...
- Wachana na mimi huu ni mfupa umemshinda fisi wewe huuwezi, jadili hoja wachana na watu soma maneno ya mwanaume hapo juu kudadeki!!
le mutuz
Kwani nimeandika somo zima la uongozi? of course uongozi ni zaidi ya haya lakini kiini hasa cha uongozi ni ushawishi siyo sheria wala taratibu. Ni uwezo wa kushawishi watu kuona wasichokiona, kukubali ambalo walikuwa hawakikubali au hawataki kukikubali na kutenda yale ambayo vinginevyo wangekuwa wanasita kuyafanya. Huwezi kuwa na kiongozi ambaye anakimbilia 'taratibu na sheria' kwa vile kashindwa kushawishi.
Kitu kimoja ambacho Nyerere alikuwa mbali sana kuliko viongozi wetu wengi wa sasa ni kuwa aliweza kushawishi (kama alishawishi kwa mazuri au la hilo jingine). Kiongozi ni lazima ajifunze kushawishi. Na hili ni kweli zaidi kwenye utawala wa demokrasia.
......
Tafakari ya Mwanakijiji leo...
- Wachana na mimi huu ni mfupa umemshinda fisi wewe huuwezi, jadili hoja wachana na watu soma maneno ya mwanaume hapo juu kudadeki!!
le mutuz.......
Uongozi ni ushawishi. Uongozi siyo kutegeana, kutegeshana, kunyemeleana na kufukuzana. Na uongozi siyo vitisho au mikwara. Kiongozi anayeishi kwa vitisho ni kiongozi aliyeshindwa hoja. Hili ni kweli kwa vyama vile vile; chama kinachoishi kwa vitisho kimeshindwa hoja. Tafakari
Zitto Kabwe
Uongozi ni ushawishi. Uongozi siyo kutegeana, kutegeshana, kunyemeleana na kufukuzana. Na uongozi siyo vitisho au mikwara. Kiongozi anayeishi kwa vitisho ni kiongozi aliyeshindwa hoja. Hili ni kweli kwa vyama vile vile; chama kinachoishi kwa vitisho kimeshindwa hoja. Tafakari- MwanaKijiji
Source: Facebook
Like · · Share · 13 minutes ago via mobile ·