Kuna wimbo wake Sacramento naupenda sana. Kila ninapoupiga unanikumbusha ujana wangu nikiwa Mwalimu. Tulikuwa na kijoint fulani jioni tukienda kula nyama choma, kupata kinywaji na kusikiliza muziki Congolee. A prolific music writer indeed. Kusikia kafariki roho imeniuma sana jamani mwenzenu. Naona nitapiga sana huu wimbo iwe njia yangu ya kuomboleza Tabu Ley. Sacramento, Sango Lamu.... Lakini pia nazipenda nyimbo zake Mokolo nakokufa, Felly Mour, na zile nyimbo nyingine aliimba kipindi chake na Mbilia Bel. RIP mwana wa Afrika. Tulikupenda sana...lakini Mungu kakupenda Zaidi.