Tabora pagumu kweli. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabora pagumu kweli.

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Baba Matatizo, May 6, 2011.

 1. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wana JF naomba yeyote aliyeko mkoani TABORA anisaidie kutafuta kazi yoyote ile ya kufanya.HATA KAMA NI ULINZI.Elimu yangu ni form six.Nimechoka kunyanyaswa kisa sina kazi.Naomba niwasilishe mada!
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mami,

  Fanya mpango basi uanzishe kitawi cha CHADEMA hapo sijui Kanyenye au Isevya?

  Pia angalia uwezekano wa kujiajiri kama kilimo kwani Tabora, ina ardhi kibao.

  Amini nakuambia, ukitumia akili zaidi na nguvu zaidi mwanzo, unaweza kujikuta baada ya miaka 5, ukaniandikia kuwa umenunua gari na nyumba. Uwezekano upo ila tu inabidi utumie akili kwelikweli na visenti vya mwanzo viwe ni mtaji na si kuongeza wake mmoja baada ya mwingine kama kawaida ya Wanyamwezi.

  Ikibidi, basi nenda mbali na mji maana Tabora mjini na miji ya karibu, vibaka wengi sana.

  Ningelikukaribisha Sikonge ila kwa sasa nipo Ushirombo hadi mwakani.

  Ila bado waweza kwenda huko kama ukitaka. Unaweza kuanza na kilimo na ukafungua kiduka chako ambacho ukitumia elimu yako ya Form Six basi utaweza kufika mbali. Mie nimewashawahi kuwaona jamaa wamemaliza Uhandisi na wamefungua kampuni yao ya ujenzi kwa kufunga nondo kwenye majengo. Wanakufungia nondo kwa speed ya ajabu na wana hela yao nzuri sana hadi leo hii.

  Usije ukaona kuwa kwa kuwa wewe ni Form Six basi lazima uajiriwe kazi ofisini wakati wale wa Chuo Kikuu cha Kata Dodoma hata wao hawana kazi. Kama utataka basi naweza hata kukuambia ni zao gani uanze nalo. Waweza kwenda Chuo cha Kilimo Tumbi na watakupa ushauri mzuri sana. Usiogope kazi za mikono kwani ni zoezi tu na waweza kuzoea.

  Kila la kheri katika kuanza UJASIRIMALI.
   
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwani hapo unaishi na nani? Unyanyaswe na nani? Kazi gani unadhani unao uwezo wa kufanya, zenye fani ya ulinzi,jeshini,sungusungu ama?
   
 4. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Naishi na father wangu ila ni MTATA ile mbaya!nikisema ulinzi namaanisha kwenye makampuni!Hata hivyo sichagui KAZI.
  Naomba msaada jaman!
   
 5. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ASANTE SANA ILA SINA MTAJI WA KUANZISHA UJASIRIAMALI.Niliomba KAZI ya msimu pale tumbaku wanadai 30000,ili nipate kazi!
  Jamani mambo magumu!
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wee jaribu kutafuta kazi yoyote upate nauli. Vijijini huko unahitaji tu jembe na shoka na waweza anza kazi. Yaani hamna hata kazi ya ualimu? Kubeba zege, kubeba magogo? Kibaya kinachonishtua ni kuwa huna hata dola 20 za kuombea kazi. Hapo kweli kasheshe.

  Unajua ili usaidiwe, lazima na wewe ujisaidie. Sidhani kama kweli hakuna kikazi chochote unaweza kufanya ili uanzishe kilimo. Tabora ni very cheap vitu vingi kwani haina hela. Hebu nenda kwa Mbunge wako huyo Msomali na mwelezee shida yako ila nenda ukiwa umeweka mipango yako kwenye karatasi na mwambie ungelihitaji fedha kadhaa ili uanzishe kishughuli kidogo sana. Hiyo kitu isizidi Laki moja na nusu. atakupatia kikazi fulani ufanye na ukishapata hela yako, TIMKA.

  Anza kuwa na fikira za kuanza kujitegemea, achana na lazima uajiriwe, otherwise: YOU ARE DEAD WITHOUT MONEY.
   
 7. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hunitakii mema?Huku ukianzisha tawi la CDM ni hatari mno!wanabana mbavu!
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wazungu wamefanikiwa kwa kubanwa mbavu. Kama unataka kufanikiwa, basi jirushe uwanjani.

  Wakikubana mbavu ndiyo wanakupa umaarufu. Wengine walifanikiwa na wengine hawajafanikiwa.

  Ndiyo maana Mandela yuko juu kwa sababu alibanwa mbavu. Akina Nyerere pia.

  Sasa wewe unataka nini duniani? Au ufuate njia nyeupe..... au ufuate njia ngumu.

