Tabia ya wanaume kutelekeza watoto wao

Tabia ya wanaume kutelekeza watoto wao

Huu ndiyo ukweli hakuna mwanaume anaeweza kumkimbia mwanae wa kumzaa ila wanawake wanasababisha hayo.mimi nimetoka kazini nimechoka unarudi home daily maneno .hata umfanyie nini anajifanya haoni

Shida si wanawake shida hamjui uchungu wa mtoto ukiujua hata mama awe kama hitler utasimama kwa ajili ya mwanao. Kina mama wanavumilia mangapi makero ya wanaume na kusacrifice furaha zao kwa ajili ya watoto wao.

Mama yako mwenyewe ukute amesacrifice mengi na kumvumilia baba yako ili tu wewe uwe kijana mweny maisha mazuri. Mama zetu wangeamua kufuata mioyo yao na kukimbia majukumu yaonkisa kero za wenzi wao am telling u wengi tungesuffer na kuishia kuwa machokoraa.
 
Hujaelewa mkuu .hapa tatizo si kukimbia majukumu ila kero za mwanamke
 
Afu maisha yakishawazidi nguvu za kiume wanarudi kudai watoto
sperm donors ni janga
 
Hujaelewa mkuu .hapa tatizo si kukimbia majukumu ila kero za mwanamke


Ukijua uchungu wa mtt hata hiyo kero utavumilia ila wengi wenu hamna uchungu. Mama zetu wangeamua kutokuvumilia kero za baba zetu nakwambia wengi tungesuffer
 
Chokochoko

Kabisaaa na hongera kwa single mothers wootee na nitawaheshimu na kuwapenda maisha yangu yootee
 
Last edited by a moderator:
kama haushi na mama toa hela hudumia ndio mpango ila wanaotelekeza ndo sio....mi sipo hivo mi nalea
 
Hongera kwa ujasiri wa single mothers waliotelekezwa ushujaa wao wa kuhimili malezi bila kutarajia peke yako ni jambo kubwa.
Ila kwa wale wanaovizia, wanaoficha watoto, wanaoamua kuwa baba asimuone mtoto haiwahusu hongera yangu
 
Tuombe ushauri wa mada hii toka kwa Dr Slaa yeye mzoefu kakataa kutunza watoto wake anatunza wa mwanamme mwenzake
 
Shida si wanawake shida hamjui uchungu wa mtoto ukiujua hata mama awe kama hitler utasimama kwa ajili ya mwanao. Kina mama wanavumilia mangapi makero ya wanaume na kusacrifice furaha zao kwa ajili ya watoto wao. Mama yako mwenyewe ukute amesacrifice mengi na kumvumilia baba yako ili tu wewe uwe kijana mweny maisha mazuri. Mama zetu wangeamua kufuata mioyo yao na kukimbia majukumu yaonkisa kero za wenzi wao am telling u wengi tungesuffer na kuishia kuwa machokoraa.

Yaaaani umeongea kitu kizuri sanaaa big up
 
Inawezakuwa ni haki yako kumchukia mwanamme wa aina hiyo lakini kumbuka watoto bado wanahitaji urafiki na baba yao bila kujali yaliyotokea nyuma (ni hulka ya binadamu kutaka kujitambulisha (identified) na baba yake kama ilivyo kwa mama). Swala ni serikali inatakiwa itunge sheria za kuwalazimisha wazazi (awe mme ama mke) ambao hawaishi na watoto kuchangia gharama za kuwalea. Nchi nyingi duniani zinafanya hivyo, sijui kwa nini CCM miaka yote hiyo hawajaliona hilo!

Huyo mwanaume kama alijua anahaki ya kuwa identified kama baba kwanini akimbie?
kama alikimbia na mimi pia
Naikimbia historia yake kama alikuepo katika maisha yangu
Mtoto akiuliza namwambia ashakufaga enzi za vita vya iddi amini..hhhhaaa sicheki kama mazuri
Ila inakera sana
 
Hili suala ni la pande zote. Tumesahau akina dada wanaotupa watoto jalalani?

Tatizo ni ukosefu wa afya ya uzazi. Unakuta binti anazaa na mtu bila kutarajia. Mfano, kama umehiari kuzaa, utakuwa na mpenzi mmoja kwa wakati mmoja. Wanaume wanakuwa wabishi sana kukubali mimba au mtoto inapotokea masela kibao wamepiga.

