Tabora yarudisha chenji ya Mil. 300 hazina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabora yarudisha chenji ya Mil. 300 hazina

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Mar 29, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MKOA wa Tabora umerudisha hazina Sh 326,192,517 walizopaswa kulipwa walimu wa Shule za Msingi baada ya kubainika kiasi hicho cha fedha kilizidi ikilinganishwa na madai yao halali. Madai ya walimu hao yalikuwa Sh 1,167,856,406 lakini baada ya kuhakikiwa yalionekana halali kulipwa ni Sh 841,662,889 hivyo fedha zilizobaki zimerudishwa hazina.

  My take
  Tukio hili ni kuonyesha uaminifu au kujipendekeza,
  au wameogopa PCCB wangezifisadi wangejulikana,
  au mgao haukueleweka mtu akamwaga unga,
  Kama wamezirudisha hazina ina maana Tabora hakuna madai zaidi ya malimbikizo ya mishahara ya walimu
  Nani alizidisha madai hayo na je kaadhibiwa?
  Je hazina imeridhika kurudishiwa? kama wameridhika kabla ya kuzitoa ilijiridhisha kuwa hakukuwa na udanganyifu wa madai?

  Mimi huwa najiuliza kwani tunapozungumzia utawala bora ni nini hasa ni kuona mtu anahubiri utawala bora au kuona matendo, je matukio kama haya yanahusika au hayahusiki na utawala bora elewa huu ni mkoa mmoja tu ambao angalau wamediliki.
  Mwisho napenda kuuliza hapa mzembe ni nani aliyepeleka hazina idadi zaidi ya mahitaji au hazina iliyotoa pesa bila kuhakiki.
  Ni tukio moja tu lakini tukijibu maswali hapo juu itawakilisha jinsi mali ya umma inavyotumika bila uangalifu, na ukiangalia kwa juu juu utasema kuna tatizo gani wakati pesa imerudi ilikotoka?
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Madiwani wote wa Tabora wanatakiwa kufutwa kazi mwezi wa kumi kwa kutokuchaguliwa tena mkoa wenyewe uko nyuma kwa kila kitu si wangechimbia bwawa jipya la kuhifadhi maji manake lilopo lilichimbwa wakati wa mkoloni na maji hayatoshelizi katika mji wa tabora au wangenunua madeski kwenye shule zao au basi wanunua ambulance ,ziwasaidie wa mama wajawazito wanapotaka kujifungua badala ya kurudisha fedha hazina ambazo zitatumika kuwaongezea CCM kwenye harambee yao ,Kwanza mwenyekiti wa halmashauri ya Tabora ni nani anaruhusu chenzi zote hizo kurudi hazina kweli maskini ataishia kuwa maskini milele
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mkuu waliomba hela za kulipa walimu, wamepewa; zimezidi wanatakiwa kurudisha. Is that simple....
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tabora yangu hii walimu wenyewe shule za msingi wa kuhesabu.
   
 5. m

  miner Member

  #5
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari hii haijakaa sawa madai ya walimu yalichukua muda mrefu kulipwa mpaka yalipohakikiwa hivyo basi pesa iliyopelekwa Tabora ilikua ni kiwango ambacho tayari kimehakikiwa inakuaje pesa zilizopelekwa ni zaid kuliko madai halisi lipo tatizo mahali fulani HAZINA. Serekali hii jamani kila mahali ni tatizo
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Watanzania bwana
  Sasa inaonekana kurudisha kisicho halali ni ujinga, teh teh teh teh.harafu hapo hapo unapiga dhidi ya ufisadi, na kubwata eti unataka viongozi wanaofuata sheria na kanuni teh teh.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu hata wangeema wameomba milioni moja ya kumalizia takweimu ungesema

  nadhani sasa inatosha iwapo tutaishia kuwa stereotypes bila analytical skills etc

  come again bro
   
 8. Kiwalani

  Kiwalani Senior Member

  #8
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu, suala ni kwamba kwa nini zilizidishwa in the first place??!! Inavyotakiwa ni kwamba orodha iliyoomba pesa wizarani iwe sawa na ya malipo huko Tabora; na si vinginevyo.
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MkamaP ukisoma para yangu ya mwisho(red) niliitoa makusudi kwa sababu nilijua kuna watu wa type kama yako watahoji hicho unachohoji, tatizo si kurudisha kisicho halali tatizo ni kimepatikanaje nani amesababisha kiwe si halali?
   
Loading...