Tabia ya Shemeji yangu

Maserati

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2014
Posts
11,602
Reaction score
20,101
Jamani wana MMU yamenikuta,

wiki hii nilipanga nikutane na shemeji yangu wa kiume, yaani ndugu wa damu wa mpenzi wangu. Nilitaka kukutana nae maeneo ya ubungo stand ili aweze kunipa funguo ya nyumba ya mpenzi wangu ambaye kwa sasa yupo safarini nje ya jiji na baadhi ya vitu ambavyo alikabidhiwa na kaka yake siku ya safari yake na wakakubaliana ataniletea. Hapo nyuma tulikubaliana siku fulani hivi kuwa aniletee lakini nilichoma sana maindi ama kuuza nyago bila ya shemeji kutokea na kwenye simu hakuwa akipatikana hewani wakati aliniambia anakuja, nilisubiri kama masaa mawili hivi.nilichukia sana lakini nikamsamehe na kukubaliana tukutane siku nyingine aweze kuniletea vile vitu.

Wiki hii sasa,

Tukakubaliana avilete vile vitu hapo ubungo stand na nilimpa tahadhari ya kujali mida kwani siku hiyo nilikuwa na sehemu zingine za kwenda, so on time awe amefika na yeye akahafiki hilo na kukubaliana iwe saa 5 asubuhi.basi on time bidada nikafika zangu ubungo na kumpigia kumjulisha kama mimi nimekwisha fika.

1-alichelewa kupokea simu kama mara 2 hivi na alipopokea akasema yupo njiani anakuja, nilipo muuliza yuko wapi akasema hajui wapi. Nikapata wasi wasi kwa kauli yake hiyo, nikampigia mpenzi wangu na kumuomba amuulize mdogo wake yuko wapi.kweli akatekeleza akanipa jibu lililonikera, kwamba ndo anatoka nyumbani maeneo ya buguruni kwa shangazi yao.

Nikavuta muda kama dak.15 nikampigia nikamuliza tena umefikia wapi akanijibu nipo river side na nimpe kama dak.10 atakuwa amefika.nilikuwa makini sana na muda wangu lakini nilipochek time ilikuwa saa sita mchana.nikamvumilia lakini mpaka saa sita na dak.20 hakuwa amefika.nikamtumia sms nikamwambi kama upo mbali sema mm niendelee na my schedule akasema hayupo mbali nimsubiri, nilikaa mpaka dak30 ya saa sita hakuw amefika.

Sasa ikawa inaelekea saa saba kasoro, kw kuw nilikuwa nimeshachelewa event moja nika I cancel lakini hii nyingine nilishindwa kui cancel nikamwambia "nakuomba shuka hapo ulipo na urudi kwani mimi sitaweza tena kukusubiri ninachelewa sehemu nyingine, hivo vitu viweke na atakuja kuvichukua kaka yako.hakunijibu basi mimi niakondoka zangu.saa saba anatumia sms eti nimefika uko wapi, nikamjbu niliko magomeni hospital.

Akaanza kupanic na kunitumia sms mbaya.of coz mimi ni binadamu na nina hisia pia, na kwa kuwa alikuwa amekwisha nikwaza basi tulijibishana kwa sms na alishanitukana lakini mimi sikumjibu sms za kumtukana but nilimjibu kumuonyesha ni jinsi gani alinikera.

Nina hofu kwa mpenzi wangu kwa hili lililo tokeA, atanielewa kweli. ?? Kwasababu nilivo mwambia akasema siwezi liongelea hili kwa sasa nisubiri nirudi.yeye anarudi week ijayo na sku zilizofuata baada ya tukio tumekuwa tukiwasiliana kama kawaida.
Kiukweli nina wasi wasi. .
 
Twin...
Umeishiwa bundle nini?? Hebu sema fasta nkutumie kwa mtandao gani??
 
sasa wasiwai wa nini?

waswahili mbona tuna shida?
umsubiri mtu saa nzima halafu akutukane na uwe wewe una wasiwasi?

mimi hata mama yangu mzazi simsubiri saa nzima......

ukijiendekeza utakuwa 'a doormat kwa watu'
kila mtu atakusubirisha masaa kadhaa...kila wakati..
tell them to go to hell wote mtu na mdogo wake...
 
utaeleza ilivyokuwa.PERIOD!
huyo dogo asikuumize kichwa !
halaaafu huyo jamaa yako anapenda keeesi enh?
ishu nyepesi hivyo anaiweka pending ati msubiri arudi ndo muongee!
dah!
jiandae kuwa na unnecessary conflicts if at all huyo ndo mume mtarajiwa!
 
Kwa maelezo hayo kama huja yachakachua then huyo mpenzi wako hana sababu ya kukukasirikia wewe,unless kama mpenz wako ni wale wanao endeshwa na ndugu bila kujali uhalisia wa jambo.

Jambo la pili,ndugu yangu hana mamlaka ya kumtukana mpenzi wangu,hata kama ana makosa.Kwahiyo alitakiwa kulikemea hilo kwanza bila kasubiri arudi.Kwa hili nina wasiwasi jamaa atakuwa ni type ya watu niliotaja hapo juu
 
utaeleza ilivyokuwa.PERIOD!
huyo dogo asikuumize kichwa !
halaaafu huyo jamaa yako anapenda keeesi enh?
ishu nyepesi hivyo anaiweka pending ati msubiri arudi ndo muongee!
dah!
jiandae kuwa na unnecessary conflicts if at all huyo ndo mume mtarajiwa!

No, nadhani pengne haitaj unfair decision coz yuko mbal.nam nmeanza kumueleza kwa kumuulza baadh ya vtu ambavyo mdogo wake kanlopokea..
 

Na huyo mdogo wake nishawah skia habar zake.huwa haziend na kaka ake.yaan dak.2 mbele..hayupo hvo mpenz wangu.n mskivu na anapenda kutoa fair decision
 

Not to my puppy..I can't let him go..uzur wake naujua mm.na ana meng madhur na madhaifu ya kuhesabka.n mskvu sana hata kwenye decision making yupo in leizzure affair
 
Not to my puppy..I can't let him go..uzur wake naujua mm.na ana meng madhur na madhaifu ya kuhesabka.n mskvu sana hata kwenye decision making yupo in leizzure affair

mapenzi ni utumwa hiyari.....so enjoy tu ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…