Kwa uelewa wangu wazungu wote sio sawa wanatofautiana kama nchi zetu lakini wana uelewa zaidi yetu na hiyo inatokana na malezi ya tangu utotoni kwa mfano mtoto asiongee na strangers au kupokea zawadi yoyote na pia kuingiliana kwa maisha yaani kila mtu kivyake. Hao ni British lakini wanapenda sana gossip (udaku) kuhusu kunuka kwao hilo kila binadamu wana harufu zao kutokana na vyakula vyao, hata mhindi utasema ana harufu lakini nae anakushangaa wewe, wana tabia zingine kama niseme labda uchoyo maana hata mkiingia hotel kila MTU alipe chake hakuna kulipiana, hao ni western Europeans tofauti na eastern ambao wao wanaishi kama sisi kwa kusaidiana na kutembeleana hata kama ni rafiki tu, hiyo tabia pia wanayo wataliano yaani kuishi pia na wazazi wao hata wakiwa wakubwa na kazi zao bado wanawajali wazazi, wazungu kwa tabia hizo alizozitaja siziafiki nyingi kwani wengi wanaokuja huku kama volunteers ni waliomaliza shule na kuja kujionea maisha au kutoa msaada wa aina yoyote kwa hiyo wanakuwa na matumizi ya kukidhi mda wapo hapa na kuishi kama sisi hawawezi kuishi hotel kubwa, wa Irish pia ni wazuri wanakuja kukugongea na kukuomba maziwa au chochote kile, watakusalimia na msaada wanao, naona alieleta mada ameona baadhi ya wazungu aidha anafanya kazi baa au hotel Porter maana ameona maisha yao ya kunya tu na sio maisha kwa ujumla, hebu angalia anaposema wanaingia toilet bila viatu lakini haoni ndugu yake alieingia chooni na viatu halafu baada ya kurudi sitting room akapandisha miguu na viatu juu ya sofa akiona ni uzungu. Maisha ni malezi sio kuiga nani amefanya nini