Tabia ambazo hujenga mataifa

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kuna tabia ambazo hufanya mataifa kuendelea na kuna tabia ambazo zikiwepo katika mataifa, kamwe watu hao hawatoendelea. Jamii zozote ambazo zina thamini familia na mahusiano yao katika jamii, na malengo yao ya pamoja kama jamii na kama taifa, lazima watu hawa wapige hatua. Kinyume cha hapo jamii zinazofuata ubinafsi kupiga kwao hatua ni vigumu mno. Umoja wa nchi katika mataifa ya aina hii hupungua na malengo yao ya pamoja huyayuka. Umoja katika malengo ni nguzo ya maendeleo ya taifa lolote.

Utulivu katika mataifa yeyote unategemea sana usimamizi wa misingi ya haki na maadili ya taifa. Maadili yanapomong'onyoka katika taifa; hakuna amani na hakuna maendeleo. Kwasababu maendeleo yeyote katika taifa yanahitaji utulivu. Sio tu kutokuwepo na vita katika taifa bali utulivu wa kiakili na kiroho. Na utulivu huu unajengwa katika mahusiano yetu.
 
Back
Top Bottom