"Ndugu zangu,
Hatari kubwa ninayoiona mbele yetu ni kwamba, uzalendo, utu na udugu miongoni mwetu Watanzania unaondoka kwa kasi ya ajabu, nyuma yake kumeachwa ubinafsi uliotamalaki na wenye kutanguliza zaidi maslahi- na si maslahi ya umma, ni ya binafsi.
Maana, unajiuliza; ni kwa nini mtu anayekufahamu vizuri anashindwa kukuelezea kwa uhalisia jinsi anavyokufahamu. Badala yake, kwa makusudi, na kwa nia ovu, anaupotosha ukweli?
Na bado atakuita ndugu!"- Tafadhali Usininukuu.
Maggid Mjengwa,
Iringa