Tabia ya kuleta picha mbaya na kusema "TYPE AMEN", nani aliianzisha?

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Hivi karibuni kumezuka tabia ya kuweka picha mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, picha ambazo zinaonyesha mtu ana matatizo fulani hasa magonjwa ya Cancer au mengineyo, au mtu ameumia katika ajali mbaya n.k. halafu kunakuwa na tu'vimaelezo halafu unaambiwa TYPE AMEN..utabarikiwa sijui itakuwaje!
Anyway hoja yangu haina lengo laa kuingilia imani ya dini yoyote lakini, swali ni kwamba, Ni nani anafanya hivi na kwa masilahi ya nani? Kama tulitaka kumsaidia muathirika basi bora ingewekwa akaunti namba kwamba watu wachangie, au useme tu watu wambwombee mhusika apate nafuu kila mtu kwa imani yake.
Huwa nakereka sana maana picha zinazowekwa sio tu za kutisha lakini pia nna uhakika haziwi na ridhaa ya wahusika...na hii ni Unethical kidaktari, kibinadamu na pia kimungu.
Nimesikia sikia kwamba kuna watu wenye imani zza kishetani ndo huwa wana fanya hivi na hizo AMEN mnazotype na SHARING na LIKES zinawaongezea vyeo huko ushetanini....
Wajuzi mje mtujuze tafadhali
cc. Mshana jr.
 
Ni biashara kwa ninavyojua zile likes na comments
That is business haswaa, unaona kuna likes laki ngapi na comment malaki hapo, that is how smart people makes business..

ukishalike au kucoment baada ya muda watakuletea matangazo yao..unashangaa hili tangazo linahusiana vp na ww.
 
Nazani ukiwa na visitors wengi inaonesha watu wa Facebook wanakulipa ndo maana hao washenzi wanakuja na gia hiyo.
 
Hivi karibuni kumezuka tabia ya kuweka picha mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, picha ambazo zinaonyesha mtu ana matatizo fulani hasa magonjwa ya Cancer au mengineyo, au mtu ameumia katika ajali mbaya n.k. halafu kunakuwa na tu'vimaelezo halafu unaambiwa TYPE AMEN..utabarikiwa sijui itakuwaje!
Anyway hoja yangu haina lengo laa kuingilia imani ya dini yoyote lakini, swali ni kwamba, Ni nani anafanya hivi na kwa masilahi ya nani? Kama tulitaka kumsaidia muathirika basi bora ingewekwa akaunti namba kwamba watu wachangie, au useme tu watu wambwombee mhusika apate nafuu kila mtu kwa imani yake.
Huwa nakereka sana maana picha zinazowekwa sio tu za kutisha lakini pia nna uhakika haziwi na ridhaa ya wahusika...na hii ni Unethical kidaktari, kibinadamu na pia kimungu.
Nimesikia sikia kwamba kuna watu wenye imani zza kishetani ndo huwa wana fanya hivi na hizo AMEN mnazotype na SHARING na LIKES zinawaongezea vyeo huko ushetanini....
Wajuzi mje mtujuze tafadhali
cc. Mshana jr.
Umenena vyema mkuu, unajua watu kwa kukosa knowledge of God and self wanadhani Mungu anaishi Facebook, Twitter and various forums. Wamekua wakitumia picha wasizojua chanzo chake kwa vitisho na kuaminisha watu kuwa ni uumini au kuwa mwenye imani kwa ku-type "Amen" or else if u don't type Amen or 4ward 2 others u will b cursed or befellen with a calamity. Huu ni upuuzi uliotukuka wa church goers.

Thanks for highlighting this matter
 
Bahati nzuri mimi nimelijua hilo tangu nikiwa shule ya msingi. Kulikuwa kuna barua za Mt Yuda Thadei zinasambazwa ukipokea na wewe unatakiwa kuandika tisa na kusambaza kisha unaomba unachotaka, usiposambaza unapata mikosi sijui Miaka saba... Sister anayefundisha dini alipoziona akasema waambie wote walioandika wazilete mimi nazipeleka kanisani zikaombewe basi tukakusanya fasta. Kisha akatuambia nakwenda kuzichoma moto huu ni upuuzi kama unataka kusali novena au maombi maalumu zipo sala lakini sio kusambaza barua. Leo ninapoona sijui usipo type Amen utapata mikosi naona he! kumbe bado wapo waliochelewa!
 
Kiukweli binafsi huwa inanikera Sana,kujinufaisha kwa kutumia tatizo la mtu,sijui huwa kinawafurahisha nini kupost kilema cha mtu na kutunga vijineno vya uongo,me huwa nawambia " kama hiyo pic imekufurahisha na yakupate"
 
Back
Top Bottom