Tabata Dampo wahoji Lubuva kurejeshwa kazini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabata Dampo wahoji Lubuva kurejeshwa kazini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Dec 26, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Date::12/25/2008
  Tabata Dampo wahoji Lubuva kurejeshwa kazini

  Geofrey Nyang’oro na Latifa Karugila
  Mwananchi

  WAKAZI wa Tabata Dampo na Profesa wa Sayansi ya Siasa, Mwesiga Baregu wamesikitishwa na kitendo cha serikali kumhamishia Shinyanga aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala John Lubuva, wakisema kitendo hicho ni mwendelezo wa serikali kuwalinda mafisadi.

  Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti, walisema kitendo hicho kinaifanya jamii iamini serikali ilihusika katika uzembe wa kuwabomolea nyumba wakazi wa Tabata. Wakazi hao wa Tabata Dampo walisema haliwaingii akilini kuona mkurugenzi huyo ambaye alisimamishwa kazi kwa tuhuma anarudi madarakani bila maelezo ya kina.

  “Kamwe haiwezi kutuingia akilini kama kitendo alichokifanya Mkurugenzi huyu cha kuruhusu bomoabomoa ambayo hata serikali ilikiri kuwa ni haramu leo awe amesharudishwa kazini,”alisema Mohammed Makalani. Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina na Sudi Juma, alisema kitendo cha mkurugenzi huyo kurudi tena madarakani haraka hivyo kinawanya waanze kutilia shaka dhima ya utawala bora seriakalini.

  Naye Profesa Baregu ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , alisema serikali ilipaswa kuelezea wananchi juu ya hatua ilizozichukua kutokana na kutuhumiwa kwake kuhusika na bomoabomoa hiyo kabla ya kumpangia kituo kingine cha kazi. Alisema kitendo cha Lubuva kuwa kazini huku suala lake likiwa bado limefunikwa na utata, kinaleta hisia kuwa watendaji wenye nafasi za juu serikalini wanalindana.

  “Jambo hili ni kubwa na lilishajulikana kwa wananchi serikali ilipaswa kuwataarifu wanachi juu ya kila hatua zilizochuliwa kabla ya kumpangia kituo kingine cha kazi ili kuwaondolea hofu wananchi na kuwafanya wawe na imani na serikali yao,”alisisitiza Profesa Beregu. Sakata la bomoabomoa nyumba za wakazi wa Tabata Dampo, lilitikisa nchi mapema mwaka huu na serikali kulazimika kulipa fidia ya sh 20 milioni kwa kila nyumba.
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Yaani bongo kwetu ni mwendo mdundo. Hata brother Dito kabla hajawa mgeni wa malaika tulishuhidia akiwa mjasiriamali wa nguvu wa kusafirisha asali uarabuni! Na kuhutubia mikutano ya hadhara! Hii ndiyo bongo mambo yote yanaendeshwa na TECHNICAL KNOW WHO!
   
Loading...