Samiaagain2025
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 2,926
- 3,054
Wanajamvi heshima kwenu,
Tangu mwanzo na hata sasa, serikali ya awamu ya tano inajipambanua kama "serikali ya wanyonge". Wananchi wengi sasa wanazidi kuuliza kuwa hawa ni wanyonge wa aina gani?:
Tutafakari.
Tangu mwanzo na hata sasa, serikali ya awamu ya tano inajipambanua kama "serikali ya wanyonge". Wananchi wengi sasa wanazidi kuuliza kuwa hawa ni wanyonge wa aina gani?:
- Wakulima ambao bei za mazao yao hazieleweki, mfano: bei ya pamba na korosho.
- Wanufaika wa HESLB wanaodaiwa mamilioni ya pesa huku wakiongezewa na "retention fee'?
- Wahitimu wa vyuo wasio na ajira na wamesota kwa takribani miaka 5?
- Watumishi wa umma wanaolia kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja?
- Wastaafu wanaodai mafao yao NSSF na PSSSF kwa tabu na usumbufu mkubwa?
- Kwani wananchi wanaosomesha watoto wao bure sekondari wanafaidika na nini kama vijana hao hawapati ajira kwa wingi?
- Wanaochapwa viboko na baadhi ya maofisa wa serikali?
- Walipakodi na TRA?
Tutafakari.