Tabia ya Watu mitaani Kusema ameshindwa hata Ualimu

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Hiki kinatoa Taswira gani? Wakati wa Matokeo ya Sekondari hasa kidato cha nne na sita huwa ninaskia eti mtoto wa fulani ameshindwa hata Ualimu ila huwa nashindwa kuelewa wanamaanisha nini? kauli hii husikika hata kwa wauza Vitumbua na Chapati mitaani.

Nimeona ni vyema leo nianzishe mjadala kwanini wanasema hivi
 
Hizo in kauli za kijinga kwani kunawatu ni walimu tena ukikopea cheti chake na cha engineer utakuta mwalimu Ana one ya point 7 au 8 lkn engineer amepata one ya point 9 au 2 ya 12 tena nowadays hata 2.0 unakuawa engineer
 
Kuna watu mtaani wanafikiri wanaokwenda kusomea ualimu ni wale waliofeli. Ila ukweli hauko hivyo!
 
Ualimu na uaskari huwa ni option iliyobaki kwa mtu aliye feli

Don't cheat yourself! labda kwa hao askari watajitetea wenyewe ila upo absolutely wrong! nikupe mfano mdogo tu, wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza shahada ya elimu(Bed) na elimu na sanaa(Baed) waliojiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam(udsm) intake ya mwaka 2005 hakuna aliyekua na division three!! Wengi walikua ni one na two tu!
Tena hao wanachuo wote walipatikana baada ya mchujo wa mtihani wa chuo kwa wakati huo yaani Multiculation!! sasa wewe unawaongelea walimu wa kada ipi? kama ni wa grade A siku hizi nayo imefutwa walimu wote wenye sifa hizo wanajiendeleza ili wawe na diploma ya shule za msingi!!
Siyo vyema kuongea au kuandika kitu kwa sababu tu uliwahi kusikia au kudanganywa na mtu fulani! Hao walimu mnaowadharau ndio waliowafundisha kuvaa vizuri, muwe na maarifa walau kiduchu, kuoga, nidhamu, nk.
Na kama hujui, hata rais wako na waziri mkuu wako wote ni walimu!! nao walifeli mtihani pia!! basi itakua ni hatari kubwa!
 
Wanaowabeza walimu hao watu wana matatizo makubwa, hata familia zao zina matatizo lukuki...
 
Kuna watu wanaongea wasiyoyajua.
 
Hiki kinatoa Taswira gani? Wakati wa Matokeo ya Sekondari hasa kidato cha nne na sita huwa ninaskia eti mtoto wa fulani ameshindwa hata Ualimu ila huwa nashindwa kuelewa wanamaanisha nini? kauli hii husikika hata kwa wauza Vitumbua na Chapati mitaani.

Nimeona ni vyema leo nianzishe mjadala kwanini wanasema hivi

Ni mawazo tu ya watu wenye akili ndogo ila hakuna ukweli wowote. Huwezi kuwa mwalimu bora kama ulifeli! kama atatokea mwalimu wa aina hiyo basi atakua ni mamluki na daima atakua hajiamini na hata matokeo ya wanafunzi wake yatamhukumu.

Kwa walimu halisi na waliofaulu vizuri ni mwendo wa kupiga tu vipindi na kufaulisha wayoto bila shaka yoyote.
 
Ni Tanzania tu ambako mimi nimeona [inawezekana labda zipo na sehemu zingine] watu ambao hawakufanya vizuri kimasomo shule za upili ambao ndo hupelekwa kusomea ualimu.

Sasa sijui hiyo ndo akili gani tu!

Mtu hakufanya vizuri kwenye masomo yake mnampeleka akasomee ualimu halafu baadaye aje kuwafundisha watoto shuleni?

Huenda ndo maana idadi ya walio wajinga Tanzania ni kubwa sana.

Na matokeo yake ndo hayo ya kudharauliwa kwa fani ya ualimu.
 
Don't cheat yourself! labda kwa hao askari watajitetea wenyewe ila upo absolutely wrong! nikupe mfano mdogo tu, wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza shahada ya elimu(Bed) na elimu na sanaa(Baed) waliojiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam(udsm) intake ya mwaka 2005 hakuna aliyekua na division three!! Wengi walikua ni one na two tu!
Tena hao wanachuo wote walipatikana baada ya mchujo wa mtihani wa chuo kwa wakati huo yaani Multiculation!! sasa wewe unawaongelea walimu wa kada ipi? kama ni wa grade A siku hizi nayo imefutwa walimu wote wenye sifa hizo wanajiendeleza ili wawe na diploma ya shule za msingi!!
Siyo vyema kuongea au kuandika kitu kwa sababu tu uliwahi kusikia au kudanganywa na mtu fulani! Hao walimu mnaowadharau ndio waliowafundisha kuvaa vizuri, muwe na maarifa walau kiduchu, kuoga, nidhamu, nk.
Na kama hujui, hata rais wako na waziri mkuu wako wote ni walimu!! nao walifeli mtihani pia!! basi itakua ni hatari kubwa!
wadanganyee wengine.hiyo intake ya mwaka jana na mwaka juzi ni marks za GPA ambayo ni upuuzi mtupu,
 
Soma vizuri huo mwaka ni 2015 au 2005? au unadhani wachangiaji wote humu ni kizazi cha GPA? Mimi nimetolea mfano wa mwaka 2005! na kama ungekua wa mwaka huo wala usingevamia maelezo yangu kwa spidi kubwa hivyo! kuwa tu mpole ktk hili.
 
mm nafahamu watu waliofel na wanaotaka ajira za haraka na rahis ambazo sio zakuumiza vichwa ndo huenda kweny ualimu
 
Taratibu hii kitu inabadirika. Kwa sasa kujiunga chuo kikuu hasa kwa kozi za arts za ualimu ukiwa na pass marks za chini ni shida sana
 
Kifo cha elimu kilianza wakati wa UPE. Ualimu Pasipo Elimu!
Toka wakati huo, ualimu ni kwa ajili ya watu walioshindwa kila kitu. Mabadiliko yameanza kurekebisha hali hiyo, lakini donda kama hilo halitoki siku moja.
Ni mpaka ifike mahali vijana wetu bora kabisa yaani wenye division one waanze kwenda ualimu ndiyo tutajikomboa.
Kinyume cha hapo ualimu itabakia taaluma yenye kudharaulika at our own expense!
 
Tuseme ukweli. Shule za msingi hakuna mwalimu mwenye Div 1 au 2. Hakuna. Ilitokea mwaka 1977 ambapo waliopata div 2 walipelekwa ualimu. Wamestaafu hao. Waliobaki woote div 111 ya mwishoni na IV na ndio maana hata kujiendeeza inakuwa mtihani.
Sekondari ni mchanganyiko ila wengi wamepiga shule ya masomo 2 na hiyo education.
Angalieni hata hayo matangazo ya kuitwa chuoni yanajieleza vizuuri.
Hatuwadharau. Ndio ukweli mtupu.
Halafu wanadai maslahi kuliko sisi tuliowashinda shule na kupiga nondo kali chuoni.
Kwa kweli waalimu wangedai posho ya usumbufu ( maana kwa kweli watoto ni wengi na wanasumbua) na posho ya nyumba na mazingira magumu kwa wale wa nje ya mji na vijijini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom