Tabia ya Vyombo vyetu vya usalama kujichukulia sheria mkononi

Tabia ya Vyombo vyetu vya usalama kujichukulia sheria mkononi

BaloziWaMitaa

Member
Joined
Aug 14, 2017
Posts
13
Reaction score
36
Tabia ya Vyombo vyetu vya usalama kujichukulia sheria mkononi imekuwa zoefu kwa miaka mingi sasa,na hasa pale linapotokea tukio la mmoja wao kukorofishana au kudhuriwa na Mwananchi katika mazingira Fulani.

Wamekuwa wakijikusanya na kuingia mtaani kupiga watu hovyo bila kujali nani alihusika au nani akuhusika,wamekuwa wakipiga yeyote wamuonaye mbele yao,awe kijana au mzee pasipo kujali mzima kiafya au mgonjwa.

Lakini sasa linapotokea tukio la mwananchi wa kawaida kudhuriwa katika mazingira yafananayo na hayo wala hawana muda wa kuhangaika au kumhangaikia mhanga /wahanga mpaka mhusika ajiongeze mwenyewe na kwa gharama zake ikibidi.

Hivi utaratibu na sheria zilizopo walijitungia na zinafanya kazi kwa ajili yao tu? Ubabe wenu mnaodhani ni Mdogo Mdogo madhara yake yatakuja kuwatokea puani,fanyeni kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Ninyi hamna cha ajabu na ziada kuliko watanzania wengine zaidi ya dhamana ya kikazi waliyowapa watanzania hao hao mnaowanyanyasa.
 
Mkuu;
Kulikoni mwenzetu ni nini kilikukuta? Usiugumie maumivu tu, sema hao wakuu wakusikie. Mh Mwinyi ataambiwa nini hapa sasa?
 
Kwan mkuu walikufanya nn hao , nawe uliwakosea nn maana sio kwa povu hili .
 
Ndio maana kuna kipindi akiuawa askari, raia wengine wanacheka na kisha serikali inawakamata. Mfano lile tukio la Staki Shari.

Hii ni moja ya sababu inayochochea ugomvi kati ya raia na askari.

Wanakera zaidi pale ambapo wanakuja kumkamata mtu. Hata kama amekubali kukamatwa, atarambwa tu walau makofi kadhaa.

Jeshi lijitathmin, liheshimu utu wa Mtanzania na hakika litaheshimika na kupendwa na raia.
 
Nyie mnaomuuliza mleta bandiko ina maana hamjui kilichotokea ukonga jana au?
Mnamwambia anatoa povu hivi mna akili kweli?
Mnaona wanachofanyaga askaro ni sahihi?
Sheria ipi inaruhusu askari kuwapiga raia hovyo tena wapita njia,wazee,vijana mpaka wanafunzi?
Kuna siku raia watachoka na kitakachotokea sijui itakuaje,
mbaya zaidi askari wengi wanakaa uraiani tofauti na kenya.
Ukiijua historia ya ghana kuhusu askari kupiga raia mnaweza mkaelewa
 
Kuna mwenzako alipigwa mbele za mke wake na mama mkwe wake... Kwa kifupi wote walipata kichapo... Alikuja hapa jana!!
 
aiseeh sio fair lakini
NI kosa kuuwa mtu lkn wao wasichukue sheria mkononi kupiga watu!wangefata taratibu kuwatafuta waliyotenda kosa hilo!
Kuna mdau humu jf alisema alitembezewa kichapo mbele ya mke wake,Mama mkwe na watoto wake....
Mpaka ikifika 2020 vilema wataongezeka alafu nashangaa hakuna kiongozi aliykemea kitendo hicho Mpaka sasa!

Ova
 
Daaa ni udhalilishaji na unyanyasaji polisi wamewafanyia wananchi wenzetu naagiza IGP awachukulie hatua mara moja wapumbavu Hao.
 
NI kosa kuuwa mtu lkn wao wasichukue sheria mkononi kupiga watu!wangefata taratibu kuwatafuta waliyotenda kosa hilo!
Kuna mdau humu jf alisema alitembezewa kichapo mbele ya mke wake,Mama mkwe na watoto wake....
Mpaka ikifika 2020 vilema wataongezeka alafu nashangaa hakuna kiongozi aliykemea kitendo hicho Mpaka sasa!

Ova
Huo udhalilishaji waliofanya sio mzuri kiukweli na sio jambo la kuvumilika...Chuki baina ya raia na polisi ndio huanza hivihivi yaani jambo ambalo sio zuri...wao ndio wanapaswa watulinde lakini inakuwa tofauti
 
Hata wale majamaa wa mabaka mabaka nao wakifanya hivi mtalalamika mitandaoni au kwa kuwa hawa ni polisi tu?
 
Back
Top Bottom