Tabia ya CCM kucheza Rafu Kwenye Chaguzi Mbalimbali Za ndani na Nje ni Ya Kihistoria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabia ya CCM kucheza Rafu Kwenye Chaguzi Mbalimbali Za ndani na Nje ni Ya Kihistoria

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by payuka, Nov 2, 2010.

 1. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama mtaikumbuka vizuri historia katika chaguzi mbalimbali zilizoihusisha CCM, ndani na nje ya chama chao hawa jamaa hawajawahi kufanya uchaguzi wowote ulioisha salama bila tuhuma zozote.
  Walianza Kwa Kuchakachua ndani ya chama chao kwenye Kura za maoni, waliwanyima haki wale walioshinda kwa Kuchaguliwa kihalali na wananchi. Matumizi mabaya ya fedha ili kufanikisha Rushwa zao yalishika nafasi kubwa sana katika mchakato ule.

  Ni taswira hii hii ambayo imejirudia kwenye uchaguzi mkuu, matumizi ya pesa na ubabe ndo yamechukua nafasi. Wameshindwa kuheshimu maamuzi ya wananchi kwa tamaa na uchu wa madaraka. Wasidhani Wananchi ni wapumbavu walivokaa kimya.

  Nahitimisha kwa kusema hakuna jambo lisilo na mwisho, Ipo siku!!
   
Loading...