SWEETEST
Member
- Jul 17, 2013
- 26
- 4
Habari zenu wana MMU. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikijiuliza swali hili na wakati mwingine nikijipa majibu labda tatizo ni ...au.... bila kupata majibu ya uhakika ndio maana nimeamua kulileta kwenu kwa michango zaidi. Kumekuwa na tabia ya wanandoa (baadhi na si wote) kutoheshimu ndoa zao kwa kuamua kuwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa. Kama ni mume basi anakuwa na mwanamke mwingine nje ya ndoa na kama ni mke anakuwa na mwanaume mwingine nje ya ndoa ambaye watahusiana katika maswala ya kimapenzi. Tabia hii imeshamiri sana na sidhani kama ni tabia njema kwa afya ya ndoa na familia kwa ujumla. Je unafikiri tatizo hili linasababishwa na nini? Na kama ni tama kwa nini mtu aliamua kuoa au kuolewa si angeamua kuishi mwenyewe bila kuwa na mume au mke? maana wakati mwingine limekuwa likisababisha majeraha kwenye moyo wa mke au mume aliyetendwa pale inapokuja kugundulika kuwa mmoja wapo si mwaminifu na huwaathiri watoto pia. Karibuni kwa michango na nini kifanyike ili tabia hii isiendelee?