Unapoiona semi inayoyoma barabarani, sifa sio kwa dereva pekee.
Unapoona gari la abiria limefika salama safari yake sifa na shukrani sio kwa dereva pekee.
Unapoona hesabu ya tajiri imetimia tambua nyuma ya dereva kuna msaidizi muhimu almaarufu kama konda ama kwa Kiswahel sanifu, utingo.
Makonda (sio mabarcity) ni watu muhimu sana kwenye tasnia nzima ya usafiri. Kwenye magari ya mizigo ndio wasimamizi wa kupakia na kuhakikisha mzigo umefungwa vema.
Ndio wanaosimamia
service ya gari, ndio wanaojua shida zote za gari hata inapopata pancha n.k n.k, na hata dereva anapochoka ama kwenda kuosha rungu kwa mpango wa kando utingo ndio hubaki na gari.
Mabus ya mikoani tunajua dhima kubwa ya makonda kuanzia kupakia abiria mpaka ku-
overtake barabarani na matangazo yote safarini na dharura.
Kwenye daladala zetu ndio unaweza kuona nguvu halisi ya makonda. Yeye ndio wa kuamrisha gari isimame ama itembee ni mshika pesa ni mpanga matumizi nk nk.
Chini ya makonda ndio kuna wasaidizi wengine wote inapotokea kutoelewana kati ya konda na dereva mambo huenda kombo. Ni wakati wa uchaguzi, kila chama kimeshapata dereva wake, na kila dereva atakuwa na utingo wake na kila utingo atakuwa na wasaidizi wake.
Wakati vyama vingine vikionekana kujipanga vema kitimu na kuwa wamoja, chama tawala kina makunyanzi mengi. Makonda na wasaidizi muhinu wanaonesha wazi hawana furaha ama hawako pamoja na dereva wa jahazi, makada wote muhimu wako kimya kabisa!
Ninini kitatokea? CCM watachezeshwa segere mwanzo mwisho, watakuwa kama YANGA na SIMBA ama SAULI na NEW FORCE
Viwanjani ni SIMBA, SIMBA, SIMBAA.
Barabarani ni SAULI, SAULI, SAULI.
Nyuma ya tabasabu la JK kuna BM anacheka!