  Mchumia juani, hula kivulini. Na Mchumia kivulini, kama sikosei atakula JUANI.
   
 9. A

  Ame JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Kwanini ukalinde vya watu na kuacha kutafuta cha kwako? Sikonge kakupa ushauri mzuri sana. Ujue waweza hata kuamua kuosha magari kwakuwatumia vijana then baadaye mtaji ukiwa mkubwa unafungua car wash baadaye kidogo egosho la magari baadaye unanua na wewe la kwako la mizigo then unafungua petrol station mpaka baadaye unakuwa Aziz mkubwa hapo Tabora. Usidharau mwanzo mdogo maana hesabu haikamiliki bila namba hizi mbili muhimu 0 na 1na as you move your zero from its locus/loci? it reaches a point itakapo ipita 1 ina make 10 na hapo ndipo namba za hesabu zinakuwa zimekamilika.
   
 10. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Badilisha kwanza hilo jina lako, utajiitaje baba matatizo afu udhani matatizo yatakuisha? We mwenyewe umeyakubali. Pia ondoka huko Tabora pengine kaziako haiko huko, mungu ni mwaminifu atakusaidia kwani UTAJIRI NA HESHIMA VIKO MIKONONI MWAKE.
   
 11. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Dah ndugu..inaonesha una stress sana...sehemu zote hapa tz ni ngumu,si tu tabora. Najua situation uliyo nayo coz mi nishapitia huko,manake hadi home unaonekana mzigo,huna faida n.k na kama dingi ndio mtata duh sipati picha.
  Anzisha tuition kama vp..then mdogomdogo,hii itakukeep busy kiaina coz tabora shule nyingi hazina walimu, mi nilisoma hapo tabora boys,napafahamu sana. Biashara ya tuishen nahisi italipa tu, coz walimu wengi toka dar hawapendi kwenda tabora coz of transportation. Shule kama Kazima ,Uyui au Milambo wanafunzi muda wote wapo mtaani tu wanarandaranda,so take my note broo!!
   
 12. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,058
  Likes Received: 3,085
  Trophy Points: 280
  Kimsingi nakushauri utumie akili yako yote,toa mikono mfukoni,ondoa aibu yako,toka nyumbani kwenu usipende kukaa mda wote hapo kwenu asubuh-jioni,jione kama umehitimu fm4 na si6 ili usiendeshwe na elimu yako bali matatizo yako,usisahau kuomba kwa Mungu wako.

  Ukweli ni kwamba Tabora ni ngumu kidogo hvyo ni lazima uwe kama kichaa kwanza,mkoa ni mgumu kwa maana una vitabia vingi vya kiswahili,kiarabu,kahawa nyingi,hamna biashara kubwa kubwa,viwanda n.k,jaribu hata tuisheni kwa hela ndogo tu then ukiona inaripa unaongeza kidogokidogo
   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,869
  Likes Received: 2,814
  Trophy Points: 280
  Mtu mwenyewe Six imekuona halafu bado unang'ang'ania nyumbani kufanya nini? Tumia akili yako hiyo kidogo uliyonayo ili uweze kutoka kukaa nyumbani tangu asubuhi bila kazi kwanini father asiwe mtata? Fanya kazi dogo acha kulalamika tu. Mkitaka mali mtayapata shambani! Nenda kalime dogo maana shule ilikuwa ngumu.
   
 14. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  hii ni akili nimekubali
   
 15. M

  Mwana Mnyonge JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  komaa kaka maisha ni kujituma penda kujiajiri na sio kuajiliwa utatumia muda mwingi sana kwa mwajiri wako lakini napatwa na wasiwasi elimu tunayopata inamfanya mtu apende kuajiliwa badala ya kujiajiri ni muhimu mitaara yetu ya elimu ikabadilishwa imjenge mtu kujiajiri badala ya kuajiriwa
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,490
  Likes Received: 19,887
  Trophy Points: 280
  umepata div gani? i mean whats ya result
   
 17. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Komaa mdogo wangu,utafanikiwa tu.Jaribu na ujasiriamali.
   
 18. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu nilikuwa nakufikiria lakini nimeshindwa kuelewa kama kweli uko serious, nimeunganisha post ya Sikonge na ya kwako, halafu hapo kwenye bluu, sijakuelewa kabisa. unajua kwanini gonga hapa chini
  Natafuta PC ya laki mbili!
  kuwa mkweli...
   
 19. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kaka hiyo namtafutia mtu kwa kuwa yeye hana analolijua zaid katika technologia,Ndio sababu namsaidia kumtafutia.Hapo me ni WAKALA TU!
   
 20. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nimekuelewa mkuu!
  Nikiwa sehemu za mjini
  nitaku PM.
  Ili niangalie tunafanyaje,
   
Loading...