Tabora: Mfamasia kizimbani kwa kuiba dawa za kufubaza UKIMWI (ARV)

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mfamasia wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora, Francis Mlesa (33), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo kwa tuhuma za wizi wa dawa za wagonjwa

Mwendesha Mashtaka, Joseph Mwambwalu, alidai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na shtaka moja la wizi.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Edda Kahindi Mwambwalu, alidai Desemba 24, mwaka jana majira ya usiku, katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mtuhumiwa akiwa mwajiriwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, anatuhumiwa kuiba chupa 30 za vidonge vya dawa ya kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARV) zenye thamani ya Sh. 2,116,000.

Mwambwalu, alidai kuwa huku mshtakiwa huyo akitambua kwamba yeye ni mtumishi wa umma, aliamua kutenda kosa hilo kinyume cha kifungu 270 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Hata hivyo, baada ya mshtakiwa huyo kusomewa shtaka lake, alikana na hakimu kuiahirisha kesi hiyo hadi Januari 31, mwaka huu, na mshtakiwa yuko nje kwa dhamana ya Sh. 300,000 kwa maandishi.
 
MFAMASIA wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora, Francis Mlesa (33), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakmu Mkazi wa wilaya hiyo kwa tuhuma za wizi wa dawa za wagonjwa.
court.jpg

Mwendesha Mashtaka, Joseph Mwambwalu, alidai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na shtaka moja la wizi.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Edda Kahindi Mwambwalu, alidai Desemba 24, mwaka jana majira ya usiku, katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mtuhumiwa akiwa mwajiriwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, anatuhumiwa kuiba chupa 30 za vidonge vya dawa ya kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARV) zenye thamani ya Sh. 2,116,000.

Mwambwalu, alidai kuwa huku mshtakiwa huyo akitambua kwamba yeye ni mtumishi wa umma, aliamua kutenda kosa hilo kinyume cha kifungu 270 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Hata hivyo, baada ya mshtakiwa huyo kusomewa shtaka lake, alikana na hakimu kuiahirisha kesi hiyo hadi Januari 31, mwaka huu, na mshtakiwa yuko nje kwa dhamana ya Sh. 300,000 kwa maandishi.

Chanzo: IPP Media
 
hizi dawa hutolewa bure sasa alikuwa anazipeleka wap? ama kulishia mifugo (maana nasikia nguruwe hupewa wanenepe)

ama kuwapa watu wasiopenda kupanga foleni?
 
Huko Igunga Hospitali nako wana viroja.
Mwaka jana tena Mtumishi wa hiyo hospitali alibaka binti ambaye alikuwa anamuuguza mama yake baada ya kumlewesha kwa madawa
 
Back
Top Bottom