Pia wanawake muache kubambikiza wanaume mimba/watoto. Mimi binafsi nimetaarifiwa kuwa mtoto ni wangu miezi mitatu baada ya mtoto kuzaliwa. Miezi mingine hiyo alikuwa analea jamaa mwingine alikuwaamebambikizwa. Jamaa aliposhtuka akakata matumizi ndo nikatafutwa mimi. Nina mpango wa kufanya DNA maana na mie yawezekana nimeingizwa mjini.
 
mi siwaelewi ivi inakuweje unazaa na mtu hamjapanga maana raha ya mtoto ni kujipanga sasa utakuta mtu anashika mimba uajielewi na wakati mwingine ilikuwa mechi ya kirafiki tu unategemea ukishika mimba huyo mtoto atakuwa na maisha gani ndio matokeo yake mtu anakimbia kwa sababu hakujipanga
 
Sasa kwa mfano,mtu umexaa nae na huna mpango wa kumuoa...anakwambia kama mimi hunioi basi haina haja ya kumpenda mwanangu..fata maisha yako na sihitaji matunzo ya aina yeyote huyu mtoto hana baba..wewe utafanyaje??

Si bora upige kimya??
 
Ahahahahaaaaaaaaaa-mkuu kumbe hiki kitu tuko wengi,..mimi anahangaika mara huku mara kule nilishamwambia na kumuapia kamwe hatapata senti tano yangu maake kila kitu nafanya lakn ansema anataka kunikomoa sababu sijamuoa yeye.
Eti oooh,..dada yangu anafanya kazi ustawi wa jamii-nimemwambia nenda,...ila niko tayari kuacha kazi sio kumpa hela.

Duuuuuu tuko wengi japo mm iko tofauti kidogo,yangu inahitaji uzi mzima kabisa.
 
Nilisema Hapa Kuna Aina 2 Za Ndoa.
Ndoa Ya Kutungua,yaan Isiyo Na Mipango Sahihi Ambapo Ni Sawa Na Kutungua Nguo Dukani Kwa Sbb Umeiona Inavutia.

Na Bado Mabinti Bila Kumrudia Mungu Mtaachiwa Sana Watoto. Weka Msimamo Wa Kutokutana Kimwl Mpaka Ndoa.
 
Niliwahi Kusema Hapa Kwamba Kuna Aina 2 Za Ndoa, Ndoa Ya Kutungua,na Ndoa Ya Mashono.

Sasa Na Hayo Ndio Madhara Ya Ndoa Ya Kutungua, Binti Umeshindwa Kulinda Thamani Yako Mnatunguana Tu Kama Nguo Ya Mtumba.
 
Hamjui kwa nini hali hiyo hutokea.si kukimbia majukumu bali kero za mwanamke humfanya mwanaume akimbie tena wanawake wengine wakishajua kuwa umezaa nao ni wasumbufu sana mfano huo umenitokea mimi mwenyewe.mwanangu nampenda ila mama yake ni matatizo ikabidi nikimbie ila matunzo kila kitu napeleka ingawa pia bado mpaka hapa kero hazijaisha bado,bado anasumbua juzi amesema anataka aende ustawi wa jamii sasa sijui ataenda kusema nini maana kama matunzo napeleka na kodi namlipia.nimemuonya kuwa mshahara wangu ni mdogo sana kama wataenda najua kuwa kitakachofanyika ni kuangalia napata mshahara bei gani na yeye achukue bei,nahisi itakuwa vizuri akienda kwani hasara itakuwa kwake.maana mshahara wangu ni laki 250000 lakini mimi.humpaga kwa wiki sh 70000 usiulize hela natoa wapi mimi ni mchakalikaji

Ni kuhakikisha wanaume hampati watoto nje ya ndoa kwani si rahisi kutunza watoto huku na huku. Kwani huyo ukimpa 70,000.000 na mwingine 70,000.00 nk ni ngumu! Halafu ikumbukwe matunzo ni zaidi ya pesa. Aidha msisingizie mambo ya tabia ndio yanasababisha. Ukileta kiumbe duniani wajibu wako kukitunza regardless tabia ya mama!
 
Back
Top Bottom