Unampa hela ya nauli anakuuliza,"una 100???"
Kama hauna unasubirishwa chenchi na usipodai hupati hiyo100
Wengine bila aibu et 100 tu unadai?
Kama hana chenchi si dhambi akikuambia usubiri almradi akupatie au kama unayo mia mmpe ili akupatie mia mbili.
1. Unalipa nauli lets say unatoa elfu moja, na nauli ni mia nne, konda anakuuliza wangapi? Kama ninao watu/ mtu wa kumlipia si ningesema mweneyewe!
2. Unatoa shilingi elfu kumi, konda anaanza kulalamika oo unatoa hela kubwa mara kimepanda kimeshuka na maneno machafu kibao. Mimi akiniuliza huna hela ndogo hapo mpaka utoe hii, namwambia ninayo nachukua elfu kumi yangu nampa mia, maana ndio hela ndogo niliyonayo, konda anaona anadharauliwa. Unanipangiaje pesa ya kutumia? Kama huna chenchi mimi inanihusu nini?
3. Unatoa nauli mathalani elfu 2, 5 au 10, konda hakupi chenchi anasubiria sijui usahau ili a-make super profit! Huwezi fanikiwa kwa kuiba vi elfu mbili mbili vya abiria.
Ongezea na wewe kero zako.
Kweli mkuu,unakuta gari limejaa abiria halafu konda anapiga kelele gari nyeupe, abiria wakimwambia gari imejaa anasema gari haijai inajaa ndoo ya maji.konda kunidanganya eti kuna siti kumbe hakuna....
konda chenchi ni mia, anatoa safaru ya mia mbili anasema tutagawana na abiria mwenzangu....
konda gari imejaa bado anapoga kelele nje eti gari iko tupu....
nashukia manzese darajani ye kona ananilazimisha kushukia tiptop eti darajani hasimami....
Kweli mkuu,unakuta gari limejaa abiria halafu konda anapiga kelele gari nyeupe, abiria wakimwambia gari imejaa anasema gari haijai inajaa ndoo ya maji.
Unampa hela ya nauli anakuuliza,"una 100???"
Kama hauna unasubirishwa chenchi na usipodai hupati hiyo100
Wengine bila aibu et 100 tu unadai?
Mkuu kama unawahi kibaruani utakaa umsubiri konda kweli? Kazi zenyewe za macapitalist,tena ukute mhindi ndio bosi wako utakuta kavimba mashavu kama anapuliza moto vile.Itabidi ile kwake bhana ili ajifunze kutembea na chenchi za kutosha.Kama hana chenchi si dhambi akikuambia usubiri almradi akupatie au kama unayo mia mmpe ili akupatie mia mbili.
Kweli mkuu,unakuta gari limejaa abiria halafu konda anapiga kelele gari nyeupe, abiria wakimwambia gari imejaa anasema gari haijai inajaa ndoo ya maji.
Sasa kwa maana hiyo nikiwa na shilingi elfu kumi asubuhi nizurure kutafuta chenchi? au nisipande daladala?kukosa kwake chenchi mimi inanihusu nini? au ni dhambi kutoa elfu kumi asubuhi kwenye daladala?Ukisema makonda ni wachafu nitakuunga mkono. Lakini hili la chenchi linawahusu abiria na kondakta ambao lazima tuwasemee maana muda wa kuingia humu hawana. Ni asubuhi abia wanne wanatoa noti za sh. Kumi 10 sawa na sh 40, 000 wkt nauli ni sh 500?