Tabia hii tatizo ni nini?

Tabia hii tatizo ni nini?

Uhusiano wenu ulianza vipi?

Ulimng'oa mtu ili wewe upate kushika hatamu?

Historia ya mtu huyo unaifahamu vizuri?


Je, ulimpa expections kubwa kabla ya ndoa lakini baada ya ndoa kakuta si vile alivyotarajia?

n.k

wenye tabia au vigezo visivyostahili wataolewa na nani?
 
Kiukweli suala hili lipo na linasababishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na haya yafuatayo.
1. Watu huingia kwenye ndoa na mtazamo usio sahihi juu ya ndoa na huanza tangu wakati wa uchumba, unakuta watu hutoa ahadi za uongo, kuishi maisha ya uchumba tofauti na uhalisia, kuendesha mahusiano kihisia/matamanio kuliko upendo, kupuuzia kasoro ndogondogo ambazo ni za msingi kurekebisha kabla ya ndoa kwa hofu ya kumpoteza mwenza.

2. Muda wa uchumba kuwa mfupi ama mrefu na hivyo kusababisha watu kuwachoka wachumba wao wa muda mrefu kisha kuwaacha na kuoa wachumba wa muda mfupi hata bila kufanya uchunguzi wakutosha, hii husababisha mapungufu mengi kuibuka wakati wa ndoa na hivyo mtu kuona bora awe na mwenzi mwingine ili kupata faraja na amani ya moyo.

3. Ubinafsi na tamaa, mtu aliyekua kiakili na akaamua kuoa anatakiwa aridhike na mke/mme aliyenaye na anatakiwa kutambua kuwa mkewe/mewe ndiye mzuri kuliko wote waliopo ndiyo maana kaoa/olewa nae, cha msingi ni kuboresha muonekano wake ili azidi kuvutia zaidi. Wazuri huwa hawaishi hivyo ni bora kuridhika na kumpenda wa kwako.

4. Visasi, baadhi ya watu wanapenda sana kulipa visasi, hivyo mwenza wake akimsaliti naye husaliti vilevile, hii husababisha mvurugano na amani kutoweka na mwishowe thamani ya mweza huisha, mvuto haupo tena, hisia nazo huyeyuka kama barafu na kusababisha gazi katika mapenzi. Mtu huona ni bora awe na mtu wa kumpa raha maana hapati raha hata akiwa na mwenza wake.

4. Kumwacha Mungu; Hili ndilo tatizo kubwa pale tunaposahau kuwa Mungu ndiye mwanzilishi wa tasisi ya ndoa, tunapoendekeza tamaa na kumwacha Mungu lazima uchafu uibuke katika ndoa. Mungu anatakiwa kuwekwa mbele ili ndoa iweze kustawi, hapa simaanishi kwenda kanisani/msikitini tu, bali ni kumkubali MUNGU pasipo unafiki na kumkabidhi aongoze tasisi hii muhimu ya ndoa.

5. Hitimisho: Maandalizi mazuri ya uchumba ndio msingi imara wa ndoa, ukikosea kuendesha uchumba vizuri badala yake ukajikita kwenye matamanio ya pesa, uzuri wa sura, maumbile na vitu visivyokuwa na tija siku ukiingia kwenye ndoa utagundua mambo ni tofauti ndipo unapoanza kushituka na kugundua umebugi, matokeo yake ni usaliti, magonvi, mashitaka na vilio visivyokoma.
Mungu awasaidie ambao hawajaoa/olewa wafanye maamuzi sahihi maana wakati ni huu, na wale tulio oa basi tumrudie Mungu nae ni mwingi wa rehema atatupokea na kutusaidia kuongoza ndoa zetu kama tutakuwa tayari. Mambo ni mengi ya kuzungumzia ila naomba nisiwachoshe.
 
1. Tamaa
2. Malezi mabovu (ya kujilea vile upendavyo au uliyolelewa na wazazi wako)
3. Kutokuwa na hofu na Mungu
4. Kufuata mkumbo, rafiki yako ana nyumba ndogo na wewe unakurupuka kuitafuta
 
Sababu nyingi na za ukweli zimetolewa na wasemaji mbali mbali hapo juu. Lakini wanasahau sababu moja muhimu sana ambayo husababisha wanaume kutoka nje ya ndoa, nayo ni:- Wanawake kujisahau na kubweteka baada ya kuolewa. Tukishaolewa tunadhani ndiyo tumemaliza kazi, hivyo hatuna muda tena wa kumdekeza mwanaume na kumuonyesha mapenzi moto moto kama tunayokuwa nayo wakati wa uchumba. Hili humfanya mwanaume aamue kutafuta pengine pa kudekezwa, maana mwanaume ni kiumbe dhaifu na anahitaji kudekezwa kuliko hata mtoto mdogo.

Mpe mmeo haki zake na umtambue kama yeye ndiye kichwa cha familia uone kama atafurukuta hata siku moja. Utaishia kusingiziwa kwamba umemlisha limbwata kumbe ni treatment tu.
 
Mimi nafikiri ukiruka stage wakati unakua..labda kipindi cha mihemuko wewe ukiwa unafanya zile unapenda desa(kusoma) sana ukifikia stage flani hivi mambo uliyoruka na vitu ambavyo hukuwahi kua navyo(i.e pesa kimtindo, ndinga la ukweli kiasi, simu la ukweli kiasi, pamba za ukweli) inarudi nature sasa ile stage uliyoruka sasa ndo inajirudia..sasa...
 
.... Hahahahaaaa...! Sidhani kama atakuruhusu ukagongwe! Vile vile sidhani kama ungeridhia njia yoyote anayokushauri ikiwa hiyo njia haitakuridhisha!!!! .... Embu tugeukie upande wa pili! Kama mwenzio yuko fresh, wewe haukofreshi (huwezi ku-do)
Likinifika nitakujibu.
 
wenye tabia au vigezo visivyostahili wataolewa na nani?

Umesema hawastahili halafu unauliza waolewe na nani?

Mmmmmmmmmmhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!

Sasa kama hawastahili wataolewa vipi?
 
Back
Top Bottom