Tabora: Ajali ya Ndege ndogo ya U Dream ya Afrika Kusini yaua wawili

Duh... hizi ajali za ndege ukipona huwezi panda ndege tena... maana huwa hazibakizi mtu
 
Ajali ya ndege imetokea mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu wawili ambao ni rubani wa ndege hiyo na abiria wake.

Watu hao ni raia wa Afrika Kusini na walikuwa wakielekea nchini Malawi.

View attachment 1171822
View attachment 1171823

Mkuu wa wilaya Magili amesema Ndege hiyo ilikuwa inaelekea Lilongwe Malawi na baada ya kupata hitilafu ndipo ikatua jambo ambalo mamlaka ya uwanja wa ndege ilikuwa haina taarifa juu ya ndege hiyo, kufuatia tukio hilo sasa mkuu huyo wa wilaya amesema wamekusanya majivu na kuyapeleka hospitali ya Tabora kwa ajili ya uchunguzi.



Mamlaka ya Anga yatoa ufafanuzi ajali ya ndege

Ndege ndogo ya U Dream ya Afrika Kusini iliyokuwa ikitokea Entebbe Uganda imeanguka leo mkoani Tabora na kuuwa rubani na msaidizi wake wote raia wa Afrika Kusini, muda mchache tu baada ya kupaa angani.

Akizungumza na EATV kuhusu ajali hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga (TCAA), Hamza Johari, amesema ndege hiyo iliomba kutumia anga la Tanzania na iliomba kutua Tabora kwa dharura baada ya kupata hitilafu, ikiwa njiani kuelekea Lilongwe nchini Malawi.

Amesema kuwa baada ya kutua Tabora wahusika waliifanyia matengenezo na baada ya kuridhika kuwa wamemaliza waliomba kuruka kuendelea na safari lakini baada ya kupita dakika tano tu, waliomba kutua tena wakisema injini imeshindwa kufanya kazi.

“Baada ya kuruka kama dakika tano hivi walipiga simu wakisema wamepata hitilafu injini imeshindwa kufanyakazi, tukawaruhusu kutua tena lakini hatukuwaona wakirudi ndipo tukafuatilia na kubaini kuwa imeanguka,” alisema Bw. Johari.

Amesema kuwa wamefanikiwa kupata miili yote miwili ikiwa imeungua kutokana na ndege hiyo kulipuka moto na kuteketea baada ya kuanguka, ambapo miili hiyo kwa sasa imehifadhiwa katika hospitali ya Kitete. Timu ya wataalama wa anga imeshatumwa kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.
Hapa kuna watu wanatamani hiyo ingekuwa air Tanzania
 
Back
Top Bottom