Tafakari: DHAMIRA KUU YA CHADEMA NA MUSTAKABALI WA TAIFA

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,071
Nadhani watanzania wengi bado wataendelea kutafakari juu ya misimamo na dhamira kuu ya chama hiki kikuu cha upinzani nchini!
Ni vigumu kufanya tafakari na kujua malengo!
Kuna vitu ambavyo labda wao wanaweza kuvielezea kwa ufasaha zaidi.
1. Muungano na vyama vingine vya upinzani
Katika miaka ya 2005, chama kikuu cha upinzani cuf kilikaribisha vyama vyote vyenye nguvu kuunda kambi rasmi ya upinzani, jambo ambalo liliwapa nguvu chadema na nccr nao kuwa na sauti ktk bunge lile kiasi kwamba zitto na slaa wakawa miongoni mwa wabunge waliokiwa na nguvu na kujijenga kisiasa!
Ktk bunge la 2010-2015 chadema waligoma kuungana na wapinzani wenzao, wakatawala bunge na kuzika vyama vingine! Sababu kuu ya kuukataa muungano ni kwa kuwa cuf imeungana na ccm kwa upande wa Zanzibar!
Lakini wakati wa bunge la katiba wakaamua kuungana na cuf na vyama vingine kujenga ukawa ilihali, ule muungano wa ccm na cuf kwa Zanzibar bado upo pale pale!
Tafakari: Nini motive ya chadema katika muungano wa ukawa ambapo kwa sasa wao wanapewa lion share ktk majimbo? Kwanini ni pale wao wakinufaika tu ndio wanakubali kubend and not otherwise? Kwa cdm ni wao kwanza au Tanzania kwanza?
2. Kila wakati panapotokea malumbano ya kiuongozi ndani ya chama, hasa mwenyekiti Mbowe anapokuwa matatani baraza la wazee huingilia kati na kutoa suluhu ya kumlinda mwenyekiti! Hiyo ilitokea wakati wa chacha Wang we, kaborou na zitto kabwe! Wakati wote mwenyekiti alishinda na watu waliaminishwa hiki chama sio cha mtu mmoja! Lakini kimantiki mwenyekiti anaonekana kusaidiwa sana na wazee ambapo Mara zote fikra za m/kiti huwa zinadumishwa, kama pale alipomtaka slaa aache ubunge na kumpisha nafasi yake ya uraisi ili chama kitoe mgombea wa ngazi hiyo na alikuwa tayari kumlipa slaa stahili zake za ubunge! Juzi amemtema slaa na kumpitisha Lowasa na kuwalazimisha viongozi wenzie wote wakubaliane na matakwa yake hata pale wenzie walipokuwa wanatishia kukikacha chama hakujali! Safari hii wazee walikuwa pamoja na mwenyekiti!
Tafakari: kuna kuburuzana ndani ya chama, ambao chama kinaenda kiukoo zaidi kuliko kutazama maslahi mapana na malengo ya chama?
3. Uteuzi wa wagombea uraisi na baadhi ya wabunge toka ccm ambao kwa kauli ya chadema hawatopokea makapi toka ccm na hawatopewa nafasi! Tumeona baada ya kuja Lowasa, slaa ametupwa, wagombea waliopitishwa ktk baadhi ya majimbo wametemwa kuruhusu makapi yachukue nafasi! Ni kweli ccm peke yao ndio wanaofanya udhalimu au hata chadema pia?
Tafakari: uadilifu kwa chadema sio pamoja na kusimamia misimamo ya chama na kuhakikisha matakwa ya wananchi pia yanaheshimiwa?
4. Kashfa ya kununiliwa mwenyekiti kwa bilioni kadhaa na kujipanga kumsafisha Lowasa kunafanya kuona ile dhamira ya kusimamia utendaji haki ipotee! Hata hivyo kufanana na kwa team mbili za ushindi za M4C na 4U movement kunaleta shida ktk kujua mipango rasmi ya team hizi mbili kabla hazijaungana? Je ni team zilizokuwa zinatafuta uraisi ktk upande wowote kwa dhamira ipi wkt before itikadi ya kambi hizi 2 ilikuwa tofauti?
Tafakari: Je chadema wana agenda nyingine yeyote katika harakati hizi za ukombozi?
4: Kushindwa kuwa na mgombea uraisi ndani ya chadema na team ukawa kwa ujumla kunatoa picha mbaya sana kwa umoja huu! Kuna !maswali mengi wanayotakiwa kuyapatia majibu, je kama Lowasa asingekuja ukawa ni kweli wasingeweza kabisa kumpata mtu ambaye angefaa kuwa raisi?
Tafakari: Je chadema na ukawa wanataka kutuaminisha kuwa miezi yote hii iliyopita waliyokuwa wanajinadi kuwakomboa watanzania hawakuwa na mikakati kiasi cha kumsubiria mtu akatwe na ccm ndio afit ktk mipango yao! Na je, Haya mengine wanayotaka kutuaminisha sio kiini macho kingine ?

Wadau yapo mengi ya tafakari mnaweza kuyaongeza!
Declaration of interest: Mimi naprefer ccm ishinde, (ingawa si mwanaxhama wa ccm) so mtizamo wangu unaweza kuwa na biase
 
Back
Top Bottom