KIBURUDISHO
JF-Expert Member
- Mar 28, 2011
- 1,002
- 274
Kama mnafika katika uwanja huu na kusoma ujumbe huu tafadhalini hebu shughulikieni hili tatizo linalotusumbua sisi tunaopokea matangazo yenu kwa njia ya satellite ya INTELSAT906E.Kwa kipindi kirefu hili tatizo limekuwa sugu mara wiki mbili signal quality zenu zinakuwa safi baada ya hapo zinasumbua au hazipatikani kabisa kama ilivyo sasa labda tu kwa wale wanaotumia yale madish yenye ukubwa wa ft8.Kwa hawa wa Star tv mlikuwa vizuri sana kwa hadi signal quality yenu ilikuwa juu sana sawa na channel ya Aljeezra.Sasa nashindwa kuelewa ninini kinachosumbua mara leo hivi mara kesho hivi naingiwa na wasiwasi kuwa labda hao wamiliki wa hivyo vingamuzi ndio mnaokula nao ili tukimbilie kwenye vingamuzi vyao kwa kuvuruga mfumo huu tunaoutumia!!!!!!!!.. Nawasilisha