Tabia mbaya kuliko

Tabia mbaya kuliko

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,822
Reaction score
140,857
Wakuu hii ni tabia inayotufanya hata tukose baraka za wazazi,ni tabia mbaya sana.Hiki kiungo kimetufanyia mangapi mazuri?hayahesabiki,sasa kwa nini tunafikia huku?
Kama unataka kumtusi mtu kwa nini Kiungo Nyeti cha Akina mama kinatumika?ujue kila Binadamu walikuja Duniani wamepitia hapo ni Mlango wa kuja Duniani Mbona watu wanauzarau sana ! Hiki kiungo cha Mwanaume Mbona hakitumiki kwenye kutusi watu?
 
Wakuu hii ni tabia inayotufanya hata tukose baraka za wazazi,ni tabia mbaya sana.Hiki kiungo kimetufanyia mangapi mazuri?hayahesabiki,sasa kwa nini tunafikia huku?

Kweli aisee af watu wanaona raha tu hata hawajistukii
 
Usikie sasa mama anavyotumia kiungo chake mwenyewe kwa mtoto wake
 
Vijana wengi wanalalamika kazi, maisha magumu ila hilo tusi la kumtukana mama ndio lipo karibu kuliko chochote, ndio laana zenyewe hizo.
Sipendi mtu anayetumia hilo tusi hata wadada now days wanalitumia sijui ndio waonekane wajanja, wakati ni mambulula tu.
 
Wana laana hata ukiangalia wengi wa hao wanaolitumia ni mirembe product
 
Mi mtu akinitukana namwambia ahsante hicho kiungo ndicho ulichopitia humo leo unaleta nyodo
 
kutukana si kuzuri km busara ipo kutamka hilo neno ni zito kutoka mdomoni...
we need to change

japo watu wa stend,migodini, hospitali nk. matusi ni kiunganish cha sentensi
 
Wakuu hii ni tabia inayotufanya hata tukose baraka za wazazi,ni tabia mbaya sana.Hiki kiungo kimetufanyia mangapi mazuri?hayahesabiki,sasa kwa nini tunafikia huku?

kiungo cha mwili kikitajwa ni tusi ??umetumia sheria gani kuhamisha kiungo kuwa tusi
 
Wanaotumia wabadilike coz si vizuri na hakuna gharama kuacha kutumia kauli mbaya
 
Wanaotumia hilo neno mimi huwa nawashangaa sana, maana wanamtukana na kuwadhalilisha wazazi wao hasa mama zao. Na asilimia kubwa ya wanaotumia hayo maneno ni Mirembe Product kama alivyosema bibi.com ukiwa na akili timamu na busara huwezi kutoa neno lolote baya asilani. Badilikeni jamani!!!!
 
kwanini jina la kiungo liwe tusi?

kwanini liwe baya?

udhalilishwaji uko wapi kusema neno la kiungo?
 
Mbona wote mnaituhumu nafsi ya tatu sasa wanaotumia hilo neno ni watu gani?
 
kwanzia leo ntakuwa natukana hivi, macho ya baba ako...
 
wanakosana busara na kumtukana mama....nachukia sana na unakuta wengine ni watu wazima wazee ila busara ndo sifuri
 
Back
Top Bottom