Tabia ya wanaume kuwapiga wanawake picha za uchi

Tabia ya wanaume kuwapiga wanawake picha za uchi

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,664
Kuna hii tabia ambayo zamani nilikuwa naiona kwenye movies za Kinigeria, lahaulaah, hata wabongo nao wameiga na kuanza kuziigiza.

Sasa watu wameamua kwenda mbali zaidi na kuweka movies katika vitendo!

Nilimsikia kijana mmoja ambaye nilimrebuke vikali mno, akisema, mabinti wote waliowahi kuwa na mahusiano naye lazima awachukue picha za uchi (au video) tena zenye utata hasa - iwe akiwa anaona au kwa kumvizia kama hataki! Lengo lake ni kwamba iwapo itatokea kutokuelewana kwao baadaye kiasi kwamba huo ugomvi ukamsababishia maumivu au aibu, atalipiza kwa kutoa picha za binti mhusika kwa mtindo wa "episodes" kwenye internet, mfano anaweza kuziupload hata JF, kabla mods hawajashtukia watu kama akina Tyta na #teampicha wanakuwa wameshazipakua.

Hebu imagine umeoana na mkeo halafu umeishi naye miaka 6, ghafla unakutana na picha zake za uchi zimesambaa kwenye internet!

Just to alert you incase you have not been careful enough!
 
Last edited by a moderator:
Anaefanya hivyo ujue sio mwanamme,hata mwanamke akuudhi vipi huwezi kuweka picha chafu Kama hizo,kwani Kama mwanamke hakutaki kwanini ulaImishe penzi? Staki mwenzie basi... Mwanamme wa aina hiyo atakua kaanguka juu ya Bata ndio mana haja timia....
 
Kwa Mwanaume kamili hawezi fanya mambo hayo ya kisoro
 
Looh huyo hajui thamani ya mahusiano na mwanamke anaekuwa nae...
ukijua thaman ya mtu siku zote utamheshimu na kumpenda kwa dhat nata kama mtabreak utaendelea kumheshim
Hao ni vijana wasio jitambua
 
Kwanini na wenyewe wanakubali kupigwa hizo picha kama siyo umalaya ni nini?

Kirikuu, uwe unasoma na kuelewa bandiko kabla ya kuandika chochote!! Kasema huzichukua kwa siri ama kwa wazi....!!

Mwanamke akikataa kupigwa picha basi jamaa anategesha kwa siri bila ya mwanamke kujua!! Umalaya umetokea wapi hapo?
 
Mambo ya kuvuja kwa picha za utupu zimekithiri sana .Si jui ni kwa sababu gani hawa wanawake wanapenda kupiga mapicha ya aina hii.
 
Hili ni issue tata kweli kweli. Dada zetu inabidi wawe waangalifu sana kwenye mahusiano. Siku hizi kuna movie camera ndogo kama kalamu. Inategwa chumbani, binti anadhani ni pen kumbe anarekodiwa.
 
Back
Top Bottom