Tabora: Serikali kuanza msako kwa wasio na vitambulisho vya ujasiriamali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa onyo kwa wajasiliamali watakaokaidi kuchukua vitambulisho vya wajasiliamali wasije wakalalamika kufuatia hatua zitakazochukuliwa na Serikali wakati wa kufanya msako wa vitambulisho hivyo kwani watakuwa wamekiuka agizo halali la Serikali.

Mwanri ametoa kauli hiyo akiwa wilayani Kaliua alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara akiwataka ili kupata uhalali wa kuendelea kufanya shughuli za ujasiliamali ni lazima wakate vitambulisho ambavyo kila mjasiliamali atakilipia shilingi elfu ishirini huku akiwanyooshea kidole watendaji watakaoshindwa kutoa vitambulisho hvyo kwa wakati.

Kwa mwaka huu Halmashauri ya wilaya ya Kaliua imepokea jumla ya Vitambulisho elfu sita pungufu ya vile vilivyotolewa mwaka jana ambapo mwaka jana jumla ya vitambulisho elfu nane.

Upatikanaji kwa vitambulisho kwa wajasiliamali wadogo kumesaidia kupunguza usumbufu waliokuwa wakiupata hapo awali.
 
Naomba kupewa tofauti ya mfanyabiashara anaetakiwa kupewa leseni na huyu wa kitambulisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…