Tabora: Ajali ya Ndege ndogo ya U Dream ya Afrika Kusini yaua wawili

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Ajali ya ndege imetokea mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu wawili ambao ni rubani wa ndege hiyo na abiria wake.

Watu hao ni raia wa Afrika Kusini na walikuwa wakielekea nchini Malawi.

78DDA258-A4FE-46B8-81BD-816D32D0205E.jpeg

04225755-4664-459D-9955-ABCE6BF126DA.jpeg

Mkuu wa wilaya Magili amesema Ndege hiyo ilikuwa inaelekea Lilongwe Malawi na baada ya kupata hitilafu ndipo ikatua jambo ambalo mamlaka ya uwanja wa ndege ilikuwa haina taarifa juu ya ndege hiyo, kufuatia tukio hilo sasa mkuu huyo wa wilaya amesema wamekusanya majivu na kuyapeleka hospitali ya Tabora kwa ajili ya uchunguzi.

Mamlaka ya Anga yatoa ufafanuzi ajali ya ndege

Ndege ndogo ya U Dream ya Afrika Kusini iliyokuwa ikitokea Entebbe Uganda imeanguka leo mkoani Tabora na kuuwa rubani na msaidizi wake wote raia wa Afrika Kusini, muda mchache tu baada ya kupaa angani.

Akizungumza na EATV kuhusu ajali hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga (TCAA), Hamza Johari, amesema ndege hiyo iliomba kutumia anga la Tanzania na iliomba kutua Tabora kwa dharura baada ya kupata hitilafu, ikiwa njiani kuelekea Lilongwe nchini Malawi.

Amesema kuwa baada ya kutua Tabora wahusika waliifanyia matengenezo na baada ya kuridhika kuwa wamemaliza waliomba kuruka kuendelea na safari lakini baada ya kupita dakika tano tu, waliomba kutua tena wakisema injini imeshindwa kufanya kazi.

“Baada ya kuruka kama dakika tano hivi walipiga simu wakisema wamepata hitilafu injini imeshindwa kufanyakazi, tukawaruhusu kutua tena lakini hatukuwaona wakirudi ndipo tukafuatilia na kubaini kuwa imeanguka,” alisema Bw. Johari.

Amesema kuwa wamefanikiwa kupata miili yote miwili ikiwa imeungua kutokana na ndege hiyo kulipuka moto na kuteketea baada ya kuanguka, ambapo miili hiyo kwa sasa imehifadhiwa katika hospitali ya Kitete. Timu ya wataalama wa anga imeshatumwa kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.
 
Which is which sasa?ndege imetua au imepata ajali na kubaki majivu?
 
Watu wawili raia wa Afrika Kusini wamefariki kwa ajali ya ndege iliyoanguka na kuteketea kwa moto wilayani Sikonge Mkoani Tabora ikitokea Uganda kuelekea Malawi.

Watu hao waliofariki ni rubani wa ndege hiyo na abiria wake.
IMG_20190803_213903.jpg
IMG_20190803_213905.jpg
 
Very soon ile dhana kwamba “usafiri wa ndege ni safety mode of transport” itabidi tuiangalie upya. Ajari za ndege sasa zinakuwa common mno kuliko hata zile za mabasi ya kwenda mikoani. These days ukipanda pipa na kutua salama unamshukuru Mungu. RIP marehemu.

Kila siku namuomba Mungu Jiwe asipitiwe na kutia mkono kwenye zile mandatory maintenance schedules za ndege za Air Tanzania kama alivyofanya kwenye upakaji wa rangi. Ile mambo haihitaji siasa. After certain number of flying hours, lazima ndege iende garage.
 
After certain number of flying hours, lazima ndege iende garage

Wanakuambia mbona inatembea kwanini tuingie gharama kwa kitu ambacho tayari kinafanya kazi hawajui kama utaratibu unapokiukwa ndipo wanaosa nafasi ya kusema wanayosema kwakuwa wanakuwa marehemu, in other words huwa wanajisahau wanadhani likitokea janga ndipo watarudi kurekebisha makosa wakati tayari ni marehemu, ni kama mtu anayesema niende hospitali kufanya nini mbona naumwa lakini sijafa
 
Mamlaka ya Anga yatoa ufafanuzi ajali ya ndege

Ndege ndogo ya U Dream ya Afrika Kusini iliyokuwa ikitokea Entebbe Uganda imeanguka leo mkoani Tabora na kuuwa rubani na msaidizi wake wote raia wa Afrika Kusini, muda mchache tu baada ya kupaa angani.

Akizungumza na EATV kuhusu ajali hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga (TCAA), Hamza Johari, amesema ndege hiyo iliomba kutumia anga la Tanzania na iliomba kutua Tabora kwa dharura baada ya kupata hitilafu, ikiwa njiani kuelekea Lilongwe nchini Malawi.

Amesema kuwa baada ya kutua Tabora wahusika waliifanyia matengenezo na baada ya kuridhika kuwa wamemaliza waliomba kuruka kuendelea na safari lakini baada ya kupita dakika tano tu, waliomba kutua tena wakisema injini imeshindwa kufanya kazi.

“Baada ya kuruka kama dakika tano hivi walipiga simu wakisema wamepata hitilafu injini imeshindwa kufanyakazi, tukawaruhusu kutua tena lakini hatukuwaona wakirudi ndipo tukafuatilia na kubaini kuwa imeanguka,” alisema Bw. Johari.

Amesema kuwa wamefanikiwa kupata miili yote miwili ikiwa imeungua kutokana na ndege hiyo kulipuka moto na kuteketea baada ya kuanguka, ambapo miili hiyo kwa sasa imehifadhiwa katika hospitali ya Kitete. Timu ya wataalama wa anga imeshatumwa kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.
Screenshot_20190804-064118_Facebook.jpeg
 
Back
Top Bottom