Tafadhali Usininukuu; Hatari Kubwa Ninayoiona Mbele Yetu...

Tafadhali Usininukuu; Hatari Kubwa Ninayoiona Mbele Yetu...

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,251
"Ndugu zangu,

Hatari kubwa ninayoiona mbele yetu ni kwamba, uzalendo, utu na udugu miongoni mwetu Watanzania unaondoka kwa kasi ya ajabu, nyuma yake kumeachwa ubinafsi uliotamalaki na wenye kutanguliza zaidi maslahi- na si maslahi ya umma, ni ya binafsi.

Maana, unajiuliza; ni kwa nini mtu anayekufahamu vizuri anashindwa kukuelezea kwa uhalisia jinsi anavyokufahamu. Badala yake, kwa makusudi, na kwa nia ovu, anaupotosha ukweli?

Na bado atakuita ndugu!"- Tafadhali Usininukuu.

Maggid Mjengwa,
Iringa
 
Utaileza mahakama jinsi unavyomjua,au ni wasifa wa marehemu maana ndiyo huwa tunapewa historia
 
ni pale unapojifanya kuwa uko juu ya watu wengine, mtu wa busara na hekima kumbe hamnazo kabisa sawa tu watu wengine wanafiki, huoni lakini waungwana tunaona mbio hizo.
 
Hadithi yako inatufundisha nini?

Sisimu sio chama tena cha siasa, ni genge la wauni, wadhuluma, wauaji na wapenda madaraka milele kwa gharama zozote.... na yeye alikuwa kada sasa wamembadilikia.
 
Kaka, yote yanayotokea yalishatabiriwa siku nyingi lakini nikupe tu moyo mkuu kuwa mwaka 2015 utakuwa wa kihistoria hapa tanganyika.

Kwani tutawakamata wote walioharibu taifa letu na kuwafungulia mashtaka na wakipatikana na hatia tutawapiga risasi hadharani kama wafanyavyo china ili kurudisha uzalendo katika taifa hili.
 
Hivi Kwanini kuimarika kwa CHADEMA kumeibua yote haya! Na kula walalahoi wengi tu wameingia kwenye huu mkumbo wa chama tawala kuiangamiza CHADEMA ili waweze kutawala!
 
Mjengwa ni mwovu tunajua vijana wa aina yaunakosali munastrategy yenu tumekujua sana hatutakubali muharibu nchi hakika hamtaweza
 
Hili swali unatakiwa kwanza uanze kujiuliza wewe, halafu ujiulize tumefikaje hapa!

Japokuwa hutakubaliana na mimi lakini naweza kesema bila kupepesa macho kuwa Kikwete ndio katufikisha hapa. Anafanya mambo ya kiswahili swahili, hana kipaji cha utawala na hana vision.

Kwa kifupi tatizo letu ni ombwe kuu la uongozi ndio limetufikisha hapa.
 
Nikikuita mnafiki sijui kama nitakuwa nimekosea kwani hata wewe umeshindwa kutuelezea ni kitugani unacho jaribu kutuambia kwa hiyo na wewe ni mmoja wao. (nyani haoni kundule)
 
Sijui ni upeo wangu wa kuelewa mdogo? Maana sijaona chochote zaidi ya UNAFIKI wa MJENGWA, na ni kawaida yake kutoa vithread ambavyo vinabaki hewani, siyo kwamba vinahitaji CRITICAL THINKING, lakini vimekaa kishabiki shabiki hivi, as if yeye ni GREAT THINKER, kwamba anataka watu wafikiri kabla ya kurespond, lakini no matter how hard you will try to cogitate, hakuna chochote cha maana unachokipata zaidi ya UNAFIKI NA UCHONGANISHI!!! Na kawaida yake huwa harudi kujibu hoja, UPUUZI TU!!!!
 
very stupidity mjengwa kuwa na akili za hovyo namna hii na kuwaza kwa kutumia masaburi,nacho sikitika mpaka sasa upo uraiani na bado huna hata soni una post uzi ndani ya sintofahamu hii.umemtumia ludo kama cdm.godamn an sham on u.put out u a ass
 
Sijui
ni upeo wangu wa kuelewa mdogo? Maana sijaona chochote zaidi ya
UNAFIKI wa MJENGWA, na ni kawaida yake kutoa
vithread ambavyo vinabaki hewani, siyo kwamba vinahitaji
CRITICAL THINKING, lakini vimekaa kishabiki
shabiki hivi, as if yeye ni GREAT THINKER, kwamba
anataka watu wafikiri kabla ya kurespond, lakini no
matter how hard you will try to cogitate
, hakuna chochote cha
maana unachokipata zaidi ya UNAFIKI NA
UCHONGANISHI
!!! Na kawaida yake huwa harudi kujibu hoja, UPUUZI
TU!!!!

Kama Mjengwa ni mtu makini basi nategemea atarudi hapa kuweka mambo sawa, miye nadhani labda alikuwa anamaanisha jinsi Mwampamba alivyojifanya kumwelezea Ludovick jinsi anavyomjua. Mjengwa hajaridhishwa na maelezo yale.

Huu ni mtazamo wangu tu.
 
Anamaanisha watu wanamjua LUDO halafu wanamkana

huyu jamaa mnafiki tu, yeye kamtosa ludovick kisa ametuhumiwa! Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki,hata kama ludovick katuhumiwa lakini hajamtendea haki kumtosa tena kwa matangazo!
 
yani we jamaa utanipatia ban yangu ya kwanza tokea nijiunge hapa Jf!
 
Ni kweli Mjengwa!! Watu wanakuwa marafiki kabla hujapatwa na maswahibu, unapopatwa hata KIBARUA CHAKO WANAKISITISHA, WANAJITENGA NAWE WAKATI HATA WAKATI UNAKAMTWA ULIKUWA UKIFANYA KAZI ZAO!! PATHETIC!!
 
"Ndugu zangu,
Hatari kubwa ninayoiona mbele yetu ni kwamba, uzalendo, utu na udugu miongoni mwetu Watanzania unaondoka kwa kasi ya ajabu, nyuma yake kumeachwa ubinafsi uliotamalaki na wenye kutanguliza zaidi maslahi- na si maslahi ya umma, ni ya binafsi.

Maana, unajiuliza; ni kwa nini mtu anayekufahamu vizuri anashindwa kukuelezea kwa uhalisia jinsi anavyokufahamu. Badala yake, kwa makusudi, na kwa nia ovu, anaupotosha ukweli?

Na bado atakuita ndugu!"- Tafadhali Usininukuu.

Maggid Mjengwa,
Iringa
http://mjengwablog.co.tz

yani we jamaa utanipatia ban yangu ya kwanza tokea nijiunge hapa Jf! Mtindo wako wa kuweka mabandiko mfu na kuanza kuchungulia kama unasoma headlines za magazeti bora usilete mada hapa.
 
Back
Top Bottom